Unajua Nimeangalia Comments Nyingi Humu Za Ndugu zangu wakristo wakishabikia Kuhusu hili swala Wakajisahau hata wao Wana Aya na Mafungu yanayofanana na Hayo tena Huenda Zaidi ya Hayo na Yenye Hatari zaidi...
Mnawaonea Sana waislam Lakini Vitabu vyote viko Sawa..
Nianze kuchambua Sasa
Mithali 20:30
"Machubuko ya fimbo husafisha uovu, Na mapigo hufikilia ndani ya mtima"
Mtu akitandikwa Bakora Vizuri zikamwingia Kabisa na akapata machubuko Basi uovo wake hautajirudia Tena (Kuliingana na Biblia)..
Hapa.Chini Ni Mchungaji akiwatandika Barabara Waumini Waliokiri Kiwa Na Dhambi ili.kuondoa Uovu wao kama.Ilivyosema Mithali...Je tutamlaumu kwa Kufanya Hivyo? BIBLIA inasema Michubuko Ya fimbo Husafisha Uovu?
View attachment 3137918
Tukimuacha Mchungaji Kwa Kufata Maandiko ama kwa kuamua Kwenda sambamba na Maandiko Tuendelee
Mithali 23:12-14
"Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.
Usimnyime mtoto wako mapigo; Maana ukimpiga kwa fimbo hatakufa.
Utampiga kwa fimbo, Na kumwokoa nafsi yake na Kuzimu."
Biblia Inaelekeza Kumpiga Mtoto kw Fimbo mpaka akili yake Ikae Sawa na Usimnyime Kipogo hicho Ns unatakiwa Utembeze Bakora Ili uokoe Nafai yake...
Sasa Kosa La Quran Kuonekana Kitabu Kibaya Ni kipi Kama Tunatetea Upande Tuangalie na Kwetu kukoje?
Quran Imesema Mwanamke asipokutii (Tuseme labda Kuchepuka) ifate Taratibu za kumshauri, Ukiona Bado hakusikii, Hama chumba (Tafsida hiyo maana yake Mnyime haki yake ya Ndoa)..ukiona bado hakusikii Mchape Pigo lisiloumiza..
Hiyo Ni Quran Sasa Bible Inasemaje Kuhusu Mke asiyesikia au Mke Muovu..
Mithali 21:9
"Ni afadhali kukaa katika pembe ya darini, Kuliko katika nyumba pana pamoja na mwanamke mgomvi."
kwahyo Ni afadhali Kumuhama Chumba Kuliko kukaa Ndani na Mwanamke Mgomvi asiyesikia Ushauri wako au Unasihi wako Its same as Aya uliyoleta..hiyo.Ni steps 2 Kutoka kwenye aya Uliyoleta..
Kuhusu Kutii
Waefeso 5:22-25
"22 Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.
24 Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.
25 Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;"
Mwanaume Akilala na Mke wake akakuta Mke wake Sio Bikra akashitaki na Kusema Mke wake sio Bikra na ana mchukia..
mwanaime Akiwa Amedanganya na wazee wa Mke wakathibitisha kuwa Binti alikuwa Bikra Atatozwa Pesa kadhaa Na ataachiwa Huru na Yule mwanamke haruhusiwi kuondoka kwa Mumewe....
Ila kama mwanamke akakutwa Sio Bikira Basi Huyo mke Atapigwa kwa Mawe mpaka Kufa (Kumbukumbu la Torati 22:13-21)
Na Mengine Mengi soma Hapa Chini...
View attachment 3137871
View attachment 3137872
Sasa Nilitaka Kusema Nini Dini zote zina Makosa Yanayofanana au Yanayozidiana Kunyoosheana Vidole Hakuwezi kuondoa Makosa Yaliyopo Kwako au Kukufanya Ujisikie vizuri kwa Kumsema Mwingine..
Tuishi kwa Amani na Kidumisha Upendo