Kama Paul Makonda angekuwa RC Dar matukio ya ajabu yasingetokea, maana alidhibiti uhalifu. Wauza shisha walipotea kama barafu iliyoyeyuka

Upuuzi mtupu.
 
Sitakishari waliuwa askari sita makonda akiwa mkuu wa mkoa shida ya watanzania wajinga kama wewe mnasahau haraka na mnapoteza kumbukumbu haraka matukio mengi yametokea kipindi cha huyo mjinga mwezio
 

Acha mzaha. Vibaka, wahuni, majambazi ni watu wenye kuipenda dunia. Huwa wanakimbiza roho zao.

Huwezi kuzuia mashambulizi ya kijihadi au kikamikaze kwa blabla za kisiasa. Unatakiwa kuwa na uwezo wa kiintelijensia wa hali ya juu na makomandoo wenye uwezo na dhamiri ya kujitoa mhanga. Sio askari waliozoea kuonea raia.

Jiulize inakuwaje Marekani wanatimka huko Afghanistan au ilikuwaje wakashusha bomu la atomiki huko Japan ili kushinda vita. Vietnam walikimbia. Iraqi wameiacha shaghalabaghala. Kupambana na mtu aliyeamua kufa si kitu ni habari nyingine.

Tuombe Mungu modeli ya Hamza isijitokeze tena. Bila shaka polisi wetu hadi sasa wamepigwa na butwaa kwa kilichotokea. Watanzania wao hawana jeuri hiyo. Wasiwasi ni wasije waka-overreact na kutandika risasi mtu anayewasogelea kuomba msaada au kutoa taarifa. Polisi wa Marekani wanaishi na hofu hiyo kila siku. Hakuna mtemi hapo.
 
Makonda aliamua kustaafu mwenyewe nafasi hiyo na kugombea Ubunge ambao aliukosa, sasa unamlilia nani?
 
Sijakuelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…