Kama serikali imeshindwa kuendesha mfumo wa ESS , bora waufute au kuwe na mbadala in case mfumo unafeli

Kumbe unataka kukopa mwalimu ndomana hasira nyingi nyingi
 
Kumbe ni siku ya pili tu? Mbona taarifa nyingine zinasema kuwa kuwa watumishi wa kada ya ualimu (au wanaotumia kalenda ya mwaka) toka mwezi wa kumi na mbili hawajawahi kutumia huo mfumo?

Pia watumishi wa idara ya ardhi nao wanadai karibu mwezi unakaribia kuisha mfumo unaowawezesha kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kuandaa hatimiliki haupo hewani? Kwamba kwa kipindi chote hiki wanaenda ofisi kufanya shughuli ambazo hazihitaji mfumo

Serikali inataka kwenda kidigitali lakini inaweka wajanja wajanja wasiokuwa na weledi kusimamia mifumo ndiomaana wanafeli
 
Kuna haja ya kufanya uchunguzi kuhusu uendeshaji wa huu mfumo kama kweli kuna dhamira ya dhati ya kutaka kujua tatizo ni nini hasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…