Kama Saudi Arabia wanasherehekea Eid Ijumaa inakuwaje BAKWATA wadai mwezi haujaonekana?

Kama Saudi Arabia wanasherehekea Eid Ijumaa inakuwaje BAKWATA wadai mwezi haujaonekana?

Nimesoma humu vema itoshe kusema Bakwata licha ya matatizo yao mengine kwenye hili huwa wapo sahihi. Wale Answar ni watukutu wanapaswa kudhibitiwa.
 
Nakazia wekeza kwenye imani yako,acha kupoteza muda kukosoa kwenye imani isiyokuhusu inaonyesha ni kiasi gani ulivyo dhaifu wa kiimani...."Pilipili usioila inakuwashia nini"
Wewe huo Uislam wenyewe huujui
 
Waliosoma dini na kujua ukweli hawewez kuendeshwa na bakwata taratibu waelewa wanaanza kuamka itafika kipindi watajikuta na wao wamerudi kundini allah awasamehe Kwa tamaa zao za kudanganya umma
samia anasemaje?
 
Nimesoma humu vema itoshe kusema Bakwata licha ya matatizo yao mengine kwenye hili huwa wapo sahihi. Wale Answar ni watukutu wanapaswa kudhibitiwa.
Mkuu hakuna mwenye matatizo humu hili suala lina uhuru tu kila mtu afanye kile anachokitaka, atakayefungua kwa mwezi wa kimataifa ni sawa hapana vibaya, na atakayefungua kwa mwezi wa kitaifa ni sawa pia hapana vibaya, wala hakuna haja ya kudhibitiana wala hakuna mamlaka ya kufanya hivyo.
 
Kwasababu mara nyingine machweo na mawio hutofautiana, ni kama kigoma na dar es salaam, watu hapo jijini wanafuturu saa 12 na dakika 24 kigoma wanafturu saa 1 kasoro au saa moja kamili na saa hazitofautiani.
Lakini mwezi ukiandama Saudi Arabia ni sawa na Tanzania point iko hapo, Pili kama ni Uislamu Saudi Arabia ndio Nyumbani kwa uislamu.

Sasa inakuwaje waliokea tu dini waenfe kinyume na wenye dini yao?
 
Hata kufuturu wapo wanao wai na wanao chelewa. Hili swala linaeleweka hata kisayansi, mwezi hauwezi kuonekana dunia nzima kwa wakati mmoja na kisheria ni kufata muandamo wa mwezi. Sidhani kama mwezi unaweza kuonekana halafu Bakwata wakaamua kutokutangaza
 
BAKWATA INA WANAZUONI NGULI KABISA TUSIIDHARAU, ELIMU YETU NI SAWIA

Mwezi March, 1844 Sir George Arthur gavana wa Bombay alidai apewe haraka ripoti muhimu ya Mwaka 1815 ya wazungu 'wavumbuzi /mabaharia wa merikebu kuhusu waliyoona walipofika Afrika Mashariki / Zanzibar na kukuta uelewa wa sayansi / jiografia ya wenyeji wa makabila yote waliokuwa wanaishi kisiwa hiki.

Maana wageni waligundua watu wa makabila tofauti tofauti Komoro, Waarabu, Baniani, Baluchi, Wazegura, Wasegejo, Wadigo n.k wa Zanzibar walikuwa na namna ya kuhesabu siku za mwaka mzima ambao kwao ni siku 354 kisha kuongeza 10 au 12 ulingane kuwa 364 au 366 kama ulivyo kalenda ....

Hivyo waswahili na makabila Afrika Mashariki wana ufahamu mkubwa jinsi misimu, urefu wa siku, miezi , mwaka huendana na jinsi dunia inavyoegama au kuikabili jua kimuegamo ndo maana kuna siku ndefu na fupi pia siku moja iliyotimia kwa usawa (equinox) yaani saa 12 za kiza na 12 za mwanga ktk saa 24 ya siku.

Hali zote hizo za 'vitimbi (manifestation ) au tuite tabia vya mgeuko wa sayari yetu dunia zinachukuliwa kwa umuhimu mkubwa ili kutambua misimu, pepo za kaskazi / kusi , mvua kubwa, mvua ndogo, kuangalia nyota agani ya Kilímia yaani kulima kwa kiswahili cha leo n.k Hakika Hii ni elimu kubwa tuliyonayo wenyeji tofauti na kalenda ya kutundika ukutani ...


