Kama Saudi Arabia wanasherehekea Eid Ijumaa inakuwaje BAKWATA wadai mwezi haujaonekana?

Kama Saudi Arabia wanasherehekea Eid Ijumaa inakuwaje BAKWATA wadai mwezi haujaonekana?

Uganda ni majirani zetu na wametangaza Eid ni kesho; lakini pia Uarabuni napo Eid ni kesho.

Kwanini Tanzania wamepanga iwe Jumamosi?
Kwani Kimsboy anasherekea lini? Au kakimbilia Iran na Urusi kwa Washia wenzake???
 
Kuna miezi mingapi? Dunia ina mwezi mmoja, sasa kwavipi uonekane Uganda hapa usionekane?
... kama umeuona Tanzania toa ushuhuda. Suala ni uonekane mahali husika na sio kuonekana kwingine.
 
Kabla ya kuzungumzia mwezi kuandama, inapaswa mtu kuwa na ufahamu mdogo tu.
Kifupi alhamisi mwezi usingeweza kuonekakana Africa mashariki...ulizama mda mchache tu baada ya jua. Haukuwa mwezi mwandamo, ila kuna maeneo ya mashariki ya kati wangeweza kupata mwezi mwandamo dakika chache tu baada ya jua kizama.
Mwezi ni mmoja ila kinajimu kuna eneo linaweza kuuona na eneo wasiuone.
 
Uganda ni majirani zetu na wametangaza Eid ni kesho; lakini pia Uarabuni napo Eid ni kesho.

Kwanini Tanzania wamepanga iwe Jumamosi?
Kuna madhehebu mawili kwenye Uislam na miaka yote huwa na tarehe tofauti za kufungua .. Answar Suna always ndio huwahi na hii ni miaka yote
 
Wakati wa kufanya biashara ya nyama pendwa umewadia hatimaye, baada ya kuwa ngumu kwa takriban mwezi mzima
 
Uganda ni majirani zetu na wametangaza Eid ni kesho; lakini pia Uarabuni napo Eid ni kesho.

Kwanini Tanzania wamepanga iwe Jumamosi?
Tanzania kila kitu siasa tu.Watu wanalazimishwa sio ijumaa ni Jumamosi.
 
Uganda ni majirani zetu na wametangaza Eid ni kesho; lakini pia Uarabuni napo Eid ni kesho.

Kwanini Tanzania wamepanga iwe Jumamosi?
Bakwata hawapo serious na kuuona., maana leo Ijumaa Uganda, Kenya, Rwanda ni sikukuuu lakin Tz hawajauona, na leo utaonekana waziwazi
 
Kuna Eid ya 2019 watu walichanganyana hivyo hivyo.... Basi me nilikuwa sehemu moja hivi dukani nikasikia Shekh asema '' Yan waislam wazima tunazidiwa akili na wakristu, wewe ushawahi ona Pasaka mbili au Christmas mbili"

Tatizo kufunga wanaanza pamoja issue kufungua sasa ndy mtiti....
Elewa kwanza maana ya Eid al-Fitr, Pasaka na xmas ndo uje ukoment
 
IDI.
MAULIDI.
KRISMAS.
PASAKA.
MWAKA MPYA.

ZOTE HIZI NI SIKUKUU ZA KI SHETANI, KIPAGANI, MNYAMA, MPINGA KRISTU.
 
Kwa hiyo siku mwezi ukiamua kujificha tutafunga mwaka mzima?
 
Hakuna njia ya mkato, watu wa mnyaaz itawapasa nao wamalizie vyungu vyao 30. Huko kwingine kote wao ni Suni, na msimamo wao taarifa za mwezi kuandama hupatikana sehemu yoyote ile duniani, kuuona kwa macho ya kibinadamu siyo kizingiti.

Hapa Bongo, BAKWATA ni zao la Shia. Ni lazima auone ama kupata taarifa za muandamo wa mwezi hapa nchini. Hapa ni sawa na kutaka kuwaeka pamoja Wakatoliki na Wasabato.
Bila shaka hoja yako inatosha kabisa kuhitimisha uzi huu.Saafi kaaabisa.
 
Back
Top Bottom