Kama ni kweli, ni picha gani unapata hapa??

Kama ni kweli, ni picha gani unapata hapa??

Si umeona sasa nilikwambia jana kuna hata wazee hovyo umemuona huyu sasa?? Nilkwambia mapemaaaa baki tu huyo sharobaro wako

Mwambie maana asifikirie kila mzee anafaa kuwa wa maana
Wengine ndo hao kula kulala
Unajikuta kila kitu anakutegemea wewe
 
Mwambie maana asifikirie kila mzee anafaa kuwa wa maana
Wengine ndo hao kula kulala
Unajikuta kila kitu anakutegemea wewe
mmmh wewe ujana wake ale na nani mimi nije kumlisha uzeeni afie mbele huko
 
mbona hajaweka wazi matumizi ya nyumba gani mimi nashaka kuwa sio nyumba yake inawezekana kwa familia ya mkewe vipi adai gharama za nyumba yake? na kama ni hivyo inawezekana huyo mdada aliwahi olewa anawatoto lakini ndo anaishi nae kiaina
 
ndo wanaume wa siku hizi. Wanalelewa. Wananunuliwa mpaka nguo za ndani. Wapo ambao hawajui hata ada ya watoto inatoka wapi!

Wakati mwingine kina dada wanakosea kuendana na wanaume kwani pindi ukianza lipa bills na kadhalika yeye atajikausha na kufanya liwe jukumu lako...vitu vingine ni kuendekeza tu ndio maana vinakua na mwisho vyaleta taabu....

Vin Diesel acha tu kaka yangu but nasema pia kuna wanawake wana bahati! Jamani.

My sisy...heri yake yule atakaepata mume bora...ukilamba garasa utaishia kuwa philosopher....
 
Khaaa!!! Huyu mwanaume kiboko sasa anamuandika email mke wake yenye hayo maneno ina maana mke wake amekuwa secretary siku hizi, halafu kudai hela uliyolipa umeme urudishiwe hii nayo kali sasa kama wana watoto si ajabu akilipa ada ya mtoto atadai mke wake pia amrudishie hela pia, ngoja niendelee kutafakari maana kuna ndoa zingine zina viroja kama sio vioja

Mwanaume lazima uwe na msimamo.
Nitajuaje huyo Suzzy alipitiwa na usingizi? Kama ndo hivyo basi tuwe tunajuliana khali ijumaa basi
 
Yani kuna watu wengine ndoa zao utadhani walilazimishana!
 
Dears,
Wakati MJ1 mie naomboleza na ya kwangu, leo asubuhi nakutana na simu ya rafiki yangu ambaye alikuwa analia simuni kiasi cha kumwomba anisms tatizo ni nini. Akaamua kuniandikia mail ya kilichomsibu;

Yeye na Mr wake wanaishi mbalimbali kutokana na kutafuta maisha. Dada Suzzy (Si jina lake halisi) anaishi nje ya nchi lakini within EAC na mumewe anaishi nchini.

Juzi jumapili Da Suzzy anasema kapigiwa simu na shemeji lakini kwa bahati mbaya alikuwa amejipumzisha hakuisikia (ilikuwa ni jioni kwenye saa kumi na mbili jioni). Lakini alipoamka na kukuta missed call, akataka kucall back, only to realize kuwa hana credit kwenye simu na huko anakokaa ni mbali na maduka. So hakuweza kupiga but akajihimu alfajiri kwenda mjini kununua voucher akampigia shemeji hakupokea, akatuma sms ya kuomba radhi ya kushindwa kuwasiliana hakupata majibu. Lakini baada ya masaa mawili, akiwa kazini akakutana na e-mail ilotoka kwa Mr wake ikisema-
kuanzia muda sasa hatokuwa anapokea simu za mkewe hovyo, na muda alioamua ni fridays mchana na mwisho saa nne tu.


Da Suzzy a
nasema amechanganyikiwa, hajui la kufanya maana anajiona kama anatumika tu kwani kwa muda wamekuwa na matatizo na Mr wake (Haya sikuwa nayajua hadi leo). Anasema mumewe kwa sasa anamdai pesa ambazo amezitumia kwa kulipia matumizi ya nyumbani huku TZ kama maji na umeme, Mama ni among ya wale ambao wanatake care kila kitu ndani ya familia, mf. matengenezo/insurances za gari la familia, chakula cha familia n.k.

Silaumu lakini ninayo mawazo juu ya hili, ila kabla sijamweleza lolote ninaomba tusaidiane, maana ninaweza kuwa ninachokifikiria sicho.

Peleka kwenye magazeti ya UDAKU
 
unaachosema ni kweli, wanawake wanayalea haya. Usikute toka wanaanza mahusiano mwanamke ndo analipa, labda kwa ujinga wa kudhania ndo anabembelezea ndoa wakifikiri kwenye ndoa watabadilika. Mwisho wa siku wanabeba mzigo wote wenyewe.

Hivi kwa nini umuhonge mwanaume? Kwa nini uwe na mwanaume asiyetambua wajibu wake?

Ajabu!
 
Back
Top Bottom