The Wasawahili also calculate their agricultural seasons from the stars called Kilímia, a name probably derived from Ku lima, to plough....

Local tribes and semi-civilized tribes, begins with sighting the moon; and the Wasawahili reckon like the Jews, the modern Moslems, and the Chinese, 12 of 29 and 30 days alternately. ‘The complete number of months with God’ being, says the Koran, ‘twelve months,’ good followers of the Prophet ignore the Ve-adar, second or embolical Adar, which the Hebrews inserted after every third year, and retain their silly cycle of 354 days. The Wasawahili add 10 to 12 days to the Moslem year, and thus preserve the orderly recurrence of the seasons. The sage in 172charge of the local almanac is said to live at Tumbatu: he finds his New Year’s Day by looking at the sun, by tracing figures upon the ground, and by comparing the results with Arabic calendars.....

‘The universal festivals,’ says the late Professor H. H. Wilson (Essays on the Religion of the Hindus, ii. 155), ‘are manifestly astronomical, and are intended to commemorate the revolutions of the planets, the alternations of the seasons, and the recurrence of cyclical intervals of longer or shorter duration.’ The Nau-roz (نوروز) or New Year’s Day, here, as in Syria, locally pronounced Nay-roz, was established in ancient Ariana, according to Persian tradition, by Jamshid, King of Kings, in order to fix the vernal equinox.[45] It is the Holi of the Hindus, 173and after the East has kept this most venerable festival for 3000 years, we still unconsciously celebrate the death and resurrection of the eternal sun-god.....

Source :
Zanzibar: City, Island, and Coast by Richard F Burton
 
Lakini mwezi ukiandama Saudi Arabia ni sawa na Tanzania point iko hapo, Pili kama ni Uislamu Saudi Arabia ndio Nyumbani kwa uislamu.

Sasa inakuwaje waliokea tu dini waenfe kinyume na wenye dini yao?
Ndio mwezi ni mmoja dunia nzima, ila nilikufahamisha mwanzo wa uzi kuwa kuna misimamo ya aina mbili, msimamo wa mwezi wa kimataifa na mwezi wa kitaifa na nikakupatia hukmu ya misimamo yote miwili sijui ulijaribu kuelewa?.

Pili saudi arabia sio wamiliki wa uislamu mtume swala na salaam ziwe juu yake hakuja kwa ajili ya wasuudi bali kwaajili ya watu wote, hivyo si sawa kufananisha mambo ya ikhtilafu za mwezi na uislamu.

"Sema! enyi watu, hakika mimi ni mjumbe wa allah kwenu nyote, {allah} ambaye ni wake yeye ufalme wa mbinguni na ardhini, hapana mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa yeye, anahuisha na anafisha, basi muaminini allah na mtume wake nabii asiyejua kusoma wala kuandika, nabii ambaye anamuamini allah na anayaamini maneno yake, na mfuateni ili mpate kuongoka".

Qur'an 7:158

Hivyo si sawa kuumilikisha uislamu saudi arabia, bali ardhi haimtakasi mtu na haimaanishi wakazi wa saudi arabia ndio waislamu kisha sisi ni wafuata mkumbo, ufahamu mbaya ulioje.
 
mbona taarifa za mwezi kuandama huko zilitoka kitambo tu.....unajifanya umeleta kitu kipya?
Wao wana mitambo kama aliyoomba mufti...
Screenshot_20230420-195627.jpg
 
Hii dini ni ya kimchongo mchongo. Inawezekana vipi nchi Moja kukawepo tarehe mbili tofauti? Leo Kuna watu kalenda inadoma tarehe Moja wengine tarehe mbili. Hii ni ya kienyeji kabisa hii dini
 
Hii dini ni ya kimchongo mchongo. Inawezekana vipi nchi Moja kukawepo tarehe mbili tofauti? Leo Kuna watu kalenda inadoma tarehe Moja wengine tarehe mbili. Hii ni ya kienyeji kabisa hii dini
Mkuu sisi ndio waislamu na tumekubali hizo tofauti za tarehe wewe unaumia nini?.
 
Back
Top Bottom