Kama Mwanasheria Mgongolwa ni makamu mwenyekiti wa kamati ya sheria na aliingia kikaoni, Yanga wameshinda kesi ya Feitoto

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
Haihitaji kwenda chuo kikuu kujua, Alex Mgongolwa wakili maarufu nchini na mwanachama kindakindaki wa Yanga aliingia kwenye kikao cha kujadili suala la Feitoto wakati akijua kabisa kuwa kuna conflict of interest, Mgongolwa ni makamu mwenyekiti wa kamati ya sheria TFF inayojadili suala la Feitoto lakini ni mwanachama wa yanga, mawakili wa Feitoto walimwekea pingamizi lkn bado aliingia kikaoni.

Sasa mnadhani Utopolo itashindwa hapo? Mnaokaa kudhani kuwa Feitoto atashinda kesi mnapoteza muda wenu bure, cha msingi suala hilo liende CAS, huku bongo kumejaa ubabaishaji mno, ujanja ujanja, unafiki, mapenzi na uhuni
Wa kufa mtu.

Feitoto akishinda kesi ntahama nchi hii


Sent from my SM-F916B using JamiiForums mobile app
 
TFF wameshindwa kabisa kulisimamia hili suala kiuweledi, wapo kiswahili sana, wanaonesha walivyo dhaifu na wasio huru kusimamia haki za wachezaji.
 
TFF wameshindwa kabisa kulisimamia hili suala kiuweledi, wapo kiswahili sana, wanaonesha walivyo dhaifu na wasio huru kusimamia haki za wachezaji.
Walio mshawishi Feitoto avunje mkataba nadhani wanaifahamu Sheria vizuri Sasa waende wakathibitishe pasina shaka kua Fei alistahili Kuvunja mkataba.
Swala la kusema Mgongolwa ana ushawishi wa kimaamuzi ni umbumbumbu.
Mgongolwa hakuwepo, Wala hakumshawishi Fei avunje mkataba, Mchuma janga ula na Nduguze.
 
Sasa mchezaji km hataki team, hata akitakiwa kurudi na akaenda kufanya tofauti na matarajio ya waliomrudisha sasa ndo nn inakua?

Bora wamuachee aende anako taka, Dogo anatafuta maslahi yake.
Upenzi wa team leo Ngasa anashindia mihogo ya mama aziza Magomeni mikumi.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Utakuwa umeamua kuhama mkuu! Kuwa nakamura mwenyekiti hakumfanyi awe na final decision
 
Mi kweli Mgongolwa hakutakiwa kuwepo swala la Morison alionyesha ukereketwa wake Kwa yanga Kwa kuwadanganya watashinda cas wakati kisheria alijua yanga wamekosea.
Hii kesi imetajwa haraka Kwa sababu ya ushawishi wake Kwa yanga ila mawakili wa feitoto wapo makini kitendo Cha kumwekea pingamizi na yeye kuingia kitawekwa kwenye rekodi na wale mawakili wanajua wakitoka hapo next itakuwa cas ambako hakuna anayemjua mtu zaidi ya kufata sheria.
 
Hivi nyie mikia hamna issue nyingine za kufanya? Mbona mnazidisha uchawa kwa Fri, tunajua kabisa Holi suala aliyeponyuma yake Wala si Azam Kama tunavyoaminishwa, Ni klabu flani hivi yenye tabia za kupenda vya dezo Kama Malaya. Anyway so far Fei Hana nafasi Tena klabuni kwetu, mchukueni Kama mlivyofanya kwa BM, Gardiel nk, sisi klabu yetu tutajipanga na tutapata mbadala wake. Ila punguzeni kupenda vya bure Kama Malaya, siku si nyingi vitawaua siku si zenu. Haya machawa endeleeni kufungua nyuzi zingine kuhusu Fei.
 
Unaongelea mbadala UPI wakati yupo Aziz Ki? Nabi alikuwa anapata shida sana kuwachezesha Aziz Ki na Feisal kwa wakati mmoja maana wote wanacheza namba moja.

Feisal ni mchezaji mzuri lakini siyo pengo kwa Yanga.
 
Tuwape pesa Chama, Manula, Inonga, na Kapombe wawaingizie kwenye account ya Simba wavunje mkataba bila mazungumzo? Be honestly.
 
Kwani ni lazima feisal ashinde iyo kesi? Hakuna uwezekano wa feisal kushindwa bila uwepo wa uyo mwanasheria? Kwanini unahitimisha ushindi kwa yanga ukiwa hata haujasikiliza hoja za pande zote mbili?.. mimi ni shabiki wa yanga ila hata yanga akiangukia pua kwenye ilo sakata nitachukulia poa tu maana iyo ni kawaida kwenye mambo ya kisheria ukibugi sehemu ndogo tu mwenzako anakupiga bao
 
Tuwape pesa Chama, Manula, Inonga, na Kapombe wawaingizie kwenye account ya Simba wavunje mkataba bila mazungumzo? Be honestly.
Wakifikia hatua hiyo hakuna kugeuka nyuma ni mkono wa kwaheri waelekee wanakotaka, mtu had kuamua kuvunja mkataba hajakurupuka kadhamiria na anajua anacho kifanyaa.

Hivi hata akirud tena huko yanga huyo Fei bado atakua na imani hapo? Au yanga itakua na imani nae?
 
yanga hawapambani kumrudisha fei klabuni na ndo maana unaona wanaendelea kusajili kwasababu hawamtaki tena huyu dogo,wanachotaka wao yanga ni utaratibu kufatwa km una timu inakutaka waje mezani na ofa ili uuzwe na klabu iliyo na mkataba inufaike,kabla ya fei hajafikia maamuzi ya kuvunja mkataba na yanga,yanga wana haki ya kupewa nafasi ya kujadiliana nae kwanza.

Hivi imagine we ndo try again unaamka anambiwa chama,phiri na inonga wameingiza pesa kwenye akaunti ya klabu ya kuvunja mikataba yao unafanya nini?unavuta shuka na kuendelea kulala au...
 
Kawaida kwenye maswala ya kisheria kama Kuna mhusika ana mgongano wa kimaslahi anatakiwa ajitoe ili haki itendeke.
Mgongolwa amejitabainisha Toka mwanzo ukifatilia swala la Morison ungeelewa kwanini mawakili wa feitoto walimtaka ajiondoe
 
Inategemea mkataba wa Chama, inonga au Phiri ukoje kitu ambacho hamtaki kuelewa yanga walikosea kuweka kipengele Cha kununua mkataba Kwa kiwango walichotaja.
Yanga sio ya kwanza hata Neymar alipoondoka Barcelona kwenda PSG alinunua mkataba wake Kwa kiwango kilichowekwa
 
Alikwepo na Morrison alishinda,mchawi mkataba.atakayeshindwa Kama anaona ameonewa.aanike mkataba wote jf .
 
Kawaida kwenye maswala ya kisheria kama Kuna mhusika ana mgongano wa kimaslahi anatakiwa ajitoe ili haki itendeke.
Mgongolwa amejitabainisha Toka mwanzo ukifatilia swala la Morison ungeelewa kwanini mawakili wa feitoto walimtaka ajiondoe
Ndo hajajitoa sasa tusubiri majibu ya iyo kesi kama feisal akishindwa ana haki ya kukata rufaha ngazi ya juu zaidi
 
Hao mbumbumbu wanajizima data, si kwamba hawajui kwamba Feisal amekosea, ila kwao wanajifariji kwa kila jambo lisilojema likitokea kwa Yanga ndio furaha yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…