Kuna Watu nawashauri mapema tu kwakuwa nimeshaona hawana Mabeki wa Kuwazuia akina Mayele na Musonda hiyo tarehe 9 April, 2023 basi GENTAMYCINE nawashauri kuanzia leo wakirejea kutoka Kuzurula na kupoteza muda na Pesa kwa Mwarabu wawatafute Waganga wazuri wa Kienyeji wa Kuwazuia Washambuliaji hawa HATARI ili ikifika tarehe tajwa ya Mtanange ( Mechi ) wote wawe ama na Shipa au Wameshikwa na Ngiri.
Popote pale walipo Watu wa Kamati ya Usajili ya Yanga SC Mimi GENTAMYCINE bila Unafiki wala Uwoga ( pamoja na kuwa ni mwana Simba SC lia lia ) nawapeni Shikamoo kwani kila mnakogusa ni patamu na sahihi.
Mwenyezi Mungu aiweke mahala pema Roho ya Marehemu Mafia Mwenzangu wa Soka la Bongo na Jicho Kali la Usajili Simba SC Zakaria Hanspoppe na Binafsi kama Mdogo wako GENTAMYCINE pengo lako naliona lipo na litaendelea kuwepo mpaka pale tu Mwarabu Mnyiramba Mmoja atakapoacha kutufanya wana Simba SC wote ni Hamnazo ( Hatuna Akili ) na Yeye anayetupeleka Baharini Uarabuni wakati hata hapa Dar es Salaam Bahari ipo ndiyo Mjanja.
Utakuwa ni Mwendawazimu Uliyetukuka ukikataa kuwa hata Msimu huu wa 2022 / 2023 NBC Premier League Yanga SC ndiyo Mabingwa tena na tuliobakia labda tupambane Kubeba Kombe la TFF ( ASFC ) au lile la Mnyama Day la kila tarehe 8 August ya kila mwaka.
Nakaribisha Matusi yote, dhihaka zote dhidi yangu GENTAMYCINE na nitashangaa nisipoona au nisipokuta Comment yoyote ile ikisema Mimi ni ( mwana ) Yanga SC dam dam au Kirusi au nina Chuki na Mwarabu Mnyiramba au siitakii Mema Simba SC.
Na nisisahau wakati tukitafuta Waganga wazuri wa Kienyeji wa Kuwaroga akina Mayele na Musonda tusimsahau pia na Kumroga na Aziz K ambaye kwa sasa nina uhakika Kipa Wetu Manula akiona tu Faulo imetokea Jirani atakuwa anapanga Ukuta wake huku na Choo chake cha kwao Matombo Mkoani Morogoro nacho taratibu kinaanza Kumpigia Hodi maeneo ya 'Kunako' ya Kibaiolojia kwani tayari anajua Mwanaume 'akikunjuka' tu ni Mawili aingie nao mazima Nyavuni au aufuate huku akitengua kabisa na Mbavu zake kisha akalazwe Sewahaji au Mwaisela Muhimbili kwa Matibabu zaidi.