Kama nyani alibadilika akawa binadamu ni kwanini nyani na sokwe wa sasa hawabadiliki tena kuwa binadamu?

Hahahaaaa

Na wewe lini utakua sokwe?
Kuna wadau huku wanasema nasisi tutabadilika mamilioni ya miaka ijayo huko sasa najiuliza tukibadilika kutoka binadamu kama tulivyoaminishwa tulikua masokwe tutakua viumbe wa aina gani tena?
 
Kubali ulikuwa nyani, tena watu weusi bado Evolution haijakamilika...Nyani wasasa hawabadiliki kwasababu ya kimazingira

Ndio maana Dinosaureus hawapo tena, mazingira yalisababisha wafe, kuna aina ya Buffallo wenye manyoyq shingoni nao walikuwepo zamani sasahv hawapo tena

Kuna Simba wale wa mapangoni maarufu Caves Lion hawapo tena na walikuwa wakubwa kuliko hawa wa sasa

Kuna ndege pia walikuwepo sasa hawapo tena

Na hata Vifaru, Tembo na wanayama wakubwa karibu wote wapo mbioni kupotea

Hii hutokea hata kwa mimea
 
Unadhani mabadiliko ya viumbe huchukua vimiaka 10,20,60 uliyoishi/utakayoishi 😀😀 Hiyo milima unayoiona leo ilianza kama vichuguu na imechukua miaka zaidi ya milioni 260 mpaka unaiona leo. Evolution siyo process ya karne mbili au tatu, hizo ni 'era' Labda kama utaishi kufikia miaka bilioni!
 
Kama nyani wa sasa wanabadilika kidogo kidogo kua kama binadamu ni kwanini basi na sisi binadamu tusibadilike kidogo kidogo kua nyani ?
unapozungumzia kidogokidogo tunamaanisha miaka milioni 100 badiliko moja, milioni 100 badiliko lingine.... hivyohivyo! it's a slow process
 
Kuna wadau huku wanasema nasisi tutabadilika mamilioni ya miaka ijayo huko sasa najiuliza tukibadilika kutoka binadamu kama tulivyoaminishwa tulikua masokwe tutakua viumbe wa aina gani tena?
Humanoids - Robot like human
 
Kama tulifikia miaka 730M kwanini sahivi tupo 2024 . Ule mwaka wa kwanza (1) halali ni upi na kwanini walipunguza miaka?
Siku.
Dah .... miaka inahesabiwa kutokana na siku. Yaani dunia ilijizungusha kwenye mhimili wake kwa siku 730m. Zimepita siku milioni 730 tangu tulipokuwa kama masokwe.

Wewe huwezi kufikisha siku 40,000 za kuishi duniani utakuwa umeshaoza. Kwa hiyo get the picture.

Na siku 40,000 zilizopita, Tanzania watu walikuwa wanatembea uchi na kujisaidia maporini na kudandia miti. Hata leo wahadzabe bado wanalala mapangoni. Tusiende mbali zaidi.

Hujui hayo?
 
Kwani nyani wa sasa wamefikisha miaka milioni
 
Humanoids - Robot like human
Kuna uwezekano watu hawatakula nyama na watashangaa kuwa mababu zao walikuwa wanaua wanyama na kuwala.
Pia kuna uwezekano watu hawatatembea kwa miguu na miguu itakua haina maana sana.
Pia kufa kutakuwa ni jambo la ajabu.
 
Ingawa binadamu ana undugu mkubwa wa kibiolojia na sokwe na viumbe vingine, ustawi wake hauna mfano, kiasi cha kufanya wengi waamini kwamba tofauti iliyopo inadai kuelezwa kwa uwemo wa roho ndani ya mwili wake; roho ambayo dini hizo zinasadiki imetiwa na Mungu moja kwa moja.


HISTORIA INAONYESHA NDUGU ZETU NI SOKWE. SASA JE, KWANINI BASI TUJITENGE NA NDUGU ZETU NI NINI HASA KIMESABABISHA NA ILITOKEAJE TOKEAJE?
 
Miaka inahesibiwa kuanzia siku au miaka hiyo walipofanya huo utafiti/ugunduzi/ dating.
Pia mwaka namba 1 ni insignificant unapoongelea scale ya miaka laki au milioni kadha.
Hilarious 😂.

Mwaka wa kwanza hauwezi kuwa insignificant.

Kwako unaweza kuwa ni insignificant kwa sababu huna jibu.

Kwa sababu huna jibu, basi unaishia kubashiri tu na kurusha idadi kubwa ya miaka.
 
Haueleweki. "Miaka 200,000 iliyopita ilianza kuhesabiwa lini ?" ndiyo swali gani?
Kama hujalielewa swali langu basi utakuwa na kichwa kigumu sana.

Nadharia ya evolution inakosa kabisa mashiko mnapoanza kurusha idadi ya miaka ambayo ni muhali kuielezea kwa ushawishi.
 

Darwin na nadharia yake ya mageuzi ya spishi nadhani hutajaielewa vizuri, viumbe wenye tabia moja ambao wanaweza kuzalishana ndiyo wanaweza kubadilika kutokana na visababishi vya mazingira yao n.k. Siyo kubadilika kutoka spishi moja kwenda spishi nyingine. Uteuzi wa kiasili ndiyo unawafanya viumbe kuweza kuwepo hapa duniani.
 
Neno la Mungu katika bilblia ni zaidi ya evolution, kumbuka kitabu cha mwanzo kimeandikwa zaidi ya miaka 6000 iliyopita, je sayansi ulikiwa inasemaje wakati huo? Vituko

Hio evolution mnayoisifia mi ya Karne ya 20, je kabla ya hapo sayansi ilsemaje? Vituko,
Sayansi inabadilika kuithibotisha biblia!!

Biblia inasema Mungu alianza kuumba Jua, mwezi na nyota, baadae akayatenga majji na nchi kavu, Siku iliyofuata, akaumba mimea tofauti tofauti, Siku inayofuata akaumba samaki baharini, Siku inayofuata akaumba wanyama na ndege, mwishoni akamuumna mwanadamu.

Kumbuka neno Siku kwa kiebrania pia lilikiwa na maana ya "age".
Sasa ukiangalia huo mfuatano wa uumbaji evolution inasemaje!! Copy and paste!
 
hahahahahahahahahahahahahahahahaha.....
hahahahahahahahahahahahahaha.....
 
au kwanini sisi binafamu hatugeuki kuwa nyani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…