Kama Saudi Arabia wanasherehekea Eid Ijumaa inakuwaje BAKWATA wadai mwezi haujaonekana?

Uganda ni majirani zetu na wametangaza Eid ni kesho; lakini pia Uarabuni napo Eid ni kesho.

Kwanini Tanzania wamepanga iwe Jumamosi?
Wewe endelea kula sikukuu sisi wengine kesho lazima tutii viongozi wetu
 
Wakati wa kufanya biashara ya nyama pendwa umewadia hatimaye, baada ya kuwa ngumu kwa takriban mwezi mzima
Basi kumbe waislamu wengi na wingi wao huathiri hiyo biashara?
 
Kwanini nchi zote zinazotuzunguka hadi Saudi Arabia leo ni sikukuu lakin Tanzania hapana
Tuna majira tofauti, mwezi ni huuhuu mmoja, wanaweza kuuona sisi tusiuone.
Ni elimu ya aina yake kama huijiu utabakia kusema unavyosema.
Ndio maana kuna mahali saa moja giza na pengine saa moja hiyohiyo bado mwanga mkubwa...
 
Kweli ndugu sio masihara. Mimi ni mdogo wako sana. Allah akuongezee Ilmu zaidi na zaidi na akubariki nayo. Akufanyie wepesi mambo yako na akupe kheri duniani na akhera. Amin.
Allahul mustaan, allah atuzidishie sote na atufanyie wepesi sote, aaamyn.
 
Kuna madhehebu mawili kwenye Uislam na miaka yote huwa na tarehe tofauti za kufungua .. Answar Suna always ndio huwahi na hii ni miaka yote
Answar sunnah si dhehebu wala pote bali ni taasisi ya kiislamu kama IPC, ISC, IF n.k yenyewe huitwa answaar muslim youth center au AMYC makao makuu yake ni tanga, tanzania.

Wanaowahi kufungua ni watu wenye msimamo wa mwezi wa kimataifa na wanaochelewa ni watu wa mwezi wa kitaifa ikiwa hawakuuona kwao, na wote wako sahihi hapana vibaya.
 
Tuna majira tofauti, mwezi ni huuhuu mmoja, wanaweza kuuona sisi tusiuone.
Ni elimu ya aina yake kama huijiu utabakia kusema unavyosema.
Ndio maana kuna mahali saa moja giza na pengine saa moja hiyohiyo bado mwanga mkubwa...
Dini ni moja na dunia ni moja. Toa porojo zako huko, peleka kwenye vilabu vya pombe za kienyeji huko kijijini kwenu
 
Kufunga wafunge waislam ila muandamo wa mwezi wanaulizia wasio waislam.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…