Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
Wakuu !
Wasalaam
Meme hio Meme inavosomeka inanifanya nikumbuke mjadala unaoendelea kuhusu Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Mh. John Heche.
Katika sayansi ya siasa kuna dhana inaitwa Political Trust na Human Capital. Kiongozi anapofikia hatua ambayo wananchi wanaendelea kumuamini hata katikati ya tuhuma, ndipo unapojua mtaji wake mkubwa sio fedha bali uaminifu wa umma.
Ndiyo maana badala ya kujibu propaganda kwa propaganda, aliomba mchango wa wananchi.
Matokeo yake ndiyo haya tunayoyaona.
Kutoka lengo la Shilingi milioni 334 ili kuendesha mkutano wa kamati kuu ya Chama, ndani ya muda mfupi mchango umevuka Shilingi milioni 50 kwa taarifa za leo jioni, tarehe 15 July.
Hizi sio habari za fedha pekee yake bali ni data za kisiasa. Inaonyesha kuwa sehemu ya wananchi imeamua kuonyesha imani yao kwa vitendo badala ya maneno.
Kwa hiyo, kama wewe ni mchambuzi wa siasa , swali muhimu sio
"amechangisha kiasi gani?", bali ni:
Ni kwa nini wananchi wako tayari kutoa fedha zao kwa hiari kukichangia Chama kwa ombi alilowaomba Wanachama, Wananchi na Wapenda haki ?
Hapo ndipo kunapokuwa na mjadala wa social capital, political trust na identity politics.
Kwenu Machawa na Walamba makalio ni hivi
Propaganda zinaweza kutengeneza kelele. Lakini katika siasa za kisasa, uaminifu wa wananchi ndiyo mtaji mkubwa kuliko propaganda.
Takwimu hazibishani.
Mtaji wa kisiasa hupimwa na kiwango ambacho wananchi wako tayari kugharamia imani yao.