Kama Mungu hayupo, binadamu katokea wapi?

Hivi mkuu kabla ya Mungu kuwepo kulikuwa kuna nini?
 
Kazi gani anazozifanya ? Mungu mwenyewe unayemsema hawezi hata kujitetea mpaka wewe ndo umtetee? Hawezi kujidhihirisha basi japo kwa sekunde?

hata inzi huishi kwa siku saba!yeye huona kaishi muda mrefu!siku utakapo funga kauli ndiyo utajua!
 
ndugu yangu unasafari ndefu!unazungumzia maswala ya vipimo,hata kazi ya mungu hupimwa kwa kazi zake!

Utapimaje kazi ya Mungu ambae hata hajulikani?

Lakini pengine unajua jinsi ya kupima kazi zake mkuu utueleweshe na sisi tujue 😀
 
Kwanza kabisa lazima uelewe yafuatayo:-
1. Kutokuwepo kwa Mungu sio imani hivyo huwezi kumwambia mtu kuwa anaamini Mungu hayupo.
2. Mtu asieamini unamwambiaje ajue hicho kitu kipoje?
3. Huo mfano wako wa meza na kalamu ni mfano batili kwasababu kujua kama kalamu haipo sio lazima ujue kalamu ikoje, ukishaona meza iko tupu basi hapo utajua fika kuwa kalamu haipo.
 
Muumini katika ubora wako! Huyo Mungu wako ndo anaruhusu kusema maneno usiyo na hakika nayo?

Kama alivyoamini maandiko kipumbavu pumbavu bila kufikirisha akili, aweza pia kuamini maneno yake kipumbavu mkuu
 
hata inzi huishi kwa siku saba!yeye huona kaishi muda mrefu!siku utakapo funga kauli ndiyo utajua!

Unaweza kuthibitisha maneno yako?

Kufunga kauli? Unamaanisha kuwa kwenye conscous au?
 
Utapimaje kazi ya Mungu ambae hata hajulikani?

Lakini pengine unajua jinsi ya kupima kazi zake mkuu utueleweshe na sisi tujue 😀

nimeshakutajia kazi zinavyofanyika ndani ya mwli wako!sijui unataka zipi zaidi!
 
Mkuu... je una uthibitisho wowote kuwa mungu ndiye aliyefanya hayo yote uliyoandika???

Uthibitisho hakuna mkuu, ni maneno tu yanayotokana na imani zao ndomana ukiomba uthibitisho wanaanza kuruka ruka tu kama maharage yaliyo jikoni.
 
hakuna kilicho kabla ya mungu mkuu!

Hivi mkuu unafikiri mungu mwenye sifa kama hizo alizopambwa nazo kwenye vitabu vyenu, yawezekana hana muumbaji wake kweli?
Unajua kila kitu kina kina chanzo mkuu!
 
ww kama huna imani ya mungu,hata akijitokeza huweza kuamini!macho pia hayana sifa ya kuthibisha ukweli!ukitaza kwenye lami wakati wa jua kali utaoni kuna madimbwa ya maji lakini kila ukisogea unakuta hakuna!kwa hiyo macho hayana sifa ya kumtambua mungu!
 
kwanza ye mwenyewe katokea wapi?
 
Ukitaza = ukitazama
Utaoni = utaona
Madimbwa = madimbwi
Mkuu uwe unachangia kwa kiswahili mana wote tukitumia kabila zetu hatutaelewana.😀

Hapo hujajibu swali lolote lile wala hoja yoyote, ulichofanya ni kutoa maelezo ambayo wala hayana uhusiano na ulichoulizwa.
 
Mkuu kazi za mwili zina uhusiano gani na Mungu? Hivi mwenzetu biology hukusoma kabisa?

mnajazwa ujinga!hata computer inaweza kuwekewa prgm maalu na ikajiendesha yenyewe! Lakini yupo aliyefanya hayo yafanyike!
 
mnajazwa ujinga!hata computer inaweza kuwekewa prgm maalu na ikajiendesha yenyewe! Lakini yupo aliyefanya hayo yafanyike!

Huyo Mungu ana kazi kubwa sana kama huo ndo upeo wako ulipoishia.
 
pole sana ndugu!maneno mengi lakini hujatoa ushahidi wowote!wa kuonyesha kwamba mungu hayupo!

Kwasababu hayupo ndomana sina haja ya kutoa ushahidi. Kama angekuwepo na watu wakathibitisha basi ningelazimika kutoa ushahidi ila huku kutokuwepo kwake ni ushahidi tosha.
USIJITOE UFAHAMU WAKATI HATA WEWE MWENYEWE UMEKIRI UPO NAE KIIMANI TU
 
unaamini kwamba mungu hayupo kwasababu humuoni,!ila unakubali ulimwengu una chanzo!lakini huelewi hicho chanzo ni nini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…