Kama Mungu hayupo, umaarufu wake unatoka wapi?

Kama Mungu hayupo, umaarufu wake unatoka wapi?

Mkitaka kuelewana kuwa Mungu yupo Au hayupo kwanza lazima muelewane kuwa Mungu ni nini

Otherwise ni vurugu tu
 
Habarini humu!

Moja kati ya maswali ambayo najiuliza ni kama Mungu hayupo sasa mbona ni jina maarufu sana, nafikiri ni jina pekee lenye kuabudiwa kwa namna tofauti tofauti.. sasa kama hayupo kwanini anaabudiwa kiasi hiki Dunia nzima!

Na kama alitungwa tu na binadamu, hao waliomtunga huyu Mungu wako wapi? inawezekanaje waliomtunga Mungu wasiwe maarufu kuliko Mungu mwenyewe? Ni nani ana ushahidi wa wazi kuhusu watu waliomtunga Mungu, wapo wapi na ni akina nani waliotunga tu uwepo wa Mungu?

Of course ni ngumu kuthibitisha uwepo wake kwa njia na kwa macho ya mwili ila effect yake ipo dhahiri kabisa, sioni kama kuna sababu ya kukataa uwepo wake eti kisa hatuwezi kumthibitisha, mwana huwezi kukithibitisha kitu usichokijua, na haina maana kama kitu hukijui basi hakipo.

Pia watu wengi ambao wanapinga uwepo wa Mungu just kwa sababu hathibitishiki kimwili hawapingi uwepo wa shetani japo naye pia hata hathibitishiki kimwili, why?

Anyway, kwa sababu wanaopinga uwepo wa Mungu wanasema Mungu ni nadharia tu na ametungwa tu na watu, sasa hao watu wanatungaje jina ambalo linaabudiwa kuliko wao? tena ni jina maarufu na kila lugha Duniani lina namna yake ya kumwita ili mradi tu lazima jina Mungu liwepo na liabudiwe.

Mungu ni kweli yupo kabisa tena bila ubishi. Yupo kabisa kama vile ulivyo uwepo wa jua na mwezi. Lakini hatuwezi kumuelewa Mungu kwa kumtafakari kwa namna tunavyolitafakari jua au mwezi. Mungu ni beyond that. Na ndio maana waliojaribu kumtafuta Mungu kwa namna ile tutafutavyo vitu vilivyoumbwa na Mungu, hawakumuona. Baadhi ya wanasayansi waliojaribu kutumuia scientific ways za kutafuta mambo hawakuweza. Mungu si kiumbe kama ilivyo wewe na mimi, kwani wewe na mimi tumeumbwa na Mungu. Macho yetu yetu hayawezi kumfikia au kumuona yeye, lakini yeye anatuona sisi na kila chembe ya dunia au umbile la kitu chochote. Mungu hana macho, mikono wala midomo na masikio kama tuliyonayo sisi, kwani hana shida ya kuwa na masikio au viungo vingine ili tuweze kujua hali mbalimbali za kimaumbile. Mungu yupo, na ili uweze kumuona ameweka taratibu ambazo zikifuatwa hizo kiuaminfu basi yule mwenye kutaka kumuona atamuona. Taratibu hizo amezikweka katika vitabu vya manabii mbalimbali waliopata kuzungumza nae pamoja na wachaMungu mbalimbali. Ili uweze kumuona Mungu unapaswa kufuata kikamilifu sheria na amri zake zilizopo kwenye Qurani, Biblia na vitabu vya manabii waliopita. Waliofanikiwa kufanya hivyo hatimaye wamemuona na wanaendelea kushuhudia maonyesho yake kwa namna mbalimbali hapa duniani
 
Soma kitabu hiki, utaelewa Ukweli kuhusu Mungu na namna ya kumuona https://www.alislam.org/library/books/OurGod.pdf
 
Habarini humu!

Moja kati ya maswali ambayo najiuliza ni kama Mungu hayupo sasa mbona ni jina maarufu sana, nafikiri ni jina pekee lenye kuabudiwa kwa namna tofauti tofauti.. sasa kama hayupo kwanini anaabudiwa kiasi hiki Dunia nzima!

Na kama alitungwa tu na binadamu, hao waliomtunga huyu Mungu wako wapi? inawezekanaje waliomtunga Mungu wasiwe maarufu kuliko Mungu mwenyewe? Ni nani ana ushahidi wa wazi kuhusu watu waliomtunga Mungu, wapo wapi na ni akina nani waliotunga tu uwepo wa Mungu?

Of course ni ngumu kuthibitisha uwepo wake kwa njia na kwa macho ya mwili ila effect yake ipo dhahiri kabisa, sioni kama kuna sababu ya kukataa uwepo wake eti kisa hatuwezi kumthibitisha, mwana huwezi kukithibitisha kitu usichokijua, na haina maana kama kitu hukijui basi hakipo.

Pia watu wengi ambao wanapinga uwepo wa Mungu just kwa sababu hathibitishiki kimwili hawapingi uwepo wa shetani japo naye pia hata hathibitishiki kimwili, why?

