Kama ndio inakutokea, utachukua hatua gani?

Mnyenz

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2014
Posts
2,933
Reaction score
8,112
Upo kwenye daladala kuna sehemu labda unaelekea katika mihangaiko yako ya kila siku, unapofika sehemu husika unashuka na kuanza kutembea, katikati ya safari yako ukiwa huna hili wala lile unashtuliwa na kofi moja zito la uso linalokupelekea kufumba macho, kabla huja kaa sawa inakuja ngumi ya uso halafu unasikia sauti ya anaekupiga ikisema "NILIKWAMBIA IPO SIKU NITAKUKAMATA TU" Ile kuinua sura unakutana na sura usiyoifaham kabisaaa! Halafu na yeye anashtuka baada ya kukuona kisha anakwambia "SAMAHANI NIMEKUFANANISHA" Je, ni uamuzi gani utauchukua???
 
dah hapa msamaha pekee ndio utakua suruhisho la timbwili ili asigeuke fundi rangi.
 
dah hiyo nayo kali........ukiwa na hasira za karibu unachafua hali ya hewa
 
Upo kwenye daladala kuna sehemu labda unaelekea katika mihangaiko yako ya kila siku, unapofika sehemu husika unashuka na kuanza kutembea, katikati ya safari yako ukiwa huna hili wala lile unashtuliwa na kofi moja zito la uso linalokupelekea kufumba macho, kabla huja kaa sawa inakuja ngumi ya uso halafu unasikia sauti ya anaekupiga ikisema "NILIKWAMBIA IPO SIKU NITAKUKAMATA TU" Ile kuinua sura unakutana na sura usiyoifaham kabisaaa! Halafu na yeye anashtuka baada ya kukuona kisha anakwambia "SAMAHANI NIMEKUFANANISHA" Je, ni uamuzi gani utauchukua???

Kwani wewe ulivyopigwa ulichukua hatua gani?
 
ukitembea kifala ---- hayo lazima yakukute, kofi mpaka litue usoni wewe ulikuwa umelala ukitembea? kisha ngumi juu? naupigwe tu!! tena kwa kufananishwa, na mimi ukimalzwa kufananishwa nakuja kukufananisha tena.
 
hahahahahahahahahahahah! jamani mimi m bavu zanguuuuuuuuuuu!hapa baba mimi ngumi ya kwanza ni nduki sisubiri nitajua badae maana wenda adui kweli....!
 
Mtu akikupiga kofi la kushoto,mgeuzie na la kulia.
 
Patachimbika! Unidhalilishe halafu useme nimekufananisha! Hapo tutakuja patana akiwa pale Muhimbili (MOI).
 
Upo kwenye daladala kuna sehemu labda unaelekea katika mihangaiko yako ya kila siku, unapofika sehemu husika unashuka na kuanza kutembea, katikati ya safari yako ukiwa huna hili wala lile unashtuliwa na kofi moja zito la uso linalokupelekea kufumba macho, kabla huja kaa sawa inakuja ngumi ya uso halafu unasikia sauti ya anaekupiga ikisema "NILIKWAMBIA IPO SIKU NITAKUKAMATA TU" Ile kuinua sura unakutana na sura usiyoifaham kabisaaa! Halafu na yeye anashtuka baada ya kukuona kisha anakwambia "SAMAHANI NIMEKUFANANISHA" Je, ni uamuzi gani utauchukua???

Pole! atakuwa alikufananisha na mgoni wake ,
 
Back
Top Bottom