Kama ni kweli ninapinga kwa Papi Ousmane Sakho 'Kutemwa' Simba SC

Wasilogwe wamuache Sakho..... SITAIFANYIA CHOCHOTE SIMBA.. Banda hamna kitu, Duncan Nyoni hamna kitu, Wawa na Kagere umri umeenda..... SAKHO AKIACHWA SIFUATILII SIMBA TENA..... cha mwisho itakuwa hiyo hela niliyochangia ujenzi wa uwanja.
 
Kama Sako katemwa basi mimi ndoa yangu na Simba ishaisha hata mchango situmi, watu wanaendeshwa na mihemko haiwezekani unamtoa dogo kumleta babu!

Chama nampenda lakini kwa hili ilitakiwa tu move on
 
Wasilogwe wamuache Sakho..... SITAIFANYIA CHOCHOTE SIMBA.. Banda hamna kitu, Duncan Nyoni hamna kitu, Wawa na Kagere umri umeenda..... SAKHO AKIACHWA SIFUATILII SIMBA TENA..... cha mwisho itakuwa hiyo hela niliyochangia ujenzi wa uwanja.
Nikajuwa niko peke yangu mwenye hayo mawazo!

Sako Banda Duncan wote wazuri wamekosa game time tu! Tuko desperate sana haikuhitajika kusajiri kabisa hili dirisha ukizingatia robo tatu ya usajiri wetu mpaka sasa haujatumika!

Wasituletee oya oya zao
 
Agiza K Vant nakuja
 
Yatakuwa ni maajabu ya Dunia Simba kumwachq yule mtoto Sakho....kaama kina ulazima, wamttoe Wawa, Mugalu au Nyoni!
Halafu Kuna watu wanamtukana Boko,mwisho wa msimu ndiye mfungaji Bora ,hebu mwachemi mwenye Ligi yake Hadi atakapo staafu
Hivi,ni kweliSimba ilikuwa inamhitaji Chama au ndiyo.kuogopa kuwa angeenda Yanga!
 
Mchezaji mzuri hasubiriwi eti kwa kupewa muda.
Sackho
Duncan
Mugalu
Hawa ni wakusitishiwa mikataba yao.
Hawana cha ajabu.
Wana rukaruka tu kiwanjani.
 
Kwanzia kwa Chikwende niliamini Simba ujinga mwingi sana acha wapambane na kunguni zao wenyewe.
 
Morison,Banda na bwalya mm naona ndio Vimeo.
Duuuh alafu wakiondoka hao ndio nn Sasa au unataka kuwavuruga Wana Simba ,hao ndio injin za Simba Wana msaada mkubwa sana
 
Genta nunakuunga mkono.
Simba wasifanye makosa ya kumtema Sakho.
Viongozi kama wapo mnaopitia mada za humu, wekeni akilini juu ya mada hii na kuifanyia kazi.
Poti wangu Mshauri Mkuu wa Mwekezaji Crescetius Magori huwa ananisoma mno kama si sana tu hapa JamiiForums hivyo naamini atakuwa ameshanisoma na kufuata huu Ushauri wangu.
 
Wataje hao wachezaji wanaompiga miba ili tuwashughulikie,wasituharibie timu yetu
 
Mliuza mabasi na mmesajiri magarasa sasa mnataka kuyaacha.
Wenzenu yanga wamemchukua wonder kid Denis nkane kweli yanga wako juu
 
Simba inapata wachezaji wazuri alafu wanawaweka benchi au kuwaacha.
Ibrahim Amme.
Kahata.
Shiboob"Zizou".
Fraga.
Abdullswamad.
Chikwende.
Sakho.
Simba inakosa utulivu kwa wachezaji wa kubaki na wakuacha.
Sijui kwanini Yanga tusimbebe uyu Chikwende, jamaa anajua kweli kweli huyu.
 
Nakuheshimu brother,ila kumuheshimu mwalimu ni kitu kizuri.

Hizo imani za miba sijui nini,hazina ushahidi.
Kwa nini Luis na Chama hawakupigwa miba?
Sifurahishwi na upotoshaji mkubwa unaofanywa na watu wa mitandao kutoa sifa za kijinga kwa wachezaji kama vile Banda,Sakho n.k.
Tumwache mwalimu afanye kazi yake
 
Tatizo kassim dewji hana weledi wa kusajili, akiwa katibu mkuu simba alidanganya ramadhan wasso kapata timu ubelgiji kumbe kaishia airport kamuuza yanga. Baada ya kuwatoa zamalek na kuingia makundi alimsajili clement kahabuka toka uarabuni ambaye akiwa uwanjani anaishia kuanguka na hakuna cha maana alichoongeza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…