Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 12,699
- 22,598
Wale wau ambao kila kitu kizuri kikitokea wanaishia kusema ni kwa sababu Mama Samia anaupiga mwingi, kuna wakati hizo sifa kwa raisi zitawatokea puani na kumuumbua sana raisi wetu.
Juzi hapa thamani ya shilingi dhidi ya dola ilipanda ghafla, toka Shs 2700 kwa dola hadi Shs 2200 kwa dola. Watu wakaishia kumpongeza sana Raisi Samia, kwamba yeye ndio amefanikisha hilo katika utendaji wake, apewe maua yake!
Wenye akili tulikaa kimya, tukijua mabadiliko ya thamani ya fedha yanaweza kuwa na sababu nyingi sana. Leo KLM au Air France wanaweza kusema hawaji tena Zanzibar shilingi ikashuka thamani. Au Trump atashinda uchaguzi USA na dola ikashuka thamani, nk. Geopolitics ni factor kubwa katika mambo ya exchange rates. Kwa kweli nilitarajia Raisi Samia angesema jamani sio mimi, lakini akakusha kupokea sifa na pongezi!
Sasa hivi thamani ya shilingi inaanza kushuka kwa kasi. Hadi sasa imeshuka utoka Shs 2200 hadi 2400 kwa dola.
Sasa nawauliza wale wote mliokuwa mstari wa mbele kumpongeza Raisi Samia thamani ya dola iliposhuka. Raisi Samia amefanya nini kutuharibia thamani ya shilingi yetu? Tunahitaji kumkosoa kwa hilo, sivyo?