Kama nyani alibadilika akawa binadamu ni kwanini nyani na sokwe wa sasa hawabadiliki tena kuwa binadamu?

Shida kubwa haswa hapa ni kufundishwa na walimu ambao hawakuwa na maarifa sahihi kuhusu evolution. Binadamu hajawahi kuwa nyani, binadamu na nyani ni species tofauti kabisa. Ila kibaiolojia wana sifa zinazofanana na evolutionary they have the same ancenstors.

Ni sawa na mtu aseme ng'ombe alikuwa nyati, au mbuzi alikuwa suala (Hii ni kushindwa kuelezea evolution ni nini)
Evolution inaeleza namna viumbe vilivyopo sasa vinavyoshabihiana na kuelezea jinsi ambavyo viumbe hivi vinaweza kuwa na mzazi mmoja (the same Ancestors).

Kwa mfano speciaciation (aina za wanyama kwa majina yao) utaona ngombe anavofanana na nyati na wanyama wengine wa aina hiyo hii humaanisha hawa wanyama wana same ancestors ila kuna factors zilifanya wawe wanyama tofauti na sio ngombe alikuwa nyati kama wengi wanavochanganya.

Evolution is not linear. Kwamba mnyama x akabadili kuwa y mwisho awe z. Bali ni namna x y na z walivyo sasa ukilinganisha na vizazi vilivyopita.

Mfano mzuri: ni kama kuku wa kisasa na kienyeji, tunajua wote ni kuku na wamepatana kwa selective breeding yaani kujamiiana kwa kuku bora pekee.

Vipi kama kuku wa kienyeji walizaliwa wenyewe na wa kisasa wenyewe bila kuingiliana. Mwishowe utakuta hawa kuku wamekuwa tofauti kabisa na hawaingiliani tena.
 
Apes ni primates wasio na mikia. Primates ni more general. Apes ni more specific than primates.
Ndiyo maana jamaa aliyesema nyani ilibidi aelezwe zaidi kwa sababu nyani Wana mikia na ni primates.
Tume evolve from tailless primates
Not monkeys and'em
 
Kwa Tanzania kuna tabia ya kuamini masomo ya lugha, historia na sanaa zingine ni masomo ya siyo na tija.

Huwezi kujielewa na kubobea kwenye sayansi kama lugha hujaisoma vizuri.

Lugha hukomaza ubongo. Ukizoea kumuita mwanamke demu, basi hata ukikua hutamuheshimu mwanamke, ubongo wako unakuwa corrupted.

Hivyo hivyo kama apes wanaitwa nyani, basi ubongo unakuwa corrupted kuhisi ni nyani mwenye mikia badala ya nyani asiye na mikia.
I.e sokwe mtu.
 
Mkuu unapoteza muda tu. Hapa deal na watoto wanaamini yule nyani anayerukaruka kwenye miti ya jirani kwanini habadiriki akawa mtu! Ahahahahaha!
 
Miaka 200,000 iliyopita tulitoka msituni?

Hiyo miaka 200,000 umeihesabuje?

Mwaka namba 1 ulikuwa lini na mwaka 200,000 ulikuwa lini?
Walipochunguza mabaki ya watu wa kale na kuyapima umri waligundua kuwa mabaki ya kale kabisa yanayofanana na binadamu wa leo ni kutoka miaka 200-300K iliyopita.
 
Mkuu kama ndivyo kwani hizo hatua za mabadiliko hatuzioni???
Evolution inaonekana kwa muda wa miaka michache kwenye microorganism kama bacteria.

Ndiyo sababu dawa za zamani za anti- bacyeria kama tetracycline siku hizi hazifanyi kazi.

Kwa vidudu vidogo kama bacteria evolution ni rahisi kuonekana katika miaka michache. Kwa sisi wakubwa evolution inafanya kazi polepole sana ni vigumu kuona mabadiliko.

Hiki hapa chapisho la kitaalamu kutoka The Lancet linaongelea antibiotic resistance na evolution

 
Mambo ya kishetani TU kwenda kinyume na asili halisi na ukuu wa Mungu....hii Dunia uongo ndo unanguvu.
 
Tulikuwa kundi moja na nyanyi na sokwe ila sisi hatukuwa sokwe wala nyani
 
Miaka 200,000 iliyopita tulitoka msituni?

Hiyo miaka 200,000 umeihesabuje?

Mwaka namba 1 ulikuwa lini na mwaka 200,000 ulikuwa lini?
Miaka inahesibiwa kuanzia siku au miaka hiyo walipofanya huo utafiti/ugunduzi/ dating.
Pia mwaka namba 1 ni insignificant unapoongelea scale ya miaka laki au milioni kadha.
 
Kwa mantiki hiyo Miaka 5000000 hivi mbele wanaume watakua hawana ndevu na nywele na sauti zitakua kama kasuku .
 
Kwa mantiki hiyo Miaka 5000000 hivi mbele wanaume watakua hawana ndevu na nywele na sauti zitakua kama kasuku .
Uwezekano huo ni mkubwa sana hasa ukizingatia wachina tayari hawana ndevu na waafrika baba na binti wate wanapaka mkorogo na manduli yanakwisha.
 
Hahahaaaa

Na wewe lini utakua sokwe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…