Kama sauti hii ni sauti ya kweli, nimeelezwa Mpango ndio mpango mzima. Swali ni akiwa Mkristo, kwanini ni lazima awe Mkatoliki?


Hakuna dini katika Upngozi wa urais nchini kwetu. Tulishazika dini, makabila na hata rangi! Tunachoangalia ni sifa za mtu! Sasa kama hajajitokeza mtu wa dini nyingine, rangi nyingine na hata kabila jingine mwenye sifa ndiyo kusema hatutakuwa na rais au rais atakuwa mwislamu labda? Hata hivyo, waislamu nao wana madhehebu yao. Labda ungetuambia hata inapokuwa rais ni mwislamu labda huwa anakuwa Shia, maana nchi hii imeshakuwa na rais 3 wakristo na 3 waislamu. Sisi tunachotaka ni rais anayekidhi vigezo vya urais! Hata akiwa Muislamu mpaka mwisho wa dunia au mpagani mpaka mwisho wa dunia au mkatoliki au mluteri au muanglikana mpaka mwisho wa dunia, tutamchagua tu mradi awe na sifa za kuwa kiongozi wa nchi ( Head of State). Hatutaki kurudi kwenye dini za watu au makabila ya watu au rangi za watu!
 
Hiyo ndio formula iliyopangwa na walimu na haiwezekani kubadilishwa labda walimu waje wengine, lakini kaa kimya sababu soon mwalimu anarudi darasani
 
Mambo yakaanza kwenda kombo baada ya uzi huu
 
Ndio maana wanataka kumpoteza?
 
Mimi nafikiri marais wakristo wote waliyoongoza kua wakatoliki sio ajabu. Ukweli nchi hii ni kwamba wakristo ambao ni nusu ya raia wakatoliki ndio wengi kwa asilimia huenda zaidi ya nusu ya wakristo wote.
 
Wako wengi siyo Biteko tu. Na huyo niliyekutajia pia yupo. Alipopata uteuzi mbona ndugu zake upande wa 2 walifanya sherehe!!
Kwani Kikwete hakujua kuwa huyu si Mtanzania hadi wakampa cheo akampeleka kwenye maswala ya uchumi na baadaye Waziri wa fedha?
Vipi Bashe ni Mtanzania?
Vipi Kinana ni Mtanzania?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…