Kama Mungu hayupo, umaarufu wake unatoka wapi?

Kama Mungu hayupo, umaarufu wake unatoka wapi?

K
Tatizo umeupumbaza ubongo wako kwa kupenda kusoma. Kuhusu mwanadamu wa kwanza kuwepo hili swali hakuna anayeweza kujibu. Maana wanadamu wa mwanzo kabisa alikuwa na changamoto kubwa zaidi ya kuhifadhi kumbukumbu. Yaani hakuwa na muda wa kufikiria kuwa yeye ametokea wapi. Mazingira aliyoyakuta yalikua changamoto tosha. Yaan alipambana na wanyama wakali bila silaha, alipigwa na baridi bila nguo, alilala nje pasipo na uzio, alinyeshewa na mvua. Hivyo ni baadhi kati ya changamoto ambazo alikua anapambana nazo. Kwahiyo hakuwa na mawazo ya kutunza kumbukumbu

Kwa hiyo upo uthibitisho kwamba mwanadamu wa mwanzo hakuweza kuhifadhi kumbukumbu?Ulijuaje au ni hisia tu? Kwa hiyo Medula Obulangata haikuwa sehemu ya Ubongo wa mwanadamu wa kizazi unachokiongelea?Kwa hiyo kwa asili changamoto huchagiza mwanadamu kupoteza kumbukumbu au huchangia pia kuhifadhi kumbukumbu?
 
kama kweli mungu yupo kwanini wakufundishe kumuhisi yupo kuliko kumjua kwasasababu nijuavyo kuamini ni kuhisi na ndio maana watu wengi wamelizwa kwa kuwaamini watu.
Rudi kusoma tena nilichokisema halafu ndiyo uje.
 
Hawa vijana naona wamenikimbia wote hoja zimewashinda wameona wato nduki.
 
K

Kwa hiyo upo uthibitisho kwamba mwanadamu wa mwanzo hakuweza kuhifadhi kumbukumbu?Ulijuaje au ni hisia tu? Kwa hiyo Medula Obulangata haikuwa sehemu ya Ubongo wa mwanadamu wa kizazi unachokiongelea?Kwa hiyo kwa asili changamoto huchagiza mwanadamu kupoteza kumbukumbu au huchangia pia kuhifadhi kumbukumbu?
Hebu fikiria kwa makin alafu vuta hisia za mazingira ya mwanadamu wa kwanza ku exist. Hivi unadhani alikua anapata muda wa kukaa na kupumzika kwa amani?
Kwa uwezo wangu mdogo naamini alikua busy sana. Maana alikua na wakati mgumu wa kuhakikisha ana survive kutoka kwa wanyama wakali, baridi, mvua, atafute chakula na vitu vingi. Hivyo sidhani kama aliwaza habari za kutunza kumbukumbu eti wanaokuja wasipate tabu.
Tunaozaliwa miaka hii hatuna changamoto kabisa. Maana tumekuta zote zimeshatatuliwa. Ndio maana tunapata muda wa kudanganyana eti kuna mungu
 
Mkuu hivi ili uweze kuhifadhi kumbukumbu ni mpaka uwe na muda wa kupumzika? Na kumbukumbu za mambo gani unaongelea ambazo zisingeweza kuhifadhiwa kwa mtu huyo kukosa muda? Je,kama hakukuwa na kumbukumbu wewe umejuaje kuwa watu za zama hizo waliathiriwa na mazingira magumu?
 
Hebu fikiria kwa makin alafu vuta hisia za mazingira ya mwanadamu wa kwanza ku exist. Hivi unadhani alikua anapata muda wa kukaa na kupumzika kwa amani?
Kwa uwezo wangu mdogo naamini alikua busy sana. Maana alikua na wakati mgumu wa kuhakikisha ana survive kutoka kwa wanyama wakali, baridi, mvua, atafute chakula na vitu vingi. Hivyo sidhani kama aliwaza habari za kutunza kumbukumbu eti wanaokuja wasipate tabu.
Tunaozaliwa miaka hii hatuna changamoto kabisa. Maana tumekuta zote zimeshatatuliwa. Ndio maana tunapata muda wa kudanganyana eti kuna mungu
Sababu tu umekiri uwezo wako wa kufikiria ni mdogo ndio mana nimekuacha.

