Kama Serikali ya Tanzania haina dini, Mungu anayetajwa katika wimbo wa taifa ni yupi?

Kwahiyo SAMIA SULUHU NA MAJALIWA ni wakristu.,, nyie watu sijui mnataka nini...yn shida yenu mchaguliwe ht km hamna sifa....udin wenu peleken Afghanistan huko. ..
kwanini na nyie udini wenu msiupeleke vatican
 
Hivi unazungumizia viongoz Wa kiislam au wenye majna ya kiislam. Maana hao wenye majna ya kiislam mbona hata awamu ilyopita walikuwepo na hawakufanya chochote wakiongozwa na yule jamaa wa bagamoyo. Je vp huyu anaye ng'ang'ania madaraka Zanzibar kwan n mkristo? Sasa kuna haja gan kuwa na viongoz mnaotaka wawe waislam lkn matendo yao hayaendani na huo uislam?
 
 
Hukuzoea kwa sababu hamjaguswa na udini toka uhuru wa nchii hili tatizo lipo ni uvumilivu tu wa waislam ndio umetufikisha hapa
Kwani dini ni wakristo na waislamu tu? Je, na wale wanaoabudu miungu mingine nao waanze kuhoji juu ya teuzi za mh raisi? Hizo dini zenu kaeni nazo huko, sisi tunachotaka ni huduma bora za kijamii kwa wananchi basi.
Siku zote mimi naamini kuwa watu wenye udinidini uwezo wao wa kufikiri ni mdogo.
 
PUMBAVU NCHI IKO HOI WEWE UNAONGEA PUMBA ZA DINI TOKA NENDA ZAKO HUJUI KITU WEWE KAA KIMYA.
 
Waislam awamu hii ni awamu ya mtihani mkubwa sana, tujue tu uislam tangu siku ya mwanzo ni dini yenye kupigwa vita, kama mtume saw alivyosema itafika wakati uislam utakuwa kama kaa la moto ni either uivumilie imani kwa subra ukitaraja malipo yako jannah au uitupe imani uwaridhishe waliokufuru, chaguo ni lako!so anachofanya magufuli ni muendelezo ule ule, tukumbuke tumeletwa duniani ili tufanyiwe majaribu, mitihani! Naombeni tuyakumbuke haya
 
Hatuwezi kukubali dini au udini kufungamana na matakwa ya serikali na ningeiomba serikali iitazame sheria juu ya watu wanao anzisha chokochoko za udiniudini, iwe ni mkiristo, muislamu au mpagani wote wachukuliwe hatua za kisheria kwani malengo yao si mazuri juu ya hatima ya hii nchi, wanