Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

Kama Saudi Arabia na Vatican wameweza kufanya ibada majumbani sisi tuliopokea dini toka kwao tunashindwa nini?

Saudi Arabia hawakuanzisha dini yoyote. Saudi Arabia ni nchi iliyoanzishwa juzi juzi tu 1932, na wale wale walioianzisha Israel.

Kama vitu huvijuwi ni heri ukafanya japo utafiti kwa kutumia Google tu kabla hujakurupuka na ku "offend' dini zisizo kuhusu.

Muhammad mtu aliyeanzisha uislamu na kumbuni allah ni mtu wa Saudi Arabia. Hata matambiko yote ya kiislamu yanafanyika Saudia.
 
Muhammad mtu aliyeanzisha uislamu na kumbuni allah ni mtu wa Saudi Arabia. Hata matambiko yote ya kiislamu yanafanyika Saudia.
Mafundiaho hayo umeyatoa wapi? Wewe umesomea wapi Uislam? Tupe ushahidi wako. Isijekuwa umedanganywa au unajidanganya.

Nakushauri waulize Waislam upate uhakika zaidi na uelewe Imani yao. Usikurupuke.
 
Katika ulimwengu wa roho.

Lakini mwilini hata msikiti uliojengwa na Paulo ni ruksa kufanyika ibada!
Kiislam ibada ni popote na misikitini tunaifata jamaa (kujumuika pamoja) na Kwa ajilinya sala za Ijumaa ambazo ni maagizo ya Allah kutoka kwenye Qur'an kuwa inaponadiwa sala siku ya Ijumaa basi twende tukajumuike pamoja. Lakini kama kwenda huko msikitini kutaleta madhara kwako au kwa wengine basi sali hata peke yako nyumbani kwako.
 
Unajua ukishakiri kua yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yako unakua umetangaza vita na shetani, na shetani atajaribu kufanya kila njama za kukuporomosha hapo juu ulipo

Unajua kwamba shetani kapewa mamlaka ya kumjaribu binadamu na katika hili shetani kaamua kutumia huu ugonjwa kama jaribio ili kuwateka watu?

Unajua kukubali kusalia nyumbani kwa kuogopa maambukizi ambayo yamepangwa na shetani ni ishara kwamba shetani amekushinda nguvu na umekosa imani ya kupambana naye?

Unaelewa kwamba namna pekee ya kumshinda huyu shetani ilitakiwa yeyote yule ambaye amemkiri yesu kua bwana na mwokozi wa maisha yake ajitokeze katika wodi za wagonjwa wa corona kwa lengo la kuwafanyia sala ya toba kwa kuwashika vichwani?

Mnakumbuka kua ukiwa na yesu hakuna lishindikanalo maana amewaahidi kutengeneza njia mahala pasipo na njia?
Jombaa acha tamaa ya sadaka. Jombaa huu ulio andika ni usenge. Acha kupoteza watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kwenye Mitandao ninaona kusitisha Shughuli za Ibada tu lakini sijaona Mukizungumzia kufungwa kwa Mabaa?
Au Bia inauwa Virusi vya Corona ndiyomana mikusanyiko ya Baa hamuizungumzii?
 
Hata kupokea, hatukupokea dini yoyote nkutoka Saudi Arabia.

Saudi Arabia imeanza 1932. Dini zote zilizopo Tanzania zipo kwa miaka mingi sana kabla ya Saudi Arabia.a

Sifahamu Ukristo ulipokelewa kutoka wapi lakini Uislam hapa kwetu haukupokelewa kutoka Saudi Arabia.
Umepokelewa kutoka wapi? tupe elimu maana kuishi ni kujifunza.
 
Aaaaaah hapana.... Wewe huwezi kuandika hivi... Nasema tena haiwezekani.... Maana Mataga akili zenu tunazijua... Ni kama za yule aliyesema wagonjwa wa korona wasitangazwe....

Ila MATAGA mna vichwa vizito sana. Ni lini watu wameanza kupiga kelele kwamba ibada zifungwe?

Yaani mpo kama kenge... hasikii mpaka damu zimtoke...
Jana nilimsikia Prof Lipumba akisema yeye ameanza kuswalia nyumbani ili kuepuka misongamano inayoweza kusababisha maambukizi ya Covid 19.

Binafsi nikawa nimemwelewa vilivyo.

Ndipo nikaanza kutafakari, kama Waislamu kule Saudia wanaswalia nyumbani Bakwata wanashindwa nini?

Kama Wakristo kule Vatican, UK na Germany wanasalia majumbani hawa Katoliki, Anglican na KKKT wanafeli wapi?

Kama Walokole huko USA wanasalia majumbani hawa kina Kakobe, Gamanywa, Gwajima, Mwingira wanashindwa nini?

Kuna wakati yatupasa kutumia busara hata kama mamlaka za juu zimewaachia hiyo fursa bado mnatakiwa kutumia hekima ya Mungu kutenda jambo sahihi.
Serikali haiwezi kuwakataza directly lakini nyie mmebarikiwa macho ya rohoni na mwilini na hata hao wagonjwa 88 waliotangazwa hadi sasa ni waumini wenu.

Hekima ya Mungu wa mbinguni na iwe juu yenu!
 
Dini zinawafanya wengi kuwa mbumbumbu.... Fine Mungu yupo... Ila ni baada ya kuwa umechukua tahadhari ndio ukae umuombe Mungu.

Mungu amekupa akili za nini sasa?
Unajua ukishakiri kua yesu ni bwana na mwokozi wa maisha yako unakua umetangaza vita na shetani, na shetani atajaribu kufanya kila njama za kukuporomosha hapo juu ulipo

Unajua kwamba shetani kapewa mamlaka ya kumjaribu binadamu na katika hili shetani kaamua kutumia huu ugonjwa kama jaribio ili kuwateka watu?

Unajua kukubali kusalia nyumbani kwa kuogopa maambukizi ambayo yamepangwa na shetani ni ishara kwamba shetani amekushinda nguvu na umekosa imani ya kupambana naye?

Unaelewa kwamba namna pekee ya kumshinda huyu shetani ilitakiwa yeyote yule ambaye amemkiri yesu kua bwana na mwokozi wa maisha yake ajitokeze katika wodi za wagonjwa wa corona kwa lengo la kuwafanyia sala ya toba kwa kuwashika vichwani?

Mnakumbuka kua ukiwa na yesu hakuna lishindikanalo maana amewaahidi kutengeneza njia mahala pasipo na njia?
 
Ninachokijua tu ni kwamba ukiwa na Imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu / Allah hata ukisalia Sebuleni au Chumbani Kwako au Bustanini Kwako au hata Stoo basi Dua yako inakubaliwa na unabarikiwa vizuri tu. Huko kwenda Makanisani na Misikitini mara nyingine huwa ni Mbwembwe tu zilizochanganyika na Unafiki mwingi ndani yake.

Kama kuna Jambo ninaloilaumu Serikali yetu na sipendezwi nalo hata kidogo ni Kitendo cha Kuruhusu Ibada za Misikitini na Makanisani iendelee. Nina uhakika kama wasipoliangalia hili kwa marefu na mapana yake Waumini wengi wanaojazana huko / humo wataanza Kufa Siku si nyingi. Yaani Serikali inashindwa Kuzuia Ibada huko katika Nyumba za Ibada kwa sasa kwasababu inahofia Kuchukiwa na Kupoteza kama pia si Kuyimwa Kura nao.

Siasa inaharibu utaratibu mzima wa Kiafya hasa mbele ya Janga hili baya na hatari la COVID-19. Asante sana Mdau kwa hili Bandiko lako kwani ni zuri, sahihi na uliyoyaanisha hapa yana ukweli mtupu. Hongera Umenena!

Kanisani wanataka sadaka ili waishi na hawa nao wanataka kura zao ili waweze kuishi " Symbiotic relationship"
 
Saudi Arabia hawakuanzisha dini yoyote. Saudi Arabia ni nchi iliyoanzishwa juzi juzi tu 1932, na wale wale walioianzisha Israel.

