Nakuheshimu brother,ila kumuheshimu mwalimu ni kitu kizuri.
Hizo imani za miba sijui nini,hazina ushahidi.
Kwa nini Luis na Chama hawakupigwa miba?
Sifurahishwi na upotoshaji mkubwa unaofanywa na watu wa mitandao kutoa sifa za kijinga kwa wachezaji kama vile Banda,Sakho n.k.
Tumwache mwalimu afanye kazi yake
Sihitaji Kuheshimiwa na Wewe, hujui Mpira na tafadhali acha Kunipotezea muda sawa?
Sakho ni zaidi ya Chama na Miquissone kama akipewa muda na akiwa pia 100% Fit sawa?
Baadhi yenu ( Wanasimba ) ni Wapumbavu ( Mapopoma ) sana yaani mmesahau kuwa Chama na Miquissone walianza Kung'ara baada ya Msimu wa Kwanza ila leo mlivyo Wanafiki huyu Sakho ambaye kila Mtu anajua kuwa alikuwa ameanza vyema tu ila Majeraha ya ile Mechi yetu na Dodom Jiji FC ndiyo yalimpunguza Kasi hatutaki Kumvumilia na kumpa mwaka Mmoja zaidi.
Kuhusu Ushirikina ( Kupigana ) Miba kwa Wachezaji wa Ligi Kuu labda sasa leo nikuambie kuwa zaidi ya 75% ya Wachezaji wa Simba na Yanga ( hasa Wazawa ) na wachache wa Kigeni kama aliyekuwa Beki Wetu Mganda Joseph Owino Gera na Haruna Fadhil Hakizimana Niyonzima ni Marafiki zangu Wakubwa mno GENTAMYCINE Mimi na wameniambia na wananiambia mengi kuhusu Wao Kurogana ( Kupigana Miba ) huko.
Namalizia kwa Kukupa Mfano wangu halisi tu kuwa Mganga Mkubwa wa John Boko na Kipa Aishi Manula namjua na huwa nawaona hawa Wachezaji kila mara wakienda Kwake tokea akiwa anaishi pale Msasani Jirani na kwa Mwalimu Nyerere na alipohamia Kawe jirani na Baa maarufu ya Newcastle.
Nidanganye vyote ila siyo kwa Soka la Tanzania na bahati nzuri pia ni kwamba hata huu Mpira wenyewe nao nimeucheza tena kwa Kiwango kizuri tu katika Ngazi za Shule, Mtaa na Ligi Daraja la Tatu nikiwa na Watu kama akina Wycliffe Keto, Abdul Mweta, Samora ( Mdogo wake Dua Said ), Zubery Katwila, Renatus Njohole, Gwakisa Mwandambo, Marehemu Ali Yusuf Tigana na Monja Liseki sema tu Majukumu ya Elimu na 'Mikwara' ya Wazazi kukataa nisijihusishe na Mpira ndivyo vilinikwamisha na kuachana nao.
Ousmane Sakho asiachwe na Simba SC.