Maulaga59
JF-Expert Member
- Feb 1, 2021
- 2,984
- 2,971
Wanabodi
Kwa kawaida siku za Ijumaa na Jumamosi ndio huwa nakaa viti virefu, Jumapili ni family day, huwa sikai viti virefu nakaa viti vya chini na mwendo sio wa Joni Mtembezi ni mwendo wa Harusi ya Kana!.
Jumapili ya leo, niko zangu viti vya chini, usawa wa Harusi ya Kana, tena ile ya Altareni, amekuja mtu, sina uhakika kama ni wa 'kulee!', akanitamkia "Mpango ndio mpango mzima"!.
Hivyo kama HII sauti ni sauti ya kweli , then Mpango ndio mpango mzima!. Swali ni.. kwanini akiwa Mkristo, ni lazima awe Mkatoliki?!.
Ufafanuzi zaidi ni Juliasi alikuwa Mkatoliki, Benyamini alikuwa Mkatoliki, na Yohana Yosefu pia alikuwa Mkatoliki!, jee imejitokea tuu by chance of a mere coincidence au akiwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki?.
Kama sauti HII ni kweli, then anayefuata sio Dr. Huseni!, ni Fillipo!. Kwa vile huyu pia ni Mkatoliki, hivyo nauliza tena na tena, kwani akiwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki?, why?.
Jumapili Njema
Paskali.
Hakuna dini katika Upngozi wa urais nchini kwetu. Tulishazika dini, makabila na hata rangi! Tunachoangalia ni sifa za mtu! Sasa kama hajajitokeza mtu wa dini nyingine, rangi nyingine na hata kabila jingine mwenye sifa ndiyo kusema hatutakuwa na rais au rais atakuwa mwislamu labda? Hata hivyo, waislamu nao wana madhehebu yao. Labda ungetuambia hata inapokuwa rais ni mwislamu labda huwa anakuwa Shia, maana nchi hii imeshakuwa na rais 3 wakristo na 3 waislamu. Sisi tunachotaka ni rais anayekidhi vigezo vya urais! Hata akiwa Muislamu mpaka mwisho wa dunia au mpagani mpaka mwisho wa dunia au mkatoliki au mluteri au muanglikana mpaka mwisho wa dunia, tutamchagua tu mradi awe na sifa za kuwa kiongozi wa nchi ( Head of State). Hatutaki kurudi kwenye dini za watu au makabila ya watu au rangi za watu!