Anyway, kwa sababu wanaopinga uwepo wa Mungu wanasema Mungu ni nadharia tu na ametungwa tu na watu, sasa hao watu wanatungaje jina ambalo linaabudiwa kuliko wao? tena ni jina maarufu na kila lugha Duniani lina namna yake ya kumwita ili mradi tu lazima jina Mungu liwepo na liabudiwe.
Soma kitabu hiki, utajua ukweli kuhusu Mungu
https://www.alislam.org/library/books/OurGod.pdf
 
Lucifer ndiye mwenye nguvu kuliko mungu.wew huoni maovu mengi yakifanyika kuliko mazuri?

Hoja ya kwanza, Si kweli kuwa Lucifer ni mwenye nguvu kuliko Mungu na pia, si kweli kuwa duniani maovu ni Mengi kuliko mazuri. Ukweli upo hivi; Siku zote Lucifer au shetani hawezi kumshinda Mungu hata kama Dunia yote apewe Lucifer au Shetani kwa sababu Mungu ndio muumba wa Lucifer na Shetani, sasa haiwezekani muumbwaji awe na uwezo zaidi ya Muumbaji mwenyewe. Mungu ana uwezo wa Kumuondoa shetani AU Lucifer na asiathirike na chochote kwani Uwezo wote upo kwake Mungu na si Shetani au Lucifer. Haitokuja kutokea Shetani au Lucifer amshinde Mungu. Hilo haliwezi kutokea tangu kuumbwa kwa ulimwengu mpaka tutakaposimama siku ya hukumu. Tusijidanganye katika hilo.

Hoja ya Pili, si kweli kuwa duniani kumejaa maovu zaidi ya mema. Hata tukitoa mfano mdogo tu wa nyumba unayoishi utagundua kuwa si kweli maovu yapo mengi duniani. Kwa mfano, tuchukulie mlevi, mzinzi, jambazi, muuaji au mvaa nguo za uchi, hao wote wanafanya vitendo vyao kwa nyakati maalumu tu, lets usiku au mchana. Utagundua kuwa si muda wote wanakuwa kwenye hali hiyo. Kama watakuwa wakifanya hivyo muda wa usiku basi mchana watu hawa watalala au kupumzika. Sasa, muda watakao pumzika watu hawa either watakuwa wakifanya kazi ya kuhudumia matumbo yao au ya familia zao (jambo ambalo pia ni tendo jema kwa mujibu wa vitabu vya dini), sasa tunawezaje kuhitimisha kuwa maovu ni mengi duniani. Hebu tazama Mungu anaabudiwa mara ngapi kwa siku? Hata hao niliotolea mfano hapo juu, je? Huwa hawafanyanyi matendo mema kama vile kula, kunywa, kusalimia kwa tabasamu, kulisha ndugu, kuwaheshimu wazazi (hayo yote ni matendo mema kwa mujibu wa vitabu vya dini) au kumtaja Mungu au kufanya mema kwa siku?
 
Sasa
nataka nikujibu kama alivyo kujibu nusuhela kwamba sisi binadamu uhai wetu umetokana na mazingira
na mm ninaishi kutokana na vitu ambavyo vipo duniani kama kupata pumzi pamoja na chakula.
nikivikosa hivyo vitu nakufa.
unadhani ivyo vitu vinavyokufanya u ishi vilitokea wapi? Huoni ya kuwa ubadhibitisha uwepo wa Mungu?!
 
Nitathibitishaje kitu ambacho hakipo kwamba hakipo?

Unaweza kuthibitisha kwamba chumbani kwako hakuna kibatari cha dhahabu kisichoonekana na mtu kinachoelea katikati ya chumba chako?
Huwezi kupinga kitu ambacho hakipo kuwa hakipo, kipo ndio maana unapinga kuwa hakipo.

Naweza kudhibitisha kuwa chumbani kwangu kuna kibatari cha dhahabu kisichoonekana kutokana na ishara zitakazo onekana kutoka kwenye kile kibatari.
 
Kwa nini uniulize mimi kama nishawahi kuiona roho yangu? Nilishawahi kukuambia kwamba roho ipo?

Au una assume tu kwamba kwa kuwa wewe unaamini roho ipo basi kila mtu anaamini roho ipo?

Roho ni kitu gani? Unajuaje kwamba ipo na si hadithi tu?
Uwepo wa vitu visivyoonekana unadhibitisha moja kwa moja uwepo wa Mungu.

Roho ni pumzi ya uhai unayoivuta leo hii ambayo unaitumia kumpinga yeye aliyekupa yani Mungu.

Roho haiwezi kuwa hadithi, huwezi kutunga hadithi ya kitu kisichokuwepo.
 
Huwezi kupinga kitu ambacho hakipo kuwa hakipo, kipo ndio maana unapinga kuwa hakipo.

