Nililouliza lipi? Umetoa ufafanuzi upi? Wapi? Huu ni ulimwengu wa hyperlink.
Wka link hapa.
Nitajuaje kwamba ushatoa ufafanuzi na si mzushi tu?
Au utajuaj kwamba kile unachofikiri wewe ni ufafanuzi hakijawa ushuzi tu kama hujanipa link nione ulichoandika na kukichambua?
Kwa nini niendelee kusoma nyuzi zako ili kupata chochote dhidi ya swali langu wakati unanijibu sasa hivi?
Umeandika barua mbinguni na unategemea kupata majibu yaliyo na majibu ya maswali yangu baada ya miezi kadhaa?
Awepo kwenye logic. Asiwe na contradiction.
Kwanza kabisa, sihitaji uthibitisho pekee kuwa mungu hayupo ili kuonesha kwamba mungu hayupo. Nahitaji uthibitisho wowote.
Inaonekana hujaelewa kwamba mungu anayebishiwa hapa ni muungano wa dhana nyingi.
Kuna mungu muweza yote, mwenye upendo wote na mwenye ujuzi wote.
Anapingwa kwa sababu muungano wa sifa zote hizo, pamoja na dunia hii iliyojaa maovu, unaleta contradiction.
Contradiction hii, upungufu, kiini chake si katika uwepo wa vyote pamoja, ni katika ukweli kwamba vyote vinaweza kutokea tofauti lakini haviwezi kutokea pamoja.
Tukirudi kwenye mfano wangu uliotokea katika mantiki za Euclidean geometry, unaweza kuwa na mviringo bila tatizo, unaweza kuwa na pembetatu bila tatizo. Lakini pembetatu na mviringo ni vitu viwili tofauti.Huwezi kuwa na pembetatu iliyo mviringo wakati huo huo.
Unaweza kuwa na uwepo wa mviringo. Unaweza kuwa na uwepo wa pembetatu. Lakini uwepo wa pembetatu ambayo ni mviringo kwa wakati huo huo ukawa haupo. Uwepo wa Mungu ni kama uwepo wa pembetatu ambayo ni duara hii ninayosema haiwezi kuwepo.
It is a logical contradiction. It does not exist. It is imaginary.
Due to the contradiction stated above.
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote anatakiwa awe ameweza kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya. Ulimwengu wetu una mabaya. Hivyo mungu huyo hayupo/