kifupi dada wa kazi hana kazi maalumu, kazi yoyote itakayotokea ni yake, hana mwajiri maalumu, anaweza tumwa hata na mgeni, kingine ni kwamba madada wa kazi wengi nwanapitia aina fulani ya ngono, tuiite ngono shirikishi, yaani asipobanduliwa na baba mwenye nyumba, basi atapitiwa na watoto wenye nyumba, ama wageni wenye nyumba, ama shemeji mwenye nyumba ama jirani mwenye nyumba ama wote hao kwa muda tofauti, yaani anaamka alfajir, analala alfajir kasoro, ama kama kuna mtu anaweza niambia kazi za dada wa kazi za ndani ni kazi gani, na kibaya zaidi wanawake wenzao ndio huwa wanawatumikisha kama wameajiri roboti ndani, ni mara chache sana kumkuta baba mwenye nyumba anamtumikisha namna hiyo mfanyakazi za ndani. kuna baadhi ya nchi jirani wafanyakazi za ndani ni wanaume, mfano Burundi, nimeona wafanyakazi wa ndani kwenye nyumba nyingi ni wa kiume, huyu akichoka amagoma, na akigoma inabidi uinuke ukafanye mwenyewe maana mashine inakuwa imechoka kweli.