Kwako lakini wengine tunaiona kubwa
Sasa 2000 unakuwa huna majukumu mkuu, kijana wa kawaida huitaji kuajiriwa ili uipate 2000 maana ukijiajiri tu hata kwa mtaji wa 5000 unapata si chini ya 3000 kila siku......mfano huu hapa sasa.
1....ukinunua karanga kilo moja shilingi 3500 dukani.
Mkaa wa jero 500, .... ukafunga kwenye vile vimfuko ukapeleka kwa wenye viduka vya mangi au ukatembeza.
unaeza jikuta umefunga si chini ya vimfuko 25. kwa mfano kwenye viduka unamuuzia 350 kila pakiti bei ya jumla..... 350 x 25 =8750
8750-4000=4750 mtaji ulitumia 4000.....
Ukitembeza faidi ni zaidi ila wewe umetarget kuuza karanga zako jumla......sasa mkuu faida ya 4750 kwa mtaji usiozidi 5000 huoni ni bora kuliko kuajiriwa kutwa ukalipwe 2000 kwa siku.....
na hii idea inawezekana kwa kijana aliyeamua kujitoa muda wake kutengeneza karanga safi......
Mifano ni mingi sana mtaji hauzidi elfu 5000 na unapata 5000 nyingine au chini ya hapo kidogo, maana yake ukiwa na shilingi 20,000 ukichangamka kupata 10000 kila siku ni jambo jepesi.
Kuna idea ya biashara ya kijiwe nongwa cha kahawa.....
Atakuja mtu hapa aseme hesabu za makaratasi wakati hii ni real.
Hii kitu nilimpatia wife akafanya tena kwa udogo kutokana na wife ni mama wa nyumbani hili linamsave kupata pesa ya maziwa ya mtoto na hata matumizi yake madogo madogo.....