Kama vitu huvijuwi ni heri ukafanya japo utafiti kwa kutumia Google tu kabla hujakurupuka na ku "offend' dini zisizo kuhusu.
Acha upotoshaji wewe !!

Aliyekwambia waanzilishi wa Saudia ndio waanzilishi wa Israel nani?

Ibn Al Saud alianzisha ufalme wa Saudia wakati David Ben Gurion alianzisha dola ya Israel huko Mashariki ya Kati mwaka 1948.

Unataka kusema Ibn Al Saud alikuwa myahudi?
 
Ninachokijua tu ni kwamba ukiwa na Imani ya kweli kwa Mwenyezi Mungu / Allah hata ukisalia Sebuleni au Chumbani Kwako au Bustanini Kwako au hata Stoo basi Dua yako inakubaliwa na unabarikiwa vizuri tu. Huko kwenda Makanisani na Misikitini mara nyingine huwa ni Mbwembwe tu zilizochanganyika na Unafiki mwingi ndani yake.

Kama kuna Jambo ninaloilaumu Serikali yetu na sipendezwi nalo hata kidogo ni Kitendo cha Kuruhusu Ibada za Misikitini na Makanisani iendelee. Nina uhakika kama wasipoliangalia hili kwa marefu na mapana yake Waumini wengi wanaojazana huko / humo wataanza Kufa Siku si nyingi. Yaani Serikali inashindwa Kuzuia Ibada huko katika Nyumba za Ibada kwa sasa kwasababu inahofia Kuchukiwa na Kupoteza kama pia si Kuyimwa Kura nao.

Siasa inaharibu utaratibu mzima wa Kiafya hasa mbele ya Janga hili baya na hatari la COVID-19. Asante sana Mdau kwa hili Bandiko lako kwani ni zuri, sahihi na uliyoyaanisha hapa yana ukweli mtupu. Hongera Umenena!

Dini sio hizia au mawazo yako ujue, katika hali isiyo ya dharura katika mafundisho sahihi ya uislam mwanaume anawajibu wa kuswali jamaa msikitini na waumini wenzako, sio kwamba ukiswalia nyumbani hupati thawabu la zinakuwa ndogo na kama umefanya makusudi swala inaadhiniwa msikiti wewe unasali kwenye store yako ya mkaa unapata dhambi unless kuwe na dharura yoyote ile. Katika kipindi kama hichi mafundisho sasa ya Mtume wetu rehma na amani ilipaswa misikiti ifungwe watu wasalie nyumbani kutokana na hali iliyopo hadi hapo itakapokaa sawa. Lakini ni makosa na kama wewe muislam unasema kwenda kuswali jamaa msikitini ni unafiki nasi unapata madhambi na utubie kwa mola wako toba iliyo ya kweli. Inna Allah Ghafur-rRahiim.
 
Saudi Arabia hawakuanzisha dini yoyote. Saudi Arabia ni nchi iliyoanzishwa juzi juzi tu 1932, na wale wale walioianzisha Israel.

Kama vitu huvijuwi ni heri ukafanya japo utafiti kwa kutumia Google tu kabla hujakurupuka na ku "offend' dini zisizo kuhusu.
Huna akili, umeacha msingi wa hoja yake na kurukia kwenye kadosari kadogo pasipo kujua unadhihirisha ujinga wako! Ukiwa CCM halafu ukawa mfia dini unakuwa umefuzu viwango vya juu kabisa vya umaamuma!
 
Nani kakuzuia kufanyia ibada nyumbani kwako? Rais na viongozi wamekwisha kueleza hili la kuzingatia maelekezo ya kujikinga dhidi ya maambukizi na moja wapo ni kuepuka mikisanyiko na kutokusogeleana, umeenda kanisani ukaona msongamano na huwezi kaa mita moja hadi mbili dhidi ya mwenzako UKALAZIMISHWA kuingia kusali? hii kitu inahitaji self awareness, jikinge ikinge na familia yako.
IMG_20200411_163847.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom