Kama mzaha hoja ya Mbunge Shabibi inaweza kutungiwa Sheria kuongeza maumivu kwa wananchi

mtafanyaje ikipitishwa? mtalipa tu, Taifa la Mazezeta
 
kuliko kuzidi kuwaminya wananchi izo trilioni 2 zinaweza kabisa kupatikana kwa serikali kubana matumizi ya anasa na kuthibiti wizi wa pesa za walipa kodi kwenye taasisi za umma,sambamba na kufuta kabisa mashirika kausha damu kama ttcl,TANOIL n,k.
Serikali inatafuna sehemu kubwa ya bajeti kuelekezwa kwenye matumizi waliyoyapa majina kama "matumizi ya kawaida" ambayo si ya lazima.

Kumbuka watumishi wengi tunaishi nao huku mtaani na tunajua namna wanajipatia fedha kwa njia haramu au ambazo si sahihi.

Kama tukiwa serious na kuja na mfumo mpya wa uendeshaji wa serikali then nina uhakika kuwa watasave zaidi ya hizo trillion mbili.

Huu upuuzi wa kuwajazia tozo za buku buku raia ni kuyatafuta mapinduzi na wote waliohusika watachezea kitanzi very soon.
 
Huyu dawa yake ni kuacha kupanda zile daladala zake za mikoani .............tuone huu upya upya atamweleza nani?
 
Adui yetu namba Moja ni CCM
 
sawa sasa na sisi tuache kupanda gari zake mbona sisi ndio washindi
 
Tupeni mbadala,yale ni mawazo yake ya hesabu na zile ni data zake,elfu 2000 kwa mwezi na nchi nzimabtutibiwe bure we inakuuma.
Hakunaga bure kwenye nchi iliyooza kwa rushwa kama hii! Imagine leo hii tu watu wamechangia bima ila still ukifika dirisha la dawa kati ya dawa 5 utapewa mbili halafu 3 zilizobakia ukajinunulie mwenyewe.
 
Ungejua watz wanakufa kwa kukosa mia tano usingeropoka nini elf mbili hata ulewi
 
Wabongo kwa ulalamishi nini elf 2 kuokoa milioni 2 za matibabu
Kukatwa buku 2 haina shida mkuu tatizo hizo hela zinaenda kweli kufanya lililokusudiwa? Ama kuna wacenge wachache fedha zikifika hazina watagawana billion 60/60 za michango na kwenda kujenga maghorofa mbweni na kununulia mabasi na malori?
 
Hatuna shida na hilo swala la kuchangia ila tunachotaka ni accountability sio siasa baada ya michango kukusanywa. Ikiwezekana mfuko huo uwe wa raia na account iwe specific ya michango ya bima isiingiliwe na mafisadi wa CCM wala matumizi tofauti na kulipia bill na dawa za wagonjwa tu.

Hela za michango tuwe na access ya kuona zimekusanywa ngapi na matumizi yake yawe yanawekwa wazi kwa kila raia kwamba mwezi huu umechangia ngapi, jumla mfuko una bei gani in real time sio mambo ya kutuzuga kama tozo za miamala zilivyokuwa zinakatwa halafu wanaficha taarifa za makusanyo matokeo kinakuwa kichaka cha wizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…