Ila mwanadamu kujihusisha na mambo ya kiroho (Mungu pamoja na mambo ya miungu) hayajaanza leo wapo waganga na wazee wa kimila vizazi na vizazi hata kijijini kwenu wazee walikua na miungu yao kabla ya utumwa wala ukoloni.

kwa kila rangi lugha na taifa tokea kuwako kwa misingi ya dunia mwanadamu amejihusisha na masuala ya kiroho usiongelee kitu usichokifahamu.
 
Miungu yao haijihusishi na kuumbwa kwa ulimwengu
 
Miungu yao haijihusishi na kuumbwa kwa ulimwengu
Kwahiyo wewe unata kuamini ile miungu isiyojihusisha na uumbaji wa ulimwengu peke yake?

Msingi wa reply yangu haikua ni aina gani ya miungu bali ni msingi wa mwanadamu kujihusisha na msauala ya kiroho in general bila kujali usahihi wake ni kwamba mwanadamu amejihusisha na masuala ya kiroho tokea kuwapo kwake juu ya nchi na wala sio miaka ya hivi karibuni kama ulivyosema.
 
Kuna kujua na kuamini,hivyo suala la kujua halihitaji imani. Sasa labda ueleze hiyo imani potofu ina sifa zipi ili nayo niijue mwalimu wangu.
Imani potofu sifa yake moja ni hicho unachokiamini kuwa na contradiction. Kinajipinga chenyewe.

Nitatumia maneno ya biblia.Mara nyingine yana make sense.

Mark 3:25 "If a house is divided against itself, that house cannot stand".

If a proposition has a contradiction against itself, that proposition cannot be true.

Kitu hakiwezi kuwapo na kutokuwapo hapo hapo.

Pembetatu haiwezi kuwa duara.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hawezi kuumba ulimwengu ambao maovu yanaweza kufanyika kama huu wetu.

Ukiamini chochote kati ya hivyo hapo juu kipo, kwamba pembetatu duara ipo au mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu huu ambao unaruhusu maovu kufanyika, umeamini kitu chenye kujipinga chenyewe kabla mtu yeyote hajakipinga.

Umeamini kitu chenye an inherent contradiction.

Umeamini kitu ambacho hakipo.

Umeamini uongo na mauzauza.

Pembetatu duara haipo.

Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote hayupo.
 
Mungu hayupo.

Idea ya Mungu kuwapo inapata umaarufu kwa sababu watu wengi wavivu hawataki kufikiri na hawataki kuchukua responsibility, wanataka mungu awepo ili achukue dhamana ya kutatua mambo yote.

Pia watu wengi hawafikirii logically, wanafikiria emotionaly.

Pia watu wengi wanaogopa kusema wanachofikiri na ku question uwepo wa mungu kwa sababu wanaogopa kuonekana wako tofauti.

Pia kusema huamini kuwepo mungu kunaweza kukukosanisha na familia, jamaa, rafiki, kazini etc.

Kitu kukubalika haina maana ni cha kweli. Kuna wakati watu waliamini dunia ni bapa na si tufe. Hilo halikufanya dunia iwe bapa.

Kuna wakati watu waliamini jua linazunguka dunia. Hilo halikufanya jua lizunguke dunia.

Hata kama watu wote wataamini mungu yupo, kama hayupo hayupo tu.

Kama unasema mungu yupo, thibitisha mungu yupo.
Thibitisha kuwa Mungu hayupo.
 
Thibitisha kuwa Mungu hayupo.
Kisichopo hakina uthibitisho nje ya logic. Kwa sababu hakipo. Huwezi kuchukua fingerprint zake, huwezi kupima uzito wake, huwezi kupiga picha yake. Kwa sababu hakipo.

Kwenye logic, kitu kinachojipinga chenyewe (contradiction) hakiwezi kuwapo.

