Kama mtu anakopa benki 5 tofauti za Tanzania na akaweza kukimbia nchi bila kugundulika ni ishara kwamba TISS na vyombo vingine vimelala

Mkuu bila kuitaja urusi uzi haukamiliki🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Ameamua kututia machungu roho yake isuuzike,
 
Ukienda kukopa bank kama Nmb unachunguzwa mpaka chupi hata kama umekopa songesha wanajua na unaulizwa maswali kibao, sasa uyo mwenzetu ilikuwaje? Na mkuu wa Nchi kaongea na imeisha iyo hutoona chochote kinafanyika kwa wausika, ila kwa mengine eitha upinzani au machinga jamaa wanalibeba na wanakwambia kauli ya Raisi ni sheria
 
Huyu mtu analaumiwa kwa lipi hasa, kakopa siyo kaiba, nasema tena kakopa, tena kakopa mchana kweupe na jua linawaka. Sasa kama halipi madeni yake si mali alizoweka rehani ziuzwe ??? Na kama analipa madeni yake kelele za nini? Kama sheria inakataza kukopa zaidi ya benki moja, basi hapo kuna tatizo. Lakini sheria kama iko kimyaa tusipoteze muda humu kujadili vitu vilivyofanywa kisheria.

Tuhangaike na wale wa billions za ndege ya mizigo ambao wako mkononi mwa Rais. Namtafuta anifundishe kukopa benki zaidi ya kumi na mimi nifaidi looh
 
Hivyo Kipilimba angeweza kupewa nafasi ya kufundisha vijana wapya na pale UDSM wakawa na Department ya masuala haya ya security and risk management
Maneno yako yanaonyesha as if Kipilimba is the only dude kwenye system ambae anajua risk management, ndio hadi unataka awe mwalimu pale UDSM.
Kitu ambacho ni kibaya kwenye system.
 
Nakubaliana andiko

Ila tunaweza kuwalaumu TISS wakati sheria imewabana na wanashindwa kuitisha PRESS kusema walimshauri fulani fulani akutekeleza au kueleza kumefanikiwa hili na lile.

Nilimsoma sana mzee Mkuchika alivyokuwa anatoa ufafanuzi...
 
Kama amekopa tu kawaida kwenye benki tano tofauti na kutokomea mbona raisi nae ashangaa.

Hiyo yamaanisha kwamba benki zimefanya checks baada ya kutoa fedha na kisha kugundua kuwa mkopaji hakuwa si mtu wa kawaida.
 
Kama ni hivyo kwanini mkuu wa nchi aliongelee ikiwa kila kitu chajulikana?

Atupa faida gani?
Kwani wewe unafikiri imalijua tu pale baada CAG kulitaja, au limekosa tu majibu ndo maana anajikaza kaza na kulisukumia wananchi wadhani kama iko pamoja nao.
 
Nakubaliana andiko

Ila tunaweza kuwalaumu TISS wakati sheria imewabana na wanashindwa kuitisha PRESS kusema walimshauri fulani fulani akutekeleza au kueleza kumefanikiwa hili na lile.

Nilimsoma sana mzee Mkuchika alivyokuwa anatoa ufafanuzi...
TISS hushughulikia mambo kama haya nyuma ya pazia kisha kumpa kazi ya PR IGP aongee na vyombo vya habari.

TISS haipaswi kabisa kujulikana kazi zake hufanywa siri lakini vema sana.

Hii ipo kote duniani mazee hushughulika nyuma ya pazia kisha kuwaacha polisi wakimalizia pamoja na mahakama.
 
Kuilaumu TISS ni kupoteza muda. Mtu hawezi kopa mabilioni gavana asijue. Na isitoshe ukikopa benki yoyote ile lazima benki zingine watajua ukienda kukopa kwao kwasababu kabla ya kukupa hela lazima waangalie kama una deni kwingine. Hizo dhamana za kukopa mabilioni zilithibitishwa na nani? Idara ya uhamiaji iliwezaje kumpa vibali vya kuishi hadi kuweza kukopa? Kimsingi hapo kuna wazito wengi sana wamedaka mpunga tangu ile siku huyo mtu anaingia nchini. Akamatwe ili tuwajue walioko nyuma ya huo mpango wake. Lakini je hatutangaziwa msiba wake kabla ya yeye kukamatwa? TUSUBIRI HAPAHAPA JF.
 
Si kwamba TISS yalaumiwa bali yakumbushwa kuwa dunia sasa imebadilika.
 
Mkuu hapo tunawatuhumu vipi kama TISS haikufanya kazi?

Hili suala linategemea na utashi wa head of the state kama akiwa lege lege ndiyo mambo kama haya, unakumbuka tulivyokuwa na head of the state makini singa singa mzee wa IPTL alikamatiwa AIRPORT alikuwa anataka kutoroka.

Fikiria report ya CAG watu wamepiga pesa dhahiri shahiri, anawambia ajitathmini kama wana tosha, Tupo serious kweli?
 
Tiss wajishughulishe na mikopo? Hili mbona ni kosa la benki? Benki inakopeshaje mtu ambaye haimjui? Dhamana anazoweka kwanini hawazihakiki? Huu ni mchongo wa benki na TISS unawaonea bure. Hujui hata inavyofanya kazi pengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…