Naweza kudhibitisha kuwa chumbani kwangu kuna kibatari cha dhahabu kisichoonekana kutokana na ishara zitakazo onekana kutoka kwenye kile kibatari.
saizi tupo kwenye kizazi ambacho kinahitaji uthibitisho zaidi kuliko maelekezo.
hivi wewe kwa mfano upo mahakamani unaweza kuithitishia vipi mahakama kwamba mungu yupo.
 
afsi ni nini? Unaweza kuniambia nafsi ni nini kwanza? Usitumie maneno vague ambayo maana yake haiku well defined.
Unajuaje kwamba mimi nakubali nafsi ipo mpaka uanze kuniuliza habari za nafsi iko sehemu gani? Nilishawahi kukuambia nakubali nafsi ipo mpaka uniulize maswali hayo? Au una assume tu kwamba kwa sababu wewe unaamini hivi vitu basi kila mtu anaamini?
Kutokuamini uwepo wa nafsi haimaanishi kuwa haipo la hasha! Nafsi ni mtu wa ndani ambaye hufanana na wewe. Huwezi kuiona kwa macho ya kawaida wala kudhibitisha kwa vyombo vya kisayansi.
 
kama huo ni uthibitisho uwepo wa mungu kwanini watu wengine hivyo vitu wanavikosa.
Wanavikosa kivipi? Au una maanisha kufa! Kila chenye uhai lazima kiwe na uwezo wa kufa. Huo ni udhibitisho tosha kuwa Mungu yupo.
 
Kutokuamini uwepo wa nafsi haimaanishi kuwa haipo la hasha! Nafsi ni mtu wa ndani ambaye hufanana na wewe. Huwezi kuiona kwa macho ya kawaida wala kudhibitisha kwa vyombo vya kisayansi.
Sijaandika kwamba nafsi haipo kwa sababu siamini ipo.

Hujathibitisha kwamba nafsi ipo.

Unaandika tu kwamba ipo.

Kuandika tu "nafsi ipo" hakuthibitishi hilo.

Ni sawa na kuandika "Tembo wanapaa angani kutoka Serengeti kwenda Nairobi kwa kutumia mbawa zao tusizoziona".

Hilo halithibitishi kwamba wapo tembo hao wanaopaa.

Thibitisha. Usiandike tu bila uthibitisho.
 
ama yalijitokeza yenyewe au kama hayajajitokeza yenyewe, jibu lolote lile linapinga uwepo wa mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu wote.

Kwa sababu gani?

Kama vimejitokeza vyenyewe, tutaona si kweli kwamba vitu vyote hivi vinamhitaji mungu ili kujitokeza, na hivyo mungu huyu kasingiziwa tu haya mambo na inawezekana sana hayupo kabisa. Angalau habari ya mungu kuwa muumba wa vyote inakuwa uongo.

Kama haviwezi kujitokeza vyenyewe, kwa sababu hakuna chochote ambacho kinaweza kujitokeza chenyewe, ni lazima kiwe na mwanzo Fulani, na vyote hivi vimeumbwa na mungu, kwa kufuata kanuni hii hii ya "hakuna chochote kinachoweza kujitokeza chenyewe" hata huyo mungu naye anatakiwa asiweze kujitokeza mwenyewe, awe na mungu wake aliyemuumba, na huyo mungu wake naye awe na chanzo chake, hivyo hivyo ad infinitum, ad nausea.

Kwa hiyo jibu lolote litakalotolewa hapo, kama vitu vimetokea vyenyewe au vimehitaji kuumbwa, litakupa jibu la kwamba huyo mungu wako hawezi kuwepo kama unataka kuwa logically consistent
Hakuna udhibitisho ya kwamba Mungu ameumbwa, Mungu ameumba na udhibitisho upo. Vitu haviwezi kujitokeza vyenyewe lazima viwe na chanzo, hata ajali ina chanzo. Bado hujathibitisha kuwa Mungu hayupo ila unapinga tu uwepo wake.
 
saizi tupo kwenye kizazi ambacho kinahitaji uthibitisho zaidi kuliko maelekezo.
hivi wewe kwa mfano upo mahakamani unaweza kuithitishia vipi mahakama kwamba mungu yupo.
Nitawadhibitishia kwa kuwaambia "huwezi kuzungumzia kitu kisichokuwepo" ..wewe mwenyewe tayari ni udhibitisho tosha wa uwepo wa Mungu.
 
Hakuna udhibitisho ya kwamba Mungu ameumbwa, Mungu ameumba na udhibitisho upo. Vitu haviwezi kujitokeza vyenyewe lazima viwe na chanzo, hata ajali ina chanzo. Bado hujathibitisha kuwa Mungu hayupo ila unapinga tu uwepo wake.
Kama hakuna kinachoweza kujitokeza chenyewe, mungu katokeaje?

Usitake kuweka sheria kwamba hakuna kinachoweza kutokea chenyewe bila hanzo halafu hapo hapo ukaivunja kwa kusema mungu hana chanzo.

Utatupa contradiction.

Na kama tulivyoona hapo juu contradiction inaonesha uongo.
 
Nitawadhibitishia kwa kuwaambia "huwezi kuzungumzia kitu kisichokuwepo" ..wewe mwenyewe tayari ni udhibitisho tosha wa uwepo wa Mungu.
kwahiyo ww bila mzungu au mwarabu kukuambia mungu yupo wewe ungejuaje kwamba mungu yupo?
 
Back
Top Bottom