Kama mtanzania napataje fursa ya kwenda kufundisha nchi kama Shelisheli, Kanada, Norway au Kenya?

Kama mtanzania napataje fursa ya kwenda kufundisha nchi kama Shelisheli, Kanada, Norway au Kenya?

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
2,582
Reaction score
4,554
Wakuu mimi ni mwalimu natamani nikafundishe kati ya Nchi tajwa hapo juu tafadhali mwenye miongozo anipatie hapa jukwaani mimi na wanajukwaa wenye shida kama yangu tutashukuru sana

Ahsanteni
 
Wakuu mimi ni mwalimu natamani nikafundishe kati ya Nchi tajwa hapo juu tafadhali mwenye miongozo anipatie hapa jukwaani mimi na wanajukwaa wenye shida kama yangu tutashukuru sana

Ahsanteni
Ukifanya Content Analysis kuhusu hili bandiko lako utagundua kwamba wewe mwenyewe binafsi inaonekana kuwa haupo serious. Sasa Watu wengine watawezaje kukusaidia ?
 
Canada na Norway wanatumia curriculum tofauti na ya kwetu. Jiandae kwanza kufundisha international curriculum. Hao Norway wanatumia holistic.
 
Kwa mfumo wa elimu ipi mkuu otherwise study za ufundi kama welding, painting driving na nyingine pacha zake na izoo
 
Jamii forums Kuna watu kazi Yao kubwa kukatisha watu tamaa hakuna kitu ambacho hakiwezekani, watanzania tunaweza kuwatumeelimika ila bado tuna uswahili mtu kapost anaulizia vigezo vinavyotumika ili aweze kupata nafasi kama unajua mpe mwongozo sifa Gani anatakiwa awenazo sio kila post lazma comments huwa zinaathiri sana watu
 
Kuna sista kule twita aliweka namna rahisi ya kwenda kufundisha Japan, ngoja niitafute link niiweke hapa itakusaidia.
 
Unataka uende kufundisha somo gani au masomo gani?

Kufundisha norway haiwezekani wanasoma mtaala tofauti na ili uwe teacher kule inabidi usome huko huko then uombe kazi kwa vyeti vyao.
 
Unataka uende kufundisha somo gani au masomo gani?

Kufundisha norway haiwezekani wanasoma mtaala tofauti na ili uwe teacher kule inabidi usome huko huko then uombe kazi kwa vyeti vyao.
Duuh kwahiyo kwa Norway nimeshapoteza vipi hizo nchi nyingine?

Nimespecialize katika somo la Geography na History
 
Back
Top Bottom