Kwako Bwana Rajab kisauti
Nimeangalia maelezo yako.
Nionavyo mimi ni kwamba hujawahi kupata maelezo ya kisayansi yaliyo sahihi na ya kina kuhusu mwanzo wa viumbe hai duniani. Vitabu vipo vingi sana vinavyoeleza jambo hili. Kwa sasa wanasayansi wote wanakubaliana juu ya maelezo rasmi ya mwanzo wa viumbe. Maelezo uliyoyatoa hapo ni mepesi sana na hayaeleweki. Wanasayansi wanakubaliana kuwa viumbe vilianzia kwenye maji au baharini. Wanaanzia na 'primordial soup' ambamo kulikuwa na 'compounds' za kila aina ambazo zilikuwa zinaungana na kutengana. Nitaomba utafute vitabu hivyo au nenda kwenye encyclopedia ya Wikipedia (ipo kwenye mtandao wa intaneti) uanze kujielewesha kutokea hapo. Ninakushauri kwamba utakapokuwa unavisoma vitabu hivyo au maelezo husika usitafute weakness ya maelezo kwani hutaelewa. Maelezo ni magumu. Kumbuka sisi ni sawa na mpelelezi wa makosa ya jinai anayechunguza mauaji yaliyofanyika kutokana na risasi. Mpelelezi huyu anafika sehemu ya tukio bila kuwakuta wahusika na sasa anatakiwa kujenga taswira ya tukio lilivyokuwa. Ndivyo ilivyo kwetu wanadamu wa sasa. Wanasayansi wanapojaribu kugundua kilichotokea miaka zaidi ya bilioni 7 iliyopita wakati hata viumbe wa majini hawakuwepo ni changamoto kubwa sana. Hatuwezi kuwalaumu wanapojaribu kutoa maelezo sahihi ya kilichojiri wakati ule. Dini kwa upande wake maelezo yake yana mapungufu mengi sana kuliko wanasayansi. Kwa mfano dini ya Kikristu inasema umri wa dunia ni miaka 6,000 tu. Wachina peke yao wana historia ya miaka zaidi ya 5,000. Yapo mengi ya maelezo ya dini ambayo yanaacha maswali mengi kuliko majibu. Ingawa sayansi pia haina majibu yote lakini maswali ni mengi katika dini. Fahamu kuwa dini si ukristu peke yake. Kuna Uhindu, kuna Zoroastrian, kuna Uislamu, kuna Tao kuna dini za kienyeji, nk.