Pre GE2025 Kama Nape na Makamba wamewekwa kando, si Mwigulu, Biteko, Tulia, Mwinyi, Makonda wala Majaliwa watamrithi kiti Rais Samia

Pre GE2025 Kama Nape na Makamba wamewekwa kando, si Mwigulu, Biteko, Tulia, Mwinyi, Makonda wala Majaliwa watamrithi kiti Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Special Seat

Senior Member
Joined
Jul 21, 2024
Posts
169
Reaction score
301
Wanabodi,

Baada ya team moja ya wasaka Urais iliyotumia muda mwingi kujiandaa kuangushwa ni dhahiri kabisa team hii haitakaa kimya kwani hata hivyo team hii pia kama zilivyo team zingine inamtandao mpana ndani na nje ya Tanzania naamini tunaufahamu.

Kitendo Cha team hii kuangushwa wataamini kabisa ni team kinzani ndio zimefanya uchochezi kwa Rais ili kuiangusha team yao hiyo iliyomteua Mhe January Makamba kama kinara wa team.

Nikitazama ukwasi na ushawishi ilionao team hii ya kinara January Makamba nashawishika kuamini si Mwigulu, Biteko, Makonda, Tulia, Mwinyi, Mchengerwa, Jaffo, Bashe, Kikwete wala Majaliwa wataunusa Urais 2025 wala 2030.

Kuna ule usemi maarufu wa kiswahili unaosema "Ukimwaga Mboga Mimi na mwaga Ugali" tutarajie miangushano mikubwa kati ya sasa na 2030 kwani hizi team ni hakika na hii vita ni ukweli pia.

Baada ya mtifuano huo huenda Rais wa 2030 atakuwa ni mtu mpya lakini lazima awe mwenye kuchukia kabisa matendo ya rushwa na ufisadi na huenda asitoke kwenye team yoyote kati ya hizo kwani Kila team haitakuwa tayari kuona ikifukuzwa kama sio kutoroka kabisa Tanzania baada ya team kinzani kushinda nafàsi hiyo.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Rais Samia.

Pia soma: Uteuzi na Utenguzi: Nape, January na Byabato out! Jerry Silaa ahamishiwa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Makamba kwa miaka mingi anayo sifa ya upigaji. Samia kumpa uwaziri ni katika kulipa fadhila kwa kundi zima la Msoga. Hata huyo Nape kupewa uwaziri ni mwendelezo wa kumheshimu JK aliyemtoa Zanzibar na kumleta huku bara na kumpa cheo.

Kuna muda unafika hayo malipo ya fadhila yanapitwa na wakati na kupoteza nguvu na uhalali. Makamba anaweza kurudishwa baadae katika uwaziri lakini tayari analo doa la upigaji tena ule mkubwa.

Mkurugenzi mmoja wa mamlaka kubwa serikalini aliniambia kuhusu kuondolewa kwa Makamba karibu miezi saba iliyopita, lilikuwa ni suala la muda tu.
 
Anaweza asiwe na ushawishi ila anateam strong lazima ulijue hili pia
 
Anaweza asiwe na ushawishi ila anateam strong lazima ulijue hili pia
Rais anakuwa na malengo ya kitaifa siku zote anaitazama picha pana inayokuwa mbele yake. Hawajaandikiwa watu fulani na familia zao eti ndio wawe viongozi wetu wa kudumu na bahati mbaya tabia hiyo inapoota mizizi inaleta dharau kwa watu walio wengi.

SSH kanifurahisha kuwaondoa hawa mawaziri wawili wazoefu.
 
Huwezi kumpuuza January hata hivyo
 
Back
Top Bottom