Kama mtu anakopa benki 5 tofauti za Tanzania na akaweza kukimbia nchi bila kugundulika ni ishara kwamba TISS na vyombo vingine vimelala

Kama ni hivyo basi wasingetoa taarifa kuwa wameibiwa maana yaonekana wamesindwa kumpata huyo jamaa.

Na hata kama ni binafsi bado mabenki yanawajibika na sheria za masuala ya mabenki na uendeshaji wake.

Hivyo sheria, kanuni na miongozo yote ambayo hutolewa na BOT kupitia wizara ya fedha vyote hivyo vimewekwa kapuni?
 
Ni pesa ya Uchaguzi inatafutwa,

Inatafutwa pesa Ili maskini wakaangwe Kwa mafuta Yao wenyewe.
 
Hawajalala, ni mchongo,

Branch managers wote Wana mfumo uliounganishwa jikoni.

Haiwezekani ipite 5 banks wasijue.
Ziwepo pia taratibu za kuwalinda watoa taarifa "Whistleblowers" na wapewe ushirikiano.

Lazima kuna wale ambao wameambiwa "oyaa saini hapo", na wakaahidiwa kiasi fulani.

Hili suala ni very very serious.
 
Usisahau humuhumu JF watu wanaombaomba tu hela kutwa nzima
 
Hata wewe unaweza ukakopa marekani na kukimbilia Tanzania.CIA sijui TISS siyo mungu na siyo kila kitu kinawahusu.
 
Mkuu huyu aliyetajwa na Raisi hajaiba kakopa kwaiyo anaweza kuzipeleka pesa zake alizokopa Ulaya.
 
Hata wewe unaweza ukakopa marekani na kukimbilia Tanzania.CIA sijui TISS siyo mungu na siyo kila kitu kinawahusu.
Ok ila hiyo ilikuwa ni zamani sana twazungumzia miaka 20 sasa.

Wanigeria ndo walokuwa vinara wa kazi hiyo.

Jaribu sasa hivi uone ule moto kwanza siku umemaliza kukamilisha paperwork wao (benki husika na polisi) hukusubiria ile siku waenda kuchukua mzigo na utasaidiwa kwenda nao kituo cha polisi.

Huwa hawahangaiki sana maana wanafahamu kuwa mjinga ni weye utanasa tu.
 
Mkuu huyu aliyetajwa na Raisi hajaiba kakopa kwaiyo anaweza kuzipeleka pesa zake alizokopa Ulaya.
Ila sasa hivi (kama umenielewa) Ulaya wana sheria kali za kupokea fedha kutoka nje ya bara la Ulaya khasa baada ya mgogoro wa Ukraine kuna regulations nyingi dhidi ya fedha zinoingizwa huko.
 
ndiyo mana nikasema siyo bure hiyo kuna namna.
 
Sijaelewa amekopa bank

Bado unasema Ni pesa zenu? Umeenda ATM ukakosa pesa zako? Kusema kutoka nchini kiulani..kwani mkopo hauruhusu mtu kusafiri je Kama nimekopa nikafanye biashara nje ,, waliokopwa ndo watajua wewe hio elf 30 yako NMB Bado ipo
 
Ni mifumo ya kupata hiyo mikopo ndiyo imekuwa migumu lakini ukishakopa umekopa.TISS na CIA hawana mamlaka kwa sababu haujavunja sheria.
 
Wengine wana bahati sana,unaenda kukopa benki Kwa dhamana feki unapata mkopo wa mabilion,sisi wenye dhamana za ukweli tunazungushwa mwishowe tunaambulia million kadhaa tu,wanafanyaje?
 
Ni mifumo ya kupata hiyo mikopo ndiyo imekuwa migumu lakini ukishakopa umekopa.TISS na CIA hawana mamlaka kwa sababu haujavunja sheria.
Mkuu, benki yoyote ukienda kukopa ni lazima wafanye checks ikiwemo authentications za documents.

Na kama kuna tatizo kama forgery ni lazima watoe taarifa polisi na kwingine.

Ndo maana twasema huenda ni inside job ambayo ushirikiano utapata kutoka kwa Whistleblowers.

Hivyo mfumo kama ni mgumu hupati mkopo na labda iwe ni dili la wale wa ndani na nje.

Ni kweli ukikopa umekopa lakini si kwenda benki tano tofauti hapo yaashiria pia kuwa hakuna kibendera kuashiria suspisions baina ya mabenki.

Ila kama ni mpango unowahusu watu wazito hilo pia ni tatizo.

Tujaribu kutohalalisha huu wizi kwa kisingizio chochote kile.
 
Wengine wana bahati sana,unaenda kukopa benki Kwa dhamana feki unapata mkopo wa mabilion,sisi wenye dhamana za ukweli tunazungushwa mwishowe tunaambulia million kadhaa tu,wanafanyaje?
Inside job.
 
Ukute naye afisa kitengo vinginevyo hizo benki ni zile mtu anakopa ml.50 kwa magunia 20 ya pumba za mchele na kusepa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…