Mathalan. Katika Euclidean geometry, pembetatu si duara. Duara si pembetatu. Pembetatu ambayo ni duara hapo hapo haiwezekani kuwapo. Ni contradiction.

Vivyo hivyo, mungu ambaye ana uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote asingeumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote, upendo wote na ujuzi wote kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani bila kupungukiwa chochote.

Uwepo wa ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana una contradict uwepo wa huyo mungu.

Ukiamini kuwapo kwa huyo mungu umeamini contradiction kama mtu anayeamini kiwapo kwa pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.
 
Lucifer son of the morning
The light bearer

Kasome encyclopedia brittanica page ya Christianity
Kasome "falsafa Na usanifu wa hoja "
Kasome "as it was in ancient...... Rome" series

Utajua Mungu alipotoka
 
Kisichopo hakina uthibitisho nje ya logic. Kwa sababu hakipo. Huwezi kuchukua fingerprint zake, huwezi kupima uzito wake, huwezi kupiga picha yake. Kwa sababu hakipo.

Kwenye logic, kitu kinachojipinga chenyewe (contradiction) hakiwezi kuwapo.

Mathalan. Katika Euclidean geometry, pembetatu si duara. Duara si pembetatu. Pembetatu ambayo ni duara hapo hapo haiwezekani kuwapo. Ni contradiction.

Vivyo hivyo, mungu ambaye ana uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote asingeumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wote, upendo wote na ujuzi wote kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani bila kupungukiwa chochote.

Uwepo wa ulimwengu huu ambao mabaya yanawezekana una contradict uwepo wa huyo mungu.

Ukiamini kuwapo kwa huyo mungu umeamini contradiction kama mtu anayeamini kiwapo kwa pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.
Bado hujathibitisha kutokuwepo kwa Mungu ..mifano uliyotoa haina mantiki yeyote. Kwa mfano nikikuuliza, umeshawahi kuiona roho yako? Au unajua nafsi iko sehemu gani kwenye mwili? Au utabisha huna roho kwa sababu hujawai dhibitisha uwepo wake! Nini basi chanzo cha mambo yote haya? Jua, Nyota, Mwezi, wewe, wazazi wako, mvua, upepo, kupatwa kwa jua/mwezi/dunia na mengine yote yaonekanayo na yasiyoonekana. Mambo yote hayo yalijitokeza yenyewe? Tena kwa mpangilio maalumu? Kwa nin basi kuna uchawi, uganga, shetani hayo pia huamini?! Wanasayansi wamegundua mifumo mbali mbali ya jinsi vitu vinavyofanya kazi mfano usiku na mchana, mvua kunyesha, na mengineyo mengi; ina maana utendaji kazi huu, ulijiweka wenyewe? Bora huamini uwepo wa Mungu na matendo yake, kuliko kutokuamini kabisa.
 
Njoo haoa jibu hii hoja acha kukimbia hoja hapa.

Nataka kupata uelewa kutoka kwako ili nikuamini unaamini Mungu hayupo sababu ya ideology uliyonayo inayokinzana na uwepo wa Mungu sasa naitaka ideology yako kwenye kipengele cha mwanzo wa uhai ulikuaje?
nataka nikujibu kama alivyo kujibu nusuhela kwamba sisi binadamu uhai wetu umetokana na mazingira
na mm ninaishi kutokana na vitu ambavyo vipo duniani kama kupata pumzi pamoja na chakula.
nikivikosa hivyo vitu nakufa.
 
Bado hujathibitisha kutokuwepo kwa Mungu ..

Nitathibitishaje kitu ambacho hakipo kwamba hakipo?

Unaweza kuthibitisha kwamba chumbani kwako hakuna kibatari cha dhahabu kisichoonekana na mtu kinachoelea katikati ya chumba chako?

.mifano uliyotoa haina mantiki yeyote..

Mantiki ni nini? Ukiiona utaijua? Nimekuonesha kitu kinaitwa contradiction katika huyo mungu wako. Kuna mantiki gani Zaidi ya kupinga kitu kwa kuonesha contradiction? Hebu nitjie hiyo mantiki.

Kwa mfano nikikuuliza, umeshawahi kuiona roho yako?

