Kama Mwenyekiti wa Chama atajihusisha na Ugaidi na chama hakifutwi, kosa gani linaweza kusababisha chama kufutwa?

Pslmp

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2021
Posts
1,622
Reaction score
2,458
Kwanza naomba nieleweke kwamba, Huu uzi hauongelei chama chochote, isipokuwa unaangazia makosa ambayo yakifanyika ndani ya chama chochote, na nani ndani ya chama endapo atafanya makosa yanayopita uwezo wa kustiliwa hadi kupelekea kufutwa kwa Chama,

Kama M/kiti wa chama husika, anajihusisha na mambo ya kigaidi na bado chama hakuwezi kufutwa, Je, ni kosa lipi lingine ambalo linaweza kupelekea chama cha siasa kufutwa?

Kama kosa doogo kabisa la mgombea Urais kuanza kampeni kabla ya kipyenga rasimi kupulizwa, anaweza kuondolewa kwenye nafasi ya ugombea Uraisi au kuadhibiwa vikali.

Je, Ili chama kifutwe, ni makosa gani ambayo yakitendeka ndani ya chama, yanayompa nafasi Msajili wa vyama kukifuta chama hiko kupitia sheria na kanuni za usajili nchini!

Karibuni wadau na wajuzi wa mambo ili hata likitokea, wote tunakuwa tunafahamu
 
Daaah hili jambo lingekuwa kipindi cha Maghufuli aisee makelele ya hapo, ingeonekana ana chuki na wachaga, ila amejifia zake na limefanyika kipindi cha Rais mpendwa! Na Kwa jinsi wanazengo hawatilii maanani watamfunga kweli.
 
Daaah hili jambo lingekuwa kipindi cha Maghufuli aisee makelele ya hapo, ingeonekana ana chuki na wachaga, ila amejifia zake na limefanyika kipind cha Raisi mpendwa! Na Kwa jinsi wanazengo hawatilii maanani watamfunga kweli
Kwa hiki kinachoendelea, Wasukuma na wachaga, wangelihitaji mtu wa kuwasuluhisha

Lakini kwa sasa, hayo hayapo tena, na usikute, kuzuka kwa jina, Sukuma gang na chaga gang, ulikuwepo kimkakati ili kutakapotokea lolote isemwe msukuma JPM anachuki na wachaga, lakini hata hivyo, Mungu ni mwema sana.
 
Kama M/kiti wa chama husika, anajihusisha na mambo ya kigaidi, Je, ni kosa lipi lingine ambalo linaweza kupelekea chama cha siasa kufutwa?

Kama kosa doogo kabisa la mgombea Uraisi kuanza kampeni kabla ya kipyenga rasimi kupulizwa, anaweza kuondolewa kwenye nafasi ya ugombea Uraisi au kuadhibiwa vikali.

Je, Ili chama kifutwe, ni makosa gani ambayo yakitendeka ndani ya chama, yanayompa nafasi Msajili wa vyama kukifuta chama hiko kupitia sheria na kanuni za usajili nchini!

Karibuni wadau na wajuzi wa mambo ili hata likitokea, wote tunakuwa tunafahamu
CHADEMA WAMEKWISHASINGIZIWA UGAIDI MARA 100 UNAKUMBUKA KESI YA LWAKATARE?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, kwanza nakanusha kwamba, uzi huu hauihusu Chadema, uzi huu unaangazia makosa ambayo yanaweza kupelekea kufutwa kwa chama, iwe sisiemu, Chadema, ACT n.k

Umeongelea suala la Lwakale, Ni kweli huyo mbunge wa zamani kupitia Chadema alihusishwa na ugaidi wa kuzushiwa, lakini ukumbuke, Lwakatale hakuwa Kiongozi mkubwa katika Chama

Hapa, tunaongelea ngazi ya juu kabisa ya Chama chochote, kiongozi mkuu kama M/kiti, anapojihusisha na ugaidi, Je, chama kinaweza kufutwa, ama kunakosa lingine zaidi ya hapo na afanya nani ili ndio liwe kosa la kichama?
 
