Kama Nchi ziliweza kutoa nguvu za Wafalme, iweje sisi wenye Rais

Kama Nchi ziliweza kutoa nguvu za Wafalme, iweje sisi wenye Rais

Omary - Msamalia

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2020
Posts
2,077
Reaction score
4,525
Ndugai usikubali kufa kindezi (Misemo ya vijana), Wewe ni Kiongozi wa Muhimili wa Bunge na Kikatiba una nguvu za kusikiliza Hoja za kumtoa Rais au hata kuchana speech yake.

CCM wachache wanataka nafasi ya Uspika ili na wao wale kama wewe ulivokula, lakini usikubali kuiacha kizembe.

Sio Lazima Bunge kuwa upande wa serikali muda wote, utamaduni tu wa chama chenu, na sio lazima ufatwe kila wakati, kuna vitu vya ovyo Bunge linabidi lisimame na wananchi.

Ndugai Speaker anaweza kujitangaza Rais, na nchi ikawa na Marais Wawili hadi pale maji yatakapotulia.

Ndugai usijiuzulu ni muda sasa wa kutumia mamlaka ya Speaker ipasavyo.

80% na zaidi ya Watanzania na huko Kwenye Chama chenu hawako tayari kuongozwa na Rais mwanamama
 
Speaker hawezi kuachia ngazi kizembe hivyo.
 
Sio tu Mwanamama, Bali mwanamama mswahili ambaye kadiri kupambana na wanyonge, huku Akikumbatia wachache.

Huyu Mwanamke, Hafai.
Ukikumbatia sana wanyonge nchi itakuwa maskini kama enzi za magufuli maana hao wanyonge watataka kila kitu kiwe bure hata vile vyenye gharama katika uendeshaji wao watataka iwe bure matokeo yake anakopa kimya kimya na kunyang'anya fedha kwa matajiri kwa mtutu wa bunduki ili kuficha aibu

Ili mambo yaende mambo yote yanatakiwa yawe balanced
 
Ungekuwa ndungu yagu wewe ningebadilishana na gunia la ufuta
Ndugai usikubali kufa kindezi (Misemo ya vijana), Wewe ni Kiongozi wa Muhimili wa Bunge na Kikatiba una nguvu za kusikiliza Hoja za kumtoa Rais au hata kuchana speech yake...
 
Rais alistahili kumjibu Ndugai kwa staha bila ya kujali kama kauli yake ilikuwa sahihi au hapana.

Kumjibu Spika wa Bunge (japo ni Bunge bandia kwa sababu wabunge wake, wengi wao ni bandia), ni dhihirisho tosha kuwa kuna shida kubwa kwenye mfumo wetu wa utawala.

Rais kambbikia kesi Mbowe na kumweka ndani eti kwa sababu hamheshimu. Mentality hiyo hiyo inaonekana huyu Mama anayo dhidi ya kila mtu. Wanaoshamgilia Mbowe kubbikiwa kesi, wajue kuwa hata wao hawapo salama.

Huu ni wakati wa Ndugai kiyafuta makosa yake yote ya siku za nyuma, na hilo atalifanya kwa kusimama na wananchi. Anatakiwa ahakikishe kila kinachoingia Bungeni kinajadiliwa kwa maslahi ya nchi, na siyo kwa maslahi ya Serikali au chama.

Bunge limepewa na katiba yetu (hii hii mbovu), uwezo hata wa kumwondoa Rais, japo utaratibu wake ni mrefu ja aghali. Hatumshauri amwondoe Rais Samia, bado naamini Samia ni Rais mzuri lakini kuna mengi anatakiwa kujirekebisha, ila tunachomshauri Ndugai, hastahili kuwanyonge, anayebabaika bila sababu za msingi.

Ndugai anastahili kuwa thabiti alimradi kama uthabiti unaegemea kwenye sheria, katiba ya nchi na maslahi ya umma.

Kikubwa kwa sasa, Taifa linahitaji katiba mpya ili kusiwepo na wa kumtisha mwingine, hata wakati hajafanya kosa.
 
Rais alistahili kumjibu Ndugai kwa staha bila ya kujali kama kauli yake ilikuwa sahihi au hapana.

Kumjibu Spika wa Bunge (japo ni Bunge bandia kwa sababu wabunge wake, wengi wao ni bandia), ni dhihirisho tosha kuwa kuna shida kubwa kwenye mfumo wetu wa utawala.

Rais kambbikia kesi Mbowe na kumweka ndani eti kwa sababu hamheshimu. Mentality hiyo hiyo inaonekana huyu Mama anayo dhidi ya kila mtu. Wanaoshamgilia Mbowe kubbikiwa kesi, wajue kuwa hata wao hawapo salama.

Huu ni wakati wa Ndugai kiyafuta makosa yake yote ya siku za nyuma, na hilo atalifanya kwa kusimama na wananchi. Anatakiwa ahakikishe kila kinachoingia Bungeni kinajadiliwa kwa maslahi ya nchi, na siyo kwa maslahi ya Serikali au chama. Bunge limepewa na katiba yetu (hii hii mbovu), uwezo hata wa kumwondoa Rais, japo utaratibu wake ni mrefu ja aghali. Hatumshauri amwondoe Rais Samia, bado naamini Samia ni Rais mzuri lakini kuna mengi anatakiwa kujirekebisha, ila tunachomshauri Ndugai, hastahili kuwanyonge, anayebabaika bila sababu za msingi.

Ndugai anastahili kuwa thabiti alimradi kama uthabiti unaegemea kwenye sheria, katiba ya nchi na maslahi ya umma.

Kikubwa kwa sasa, Taifa linahitaji katiba mpya ili kusiwepo na wa kumtisha mwingine, hata wakati hajafanya kosa.
Ni wakati wa Ndugai kuwapa Watanzania kitu wanataka
 
Nimekuelewa. Ndugai asimame kiume hadi mama aombe msamaha.

Sio kujimwambafai tu.

Amesutwa Ndugai aibu naona mimi ati.
 
Ukikumbatia sana wanyonge nchi itakuwa maskini kama enzi za magufuli maana hao wanyonge watataka kila kitu kiwe bure hata vile vyenye gharama katika uendeshaji wao watataka iwe bure matokeo yake anakopa kimya kimya na kunyang'anya fedha kwa matajiri kwa mtutu wa bunduki ili kuficha aibu

Ili mambo yaende mambo yote yanatakiwa yawe balanced
Well spoken [emoji106][emoji120]
 
Back
Top Bottom