Kwa nini uniulize mimi kama nishawahi kuiona roho yangu? Nilishawahi kukuambia kwamba roho ipo?

Au una assume tu kwamba kwa kuwa wewe unaamini roho ipo basi kila mtu anaamini roho ipo?

Roho ni kitu gani? Unajuaje kwamba ipo na si hadithi tu?

Au unajua nafsi iko sehemu gani kwenye mwili?

Nafsi ni nini? Unaweza kuniambia nafsi ni nini kwanza? Usitumie maneno vague ambayo maana yake haiku well defined.
Unajuaje kwamba mimi nakubali nafsi ipo mpaka uanze kuniuliza habari za nafsi iko sehemu gani? Nilishawahi kukuambia nakubali nafsi ipo mpaka uniulize maswali hayo? Au una assume tu kwamba kwa sababu wewe unaamini hivi vitu basi kila mtu anaamini?

Au utabisha huna roho kwa sababu hujawai dhibitisha uwepo wake!

Roho ni kitu gani? Unajuaje kwamba ipo kweli na si hadithi tu ya kuelezea tusichokielewa?

Nini basi chanzo cha mambo yote haya? Jua, Nyota, Mwezi, wewe, wazazi wako, mvua, upepo, kupatwa kwa jua/mwezi/dunia na mengine yote yaonekanayo na yasiyoonekana. Mambo yote hayo yalijitokeza yenyewe?

Kama yalijitokeza yenyewe au kama hayajajitokeza yenyewe, jibu lolote lile linapinga uwepo wa mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote ambaye kaumba ulimwengu wote.

Kwa sababu gani?

Kama vimejitokeza vyenyewe, tutaona si kweli kwamba vitu vyote hivi vinamhitaji mungu ili kujitokeza, na hivyo mungu huyu kasingiziwa tu haya mambo na inawezekana sana hayupo kabisa. Angalau habari ya mungu kuwa muumba wa vyote inakuwa uongo.

Kama haviwezi kujitokeza vyenyewe, kwa sababu hakuna chochote ambacho kinaweza kujitokeza chenyewe, ni lazima kiwe na mwanzo Fulani, na vyote hivi vimeumbwa na mungu, kwa kufuata kanuni hii hii ya "hakuna chochote kinachoweza kujitokeza chenyewe" hata huyo mungu naye anatakiwa asiweze kujitokeza mwenyewe, awe na mungu wake aliyemuumba, na huyo mungu wake naye awe na chanzo chake, hivyo hivyo ad infinitum, ad nausea.

Kwa hiyo jibu lolote litakalotolewa hapo, kama vitu vimetokea vyenyewe au vimehitaji kuumbwa, litakupa jibu la kwamba huyo mungu wako hawezi kuwepo kama unataka kuwa logically consistent.

Tena kwa mpangilio maalumu? Kwa nin basi kuna uchawi, uganga, shetani hayo pia huamini?! Wanasayansi wamegundua mifumo mbali mbali ya jinsi vitu vinavyofanya kazi mfano usiku na mchana, mvua kunyesha, na mengineyo mengi; ina maana utendaji kazi huu, ulijiweka wenyewe? Bora huamini uwepo wa Mungu na matendo yake, kuliko kutokuamini kabisa.

Tatizo unataka kuamini, mimi nataka kujua.

Kuamini unaruhusiwa kuamini chochote. Kuna maazimio ya Umoja wa Mataifa ya kulinda haki yako ya kuamini, as long as huvunji sharia.

Lakini ukianza kutuhubiria hapa na kusema hili ndilo la kweli tuna wajibu wa kukuuliza na kupangua hoja potofu.

Hutakiwi kutuambia mungu yupo, ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote halafu kaumba ulimwengu huu ambao unaruhusu maovu yawezekane.

Kwa nini kaumba hivyo wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao maovu hayawezekani?

That is a contradiction. Kama pembetatu ambayo hapo hapo ni duara.

Ukiona contradiction hivyo, ujue kuna uongo hapo.

Huyo mungu unayemuamini ni wa uongo.
 
Back
Top Bottom