Huyu si ndo alitabiri mabaya kwa serikali hii, Kisa M/kiti wa Chadema anatuhumiwa na ugaidi?

Nabii yeyote, yeyote awe wa kifumu ama wa Mungu hatabiri mawazo ama utashi wake. Naomba utofautishe maombi na unabii.
 
Kwa hiki kinachoendelea, Wasukuma na wachaga, wangelihitaji mtu wa kuwasuluhisha,

Lakini kwa sasa, hayo hayapo tena, na usikute, kuzuka kwa jina, Sukuma gang na chaga gang, ulikuwepo kimkakati ili kutakapotokea lolote isemwe msukuma JPM anachuki na wachaga, lakini hata hivyo, Mungu ni mwema sana.
Kiongozi, hapa suala la ukabila linatoka wapi? Kuna tatizo gani kati ya Wasukuma na Wachaga?
 
Mkuu, haukosoma ujumbe wa niliyemQuote

Yeye alisema, jambo hili linalomhusu M/kiti wa Chadema lingetokea akamatwe katika kipindi cha JPM tena kwa suala hilihili la ugaidi, Ile lugha ya JPM anachukia Wachaga na ile dhana ya sukuma gang, chuki yake ingeongezeka mara elfu, na pengine kungelihitajika mtu wa kuzipatanisha hizi pande mbili,

Bahati mbaya yanatokea haya, JPM hayupo, na ndiyo maana nilitaka kusema,

Kwa Tanzania yetu mahali ilipo na kwa misingi bora iliyowekwa, sisi hatuna ukabila, na ukiona kuna kelele za ukabila, chunguza, na ukichunguza kwa umakini ndio utaweza kuona kama haya ya tuhuma za Mbowe

Kwa wenye kujisemea, mtu anaweza kusema..! kumbe ile chuki iliyokuwa ikifukuta chinichini ya Sukuma gang kuchukiana na Watanzania wenzao Wachaga, kulikuwa na namna iliyokuwa inaundwa kitaalamu, kwamba ikitokea Mbowe amedakwa kwa tuhuma hizo, iwe ni suala la mtu kuamini moja kwa moja kuwa, Msukuma JPM anachuki na wachaga,

Sasa yanatokea haya JPM msukuma hayupo,

Tuacheni sasa siasa zisiwe zinatuchonganisha, na kila mwenye kutenda kosa, awajibishwe kisawasawa na mtu mwingine yeyote na kusiwepo kusema sijui kwa sababu ya kabla lake, hapana!
 
Mkuu, kwanza nakanusha kwamba, uzi huu hauihusu Chadema, uzi huu unaangazia makosa ambayo yanaweza kupelekea kufutwa kwa chama, iwe sisiemu, Chadema, ACT n.k

Umeongelea suala la Lwakale, Ni kweli huyo mbunge wa zamani kupitia Chadema alihusishwa na ugaidi wa kuzushiwa, lakini ukumbuke, Lwakatale hakuwa Kiongozi mkubwa katika Chama

Hapa, tunaongelea ngazi ya juu kabisa ya Chama chochote, kiongozi mkuu kama M/kiti, anapojihusisha na ugaidi, Je, chama kinaweza kufutwa, ama kunakosa lingine zaidi ya hapo na afanya nani ili ndio liwe kosa la kichama?
Hata CUF tuliambiwa walileta kontena la visu na mapanga kuchinja watu watakapoanguka kwenye chaguzi 2005!!

Nachojua kama huo ugaidi utahusisha chama kama taasisi basi hapo anaweza kukifuta ila kama ni jinai ya mtu binafsi ndani ya chama then wanaweza lift the veil of incorporation ili mtu ashtakiwe yeye kma yeye (As was the case kwa Lwakatare) ila kikishtakiwa chama kama chama then kesi wakaanguka basi automatically chama kitafutwa.

Maadam it's Mbowe kama Mbowe na waliohusishwa ni walinzi wake na askari wastaafu wasio na kadi za CHADEMA then ni individual zaidi kuliko kitaasisi. So hata wakimkuta na hatia chama hakiwezi kufutwa maana kaifanya kwa individual capacity sio kama taasisi.
 
