Pre GE2025 Kama Nape na Makamba wamewekwa kando, si Mwigulu, Biteko, Tulia, Mwinyi, Makonda wala Majaliwa watamrithi kiti Rais Samia

Pre GE2025 Kama Nape na Makamba wamewekwa kando, si Mwigulu, Biteko, Tulia, Mwinyi, Makonda wala Majaliwa watamrithi kiti Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Rais anakuwa na malengo ya kitaifa siku zote anaitazama picha pana inayokuwa mbele yake. Hawajaandikiwa watu fulani na familia zao eti ndio wawe viongozi wetu wa kudumu na bahati mbaya tabia hiyo inapoota mizizi inaleta dharau kwa watu walio wengi.

SSH kanifurahisha kuwaondoa hawa mawaziri wawili wazoefu.
Unasema nini mkuu? Unafahamu jinsi Samia alivyowajaza ndugu zake ikulu na serikalini na pia jinsi alivyowajaza wazanzibar na wapemba ktk sehemu nyeti hapa Tanganyika? Wewe hili hulioni?
 
Tulia hatoshi kuwa Rais. Sisi tuliopitia jkt tunajua nini faida yake kiusalama na uzalendo. Lakini yeye juzi kaongoza Bunge kusema hicho kigezo kwa vijana wa Kitanzania hakina maana.
 
Wanabodi,

Baada ya team moja ya wasaka Urais iliyotumia muda mwingi kujiandaa kuangushwa ni dhahiri kabisa team hii haitakaa kimya kwani hata hivyo team hii pia kama zilivyo team zingine inamtandao mpana ndani na nje ya Tanzania naamini tunaufahamu.

Kitendo Cha team hii kuangushwa wataamini kabisa ni team kinzani ndio zimefanya uchochezi kwa Rais ili kuiangusha team yao hiyo iliyomteua Mhe January Makamba kama kinara wa team.

Nikitazama ukwasi na ushawishi ilionao team hii ya kinara January Makamba nashawishika kuamini si Mwigulu, Biteko, Makonda, Tulia, Mwinyi, Mchengerwa, Jaffo, Bashe, Kikwete wala Majaliwa wataunusa Urais 2025 wala 2030.

Kuna ule usemi maarufu wa kiswahili unaosema "Ukimwaga Mboga Mimi na mwaga Ugali" tutarajie miangushano mikubwa kati ya sasa na 2030 kwani hizi team ni hakika na hii vita ni ukweli pia.

Baada ya mtifuano huu Rais wa 2030 atakuwa ni mtu mpya mwenye kuchukia kabisa Matendo ya Rushwa na Ufisadi na hayuko kwenye team yoyote kati ya hizo kwani Kila team haitakuwa tayari kuona ikifukuzwa kama sio kutoroka kabisa Tanzania baada ya team kinzani kushinda nafàsi hiyo.


Mungu ibariki Tanzania,
Mungu mbariki Rais Samia​
Deep state ndiyo huamua nani awe rais,rostam na marehem mamvi wanaijua shughuli ya deep state,pesa zako hazitokusaidia wakati ukifika
 
Makamba kwa miaka mingi anayo sifa ya upigaji. Samia kumpa uwaziri ni katika kulipa fadhila kwa kundi zima la Msoga. Hata huyo Nape kupewa uwaziri ni mwendelezo wa kumheshimu JK aliyemtoa Zanzibar na kumleta huku bara na kumpa cheo.

Kuna muda unafika hayo malipo ya fadhila yanapitwa na wakati na kupoteza nguvu na uhalali. Makamba anaweza kurudishwa baadae katika uwaziri lakini tayari analo doa la upigaji tena ule mkubwa.

Mkurugenzi mmoja wa mamlaka kubwa serikalini aliniambia kuhusu kuondolewa kwa Makamba karibu miezi saba iliyopita, lilikuwa ni suala la muda tu.
Pambaneni na Ufisadi nda ya ccm na serikali yake.

Swala la Makamba kupaya au kukosa Uwaziri haina Tija kwa Watanzania zaidi ya Chuki binafsi tu na kuendelea kujazana ujinga.
 
IMG-20240723-WA0002.jpg
Alafu ukiwaangalia nyuso zao zinaonekana wameishatia vyombo!
 
Back
Top Bottom