Kama ni kweli, basi comrade Kinana amepuuzwa!

Alivyoondoka kwenda kwenye matibabu ukimuona? Au ulipewa taarifa tu?
Usilazimishe watu wakubaliane na umbea wako wa kiume, kwa hiyo wewe ndo msemaji wa familia ya Mzee Kinana?
Wewe na wenzio wenye akili kama zako mmekalia umbea na kuchunguza mambo ya watu. Pia kuchunguza sio tatizo, tatizo ni kuzusha mambo yalio nje ya uwezo wako.
Na kimtazamo unaonesha una tatizo hata kwenye familia yenu. Na sio mfano nzuri wa familia na jamii.
Kuumwa sio sifa nzuri, kuna wengine hawataki watangazwe mambo yao hadharani. Na hata kama Mzee Kikwete huwa anaenda kumsalimia sio lazima jamii mzima ijuwe.
 
Muhimu jibu hoja, hii post haina uhusiano wowote na post yoyote ya siku za nyuma. Najiuliza hivi inawezekana Mheshimiwa Kinana atoke kwenye Matibabu halafu Jakaya asiende kumjulia hali? Lazima kuna kitu tofauti.
Tangazia uma wa watanzania na tuaminishe hiyo tofauti wewe.
 
Hata kuumwa mguu kwa mwenyekiti wa NCCR Mbatia tumeona kwenye TV na magazeti,huyu Abdu mmmhhh .
 
Mbona sioni tatizo lolote....

Mmeumbuka kwenye ndege na huyo mpiga picha wenu sasa mmeibuka na non issue kuhusu mzee Kinana....

Bado nacheka kuhusu mpiga picha Woody....😀
hahahaha mpiga picha ilibidi abadili gear angani hahaha
 
Wabongo tunapenda sana udaku
Unasoma habari huku tayari ukiwa na majibu yako halafu unakuja kufungua thread,unaandika "Kama ni kweli"
Kinana ni Mtanzania awe Arusha au Dar es salaam,haiwahusu watu zaidi ya familia yake,viongozi wake na watu wa karibu tu.
Kama kawaida Bavicha mnajaribu kutengeneza tukio ili iwe hoja kwa kutumia ugonjwa wa mtu kama mlivyotaka kufanya kwa Mwamunyange,hii ni mbaya sana
 
Viongozi wa dini hebu ingilieni hili swala liishe mara moja.....mzaha mzaha uzaa usaa.
Hawawezi, tena hasa wale wazee wa waraka elekezi ndio hutawaona kabisa. Hii timua timua ingefanywa na alhaji dangadunguri maandamano yangefika feri. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa sasa ni ngumu sana kwa wanaCCM kufarijiana hasa kama wakijua anayehutaji faraja hana mahusiano mazuri na baadhi ya viongozi wenye 'say kubwa' ndani ya chama.

Msisahau dhahama ilotaka kuwapata waloenda kumuona Lema Kisongo.

Nyie vp???
Komredi hakubaliani na panga pangua za vijana alioamini kabisa ndio warithi wa chama kwa juhudi zao zakukubali kufa ila chama kipite.

Hakubali kabisaaaaaa
 
alivoondoka mbona pia hamkusema kwanini ameondoka kimya kimya??mbona mbatia ameenda kutibiwa amerudi kimyakimya hakuna aliyehoji kama mnavohoji juu ya kinana??
Hakuondoka, alitumwa, sasa amerudi nendeni mkamsalimie basi
 
Yangu lini mbowe akawa muungwana
 
Jibu hoja ni kawaida kwa kiongozi wa ngazi ya juu kama KATIBU MKUU wa chama kurudi kimyakimya? Imeanza lini? Au nako ni kubana matumizi?

Mbona tokea enzi za kikwete kinana alikuwa hapendi kupokelewa anaporudi kutoka safari za njee, iwe kikazi au binafsi.

Hata alipokuwa waziri kinana alikuwa hapendi maonyesho, yeye sio mpenda publicity, anachokifanya kinakuwa strategically executed.
 
Ana umwa ugonjwa gani? Marufuku ya mwenyekiti siku hizi ni aina mpya ya ugonjwa?
Mzee kinana siku ile ulipoandika barua ya kujiuzulu ndio ulikua uponyaji wako kwa huu ugonjwa wa mwenyekiti.
 

In Tanzanian politics , please clarify for us which are dirty hands and which are clean?

You are criticizing this gentleman for supporting the party he believes in , that's Democracy, or to you it's the G W Bush methalogy " YOU ARE WITH ME OR YOU ARE CONDEMNED "

As the supporter of the other side does it means you receive the crumbs of a golden loaf.

I wonder in this situation between you and the other gentleman who is the stupid one? I believe if you have any bornwith intelligence you will see faults and like a true gentleman, will apologize for the insults. Otherwise you will prove to us differently and we shall judge you so.
 
Unaweza kuwa sahihi kwa kiasi fulani. Lakini inawezekana daktari wake ameshauri mgonjwa apewe muda mrefu wa kupumzika (Strict Bed Rest = SBR). Kwa kutambua wadhifa wa mgonjwa kwa jamii mlolongo wa watu kwenda kumtembelea ni expected, kitu ambacho kinaweza kuwa na madhara kwake. Hivyo masharti ya daktari ya SBR yanapaswa kuzingatiwa na ndiyo maana kurejea kwake hakukutangazwa.

Cha mhinu tumuombee kwa Mwenyezi Mungu amrejeshee afya yake kiongozi wetu mpendwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…