Kwa hiki kinachoendelea, Wasukuma na wachaga, wangelihitaji mtu wa kuwasuluhisha

Lakini kwa sasa, hayo hayapo tena, na usikute, kuzuka kwa jina, Sukuma gang na chaga gang, ulikuwepo kimkakati ili kutakapotokea lolote isemwe msukuma JPM anachuki na wachaga, lakini hata hivyo, Mungu ni mwema sana.
Mbona hii kesi ilifunguliwa JPM akiwa Rais?? Hta Mama samia kajitetea hivyo..... So huwezi ukajitoa kumuingiza JPM kwenye hii kesi.

Lakini mwanzo walimuachia baada ya presha ya ubalozi wa ujerumani na EU nashangaa ghafla eti ushahidi umepatikana!! Kwani kipindi kile wanamkamata na Boniface Jacob ushahidi haukuwepo?? Na toka lini kesi ya ugaidi ina dhamana hadi akaachiwa unconditionally?
 
Hata CUF tuliambiwa walileta kontena la visu na mapanga kuchinja watu watakapoanguka kwenye chaguzi 2005!!

Nachojua kama huo ugaidi utahusisha chama kama taasisi basi hapo anaweza kukifuta ila kama ni jinai ya mtu binafsi ndani ya chama then wanaweza lift the veil of incorporation ili mtu ashtakiwe yeye kma yeye (As was the case kwa Lwakatare) ila kikishtakiwa chama kama chama then kesi wakaanguka basi automatically chama kitafutwa.

Maadam it's Mbowe kama Mbowe na waliohusishwa ni walinzi wake na askari wastaafu wasio na kadi za CHADEMA then ni individual zaidi kuliko kitaasisi. So hata wakimkuta na hatia chama hakiwezi kufutwa maana kaifanya kwa individual capacity sio kama taasisi.
Pointi
 
Basi chadema ifutwe tu. Ili maushungi atulize nafsi yake.
 
Yaani kwa kuwa mwenyekiti anatuhumiwa kwa ugaidi halafu eti chama kifutwe! Kwani mtuhumiwa ni yeye binafsi au chama?
 
Mkuu, kwanza nakanusha kwamba, uzi huu hauihusu Chadema, uzi huu unaangazia makosa ambayo yanaweza kupelekea kufutwa kwa chama, iwe sisiemu, Chadema, ACT n.k

Umeongelea suala la Lwakale, Ni kweli huyo mbunge wa zamani kupitia Chadema alihusishwa na ugaidi wa kuzushiwa, lakini ukumbuke, Lwakatale hakuwa Kiongozi mkubwa katika Chama

Hapa, tunaongelea ngazi ya juu kabisa ya Chama chochote, kiongozi mkuu kama M/kiti, anapojihusisha na ugaidi, Je, chama kinaweza kufutwa, ama kunakosa lingine zaidi ya hapo na afanya nani ili ndio liwe kosa la kichama?
Kwanini usisubiri hukumu mkuu pamoja na rufaa pia kama itakuwepo kisha ndo taratibu za kukifuta chama ama lah zifuatwe.

Sasa hizi ni tuhuma tu unataka chama kifutwe kwasababu ya tuhuma tu?
 
[/QUOTE]
Pointiu
Yaani kwa kuwa mwenyekiti anatuhumiwa kwa ugaidi halafu eti chama kifutwe! Kwani mtuhumiwa ni yeye binafsi au chama?
Ni kosa lipi sasa linaloweza kupelekea kufutwa kwa Chama mkuu, na nani atende ndipo iwe sababu ya kufutwa chama?
 
Kwanini usisubiri hukumu mkuu pamoja na rufaa pia kama itakuwepo kisha ndo taratibu za kukifuta chama ama lah zifuatwe.

Sasa hizi ni tuhuma tu unataka chama kifutwe kwasababu ya tuhuma tu?
Sawa mkuu
 
Aliyeshitakiwa ni Freeman Mbowe, si mwenyekiti. Tujifunze kutofautisha vitu hivi.
 
Back
Top Bottom