Kama nyani alibadilika akawa binadamu ni kwanini nyani na sokwe wa sasa hawabadiliki tena kuwa binadamu?

Kama nyani alibadilika akawa binadamu ni kwanini nyani na sokwe wa sasa hawabadiliki tena kuwa binadamu?

Shida kubwa haswa hapa ni kufundishwa na walimu ambao hawakuwa na maarifa sahihi kuhusu evolution. Binadamu hajawahi kuwa nyani, binadamu na nyani ni species tofauti kabisa. Ila kibaiolojia wana sifa zinazofanana na evolutionary they have the same ancenstors.

Ni sawa na mtu aseme ng'ombe alikuwa nyati, au mbuzi alikuwa suala (Hii ni kushindwa kuelezea evolution ni nini)
Evolution inaeleza namna viumbe vilivyopo sasa vinavyoshabihiana na kuelezea jinsi ambavyo viumbe hivi vinaweza kuwa na mzazi mmoja (the same Ancestors).

Kwa mfano speciaciation (aina za wanyama kwa majina yao) utaona ngombe anavofanana na nyati na wanyama wengine wa aina hiyo hii humaanisha hawa wanyama wana same ancestors ila kuna factors zilifanya wawe wanyama tofauti na sio ngombe alikuwa nyati kama wengi wanavochanganya.

Evolution is not linear. Kwamba mnyama x akabadili kuwa y mwisho awe z. Bali ni namna x y na z walivyo sasa ukilinganisha na vizazi vilivyopita.

Mfano mzuri: ni kama kuku wa kisasa na kienyeji, tunajua wote ni kuku na wamepatana kwa selective breeding yaani kujamiiana kwa kuku bora pekee.

Vipi kama kuku wa kienyeji walizaliwa wenyewe na wa kisasa wenyewe bila kuingiliana. Mwishowe utakuta hawa kuku wamekuwa tofauti kabisa na hawaingiliani tena.
 
Kwenye classification hakuna monkeys na apes. Kuna primates. Sisi sote. Yaani binadamu, nyani, sokwe(apes), lemurs, Orangutan nk nk ni primates. Tuna common ancestor. Kila mmoja ameevolve kwa namna yake.

Kulingana na evolution ya mwanadamu. Binadamu tulikuwa kama primates wengine. Tukiishi kwenye misitu ya Africa Mashariki. Tulijaa manyoya na tulikuwa na ngozi nyeupe. Tukiruka mitini. Kama sokwe walivyo na wanavyofanya leo.

Miaka 200K iliyopita tulitoka msituni na kuingia kwenye Savannah ya East Africa. Sababu ya jua la savvanah tukapoteza manyonya. Ngozi yetu nyeupe ikawa nyeusi. Na pilika za savannah zikafanya tutembee kwa kusimama, kutumia zana na maendeleo mengine. Kutoka hapo ndiyo tukasambaa dunia nzima.

Kwa ufupi, uhusiano wetu na "apes" ni kama uhusiano wa Chui, paka na Simba. Au ng'ombe na nyati. Ni wanyama wenye common ancestor. Walio kwenye order moja. Kusema binadamu wametokana na apes ni sawa na kusema Simba wametokana na Chui.
Apes ni primates wasio na mikia. Primates ni more general. Apes ni more specific than primates.
Ndiyo maana jamaa aliyesema nyani ilibidi aelezwe zaidi kwa sababu nyani Wana mikia na ni primates.
Tume evolve from tailless primates
Not monkeys and'em
 
Nimeeleza hapo awali kuwa tuna matatizo mengi sana ya kuelewa haya mambo kutokana na lugha tu.

Sasa hapo mtu anachanganya apes, chimpanzees, hominids, homo sapiens na nyani.

Inabidi muanze kufundishana Kiingereza kwanza kabla ya kuingia kwenye evolution
Kwa Tanzania kuna tabia ya kuamini masomo ya lugha, historia na sanaa zingine ni masomo ya siyo na tija.

Huwezi kujielewa na kubobea kwenye sayansi kama lugha hujaisoma vizuri.

Lugha hukomaza ubongo. Ukizoea kumuita mwanamke demu, basi hata ukikua hutamuheshimu mwanamke, ubongo wako unakuwa corrupted.

Hivyo hivyo kama apes wanaitwa nyani, basi ubongo unakuwa corrupted kuhisi ni nyani mwenye mikia badala ya nyani asiye na mikia.
I.e sokwe mtu.
 
Human evolution is the evolutionary process within the history of primates that led to the emergence of Homo sapiens as a distinct species of the hominid family that includes all the great apes.[1] This process involved the gradual development of traits such as human bipedalism, dexterity, and complex language,[2] as well as interbreeding with other hominins (a tribe of the African hominid subfamily),[3] indicating that human evolution was not linear but weblike.[4][5][6][7] The study of the origins of humans involves several scientific disciplines, including physical and evolutionary anthropology, paleontology, and genetics; the field is also known by the terms anthropogeny, anthropogenesis, and anthropogony.[8][9] (The latter two terms are sometimes used to refer to the related subject of hominization.)

The hominoids are descendants of a common ancestor.
Primates diverged from other mammals about 85 million years ago (mya), in the Late Cretaceous period, with their earliest fossils appearing over 55 mya, during the Paleocene.[10] Primates produced successive clades leading to the ape superfamily, which gave rise to the hominid and the gibbon families; these diverged some 15–20 mya. African and Asian hominids (including orangutans) diverged about 14 mya. Hominins (including the Australopithecine and Panina subtribes) parted from the Gorillini tribe between 8 and 9 mya; Australopithecine (including the extinct biped ancestors of humans) separated from the Pan genus (containing chimpanzees and bonobos) 4–7 mya.[11] The Homo genus is evidenced by the appearance of H. habilis over 2 mya,[a] while anatomically modern humans emerged in Africa approximately 300,000 years ago.
Mkuu unapoteza muda tu. Hapa deal na watoto wanaamini yule nyani anayerukaruka kwenye miti ya jirani kwanini habadiriki akawa mtu! Ahahahahaha!
 
Miaka 200,000 iliyopita tulitoka msituni?

Hiyo miaka 200,000 umeihesabuje?

Mwaka namba 1 ulikuwa lini na mwaka 200,000 ulikuwa lini?
Walipochunguza mabaki ya watu wa kale na kuyapima umri waligundua kuwa mabaki ya kale kabisa yanayofanana na binadamu wa leo ni kutoka miaka 200-300K iliyopita.
 
Mkuu kama ndivyo kwani hizo hatua za mabadiliko hatuzioni???
Evolution inaonekana kwa muda wa miaka michache kwenye microorganism kama bacteria.

Ndiyo sababu dawa za zamani za anti- bacyeria kama tetracycline siku hizi hazifanyi kazi.

Kwa vidudu vidogo kama bacteria evolution ni rahisi kuonekana katika miaka michache. Kwa sisi wakubwa evolution inafanya kazi polepole sana ni vigumu kuona mabadiliko.

Hiki hapa chapisho la kitaalamu kutoka The Lancet linaongelea antibiotic resistance na evolution

 
Mambo ya kishetani TU kwenda kinyume na asili halisi na ukuu wa Mungu....hii Dunia uongo ndo unanguvu.
 
Ndugu zangu.

1: Tukiachana na maswala ya kidini, historia inatuambia binadamu wa kwanza alikua ni nyani / sokwe /chipanze, sasa kama kweli binadamu tulikua ni manyani ni kwanini nyani / sokwe tunaowaona sasa hivi hawabadiliki kua binadamu na wala hawakatiki tena mikia na kua na mwili na utashi wa binadamu kama historia ilivyokua huko awali?

2: Je, kama kweli tulikua nyani na tukabadilika kua binadamu ni kwanini sahivi haiwezekani tena binadamu kubadikika na kurudia kua nyani kama wanasayansi wanavyodai?
Tulikuwa kundi moja na nyanyi na sokwe ila sisi hatukuwa sokwe wala nyani
 
Miaka 200,000 iliyopita tulitoka msituni?

Hiyo miaka 200,000 umeihesabuje?

Mwaka namba 1 ulikuwa lini na mwaka 200,000 ulikuwa lini?
Miaka inahesibiwa kuanzia siku au miaka hiyo walipofanya huo utafiti/ugunduzi/ dating.
Pia mwaka namba 1 ni insignificant unapoongelea scale ya miaka laki au milioni kadha.
 
Kwa mantiki hiyo Miaka 5000000 hivi mbele wanaume watakua hawana ndevu na nywele na sauti zitakua kama kasuku .
 
Kwa mantiki hiyo Miaka 5000000 hivi mbele wanaume watakua hawana ndevu na nywele na sauti zitakua kama kasuku .
Uwezekano huo ni mkubwa sana hasa ukizingatia wachina tayari hawana ndevu na waafrika baba na binti wate wanapaka mkorogo na manduli yanakwisha.
 
Ndugu zangu.

1: Tukiachana na maswala ya kidini, historia inatuambia binadamu wa kwanza alikua ni nyani / sokwe /chipanze, sasa kama kweli binadamu tulikua ni manyani ni kwanini nyani / sokwe tunaowaona sasa hivi hawabadiliki kua binadamu na wala hawakatiki tena mikia na kua na mwili na utashi wa binadamu kama historia ilivyokua huko awali?

2: Je, kama kweli tulikua nyani na tukabadilika kua binadamu ni kwanini sahivi haiwezekani tena binadamu kubadikika na kurudia kua nyani kama wanasayansi wanavyodai?
Hahahaaaa

Na wewe lini utakua sokwe?
 
Back
Top Bottom