Kama Mungu ni mmoja Kwa nini kuna dini nyingi tofauti duniani?

Kama Mungu ni mmoja Kwa nini kuna dini nyingi tofauti duniani?

Ukimwona mtu wa dini anakuambia Mungu ni mmoja huyo ni tapeli anataka kujaza watu mahali anapoongoza ili apate sadaka nyingi.
Yes Mungu ni mmoja kwa maana kamili ila si mmoja.
Kila aina ya ibada inamwakilisha mungu wake halisi.
Hivyo kuna mungu wengi sana .
Kuna mungu mmoja huyo yeye anaabudiwa mpaka na majini(demons) kuwa makini naye. Ni muongo sana
 
Sijawahi kuelewa kwa nini kuna watu wanasema mungu ni mmoja ila duniani kuna dini nyingi mbalimbali tofauti kila moja ikiwa na maelezo tofauti kabisa kuhusu mungu.
Kwasababu huyo Mungu mmoja alituumba kwa Mfano wake(tuna umungu ndani yetu na akatupa hiyari kupitia huo uwezo aliotujaaliya,

Katika huo uwezo unaweza akaamini chochote na kikaleta matokeo kikubwa inatakiwa uwe na imani na unachokiamini.

Ukiwa na imani hata iwe ndogo ukiamini mti, jiwe, mnyama au mlima hata wanadamu mwenzio uatajibiwa kile unachokiomba... Sasa hapa haimaanishi kile unachokiomba ndio kinanguvu Hapana nguvu unayo wewe nyewe tena ndani yako ndio maana inatakiwa uwe na imani kwanza(umungu)

Na ndio maana kwenye maandiko Mungu ameagiza tusiabudu miungu mingine ila yeye(kwasababu anajua hiyari na kipawa alichokupa kitafanya kazi tu, mahali wakati na hali yoyote ile.
 
Mungu ni mmoja. Hiyo miungu mingine ni matokeo ya free will aliyotuumba nayo Mungu.
 
Mungu hayupo, kuna imani tu.

Imani haithibitishi kuwa kinachoaminiwa kipo.

Ili useme Mungu yupo hutakiwi kutumia imani.

Imani ni mashaka, Imani ni wasiwasi, imani ni betting, imani ni kama mchezo wa ku flip coin huwezi kujua itaangukia kwenye nini.

Penye wasiwasi hapana uhakika. Palipo kosekana uhakika hapawezi kuwa na uthibitisho.
 
Kati ya mada za kijinga ni hizi za kujadili uwepo wa Mungu ni bora mkishashiba mihogo mjue mambo mengine ni ushauri wa bure tu
 
Sijawahi kuelewa kwa nini kuna watu wanasema mungu ni mmoja ila duniani kuna dini nyingi mbalimbali tofauti kila moja ikiwa na maelezo tofauti kabisa kuhusu mungu.
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

Wanadamu ndio wamemtunga Mungu vichwani mwao na ndio maana wanahangaika kufosi na kulazimisha uwepo wake.

Mungu hajawahi kuwepo na hayupo kujidhihirisha mwenyewe, kujitetea mwenyewe, kujiongelea mwenyewe na kujithibitisha mwenyewe kwamba yupo.

Ni wanadamu na viherehere vyao tu wanafosi na kumpambania Mungu ambaye hayupo, aonekane yupo.
 
Sijawahi kuelewa kwa nini kuna watu wanasema mungu ni mmoja ila duniani kuna dini nyingi mbalimbali tofauti kila moja ikiwa na maelezo tofauti kabisa kuhusu mungu.
Kama London ni moja duniani, kwa nini kuna njia nyingi (routes) za kufika huko?
 
Back
Top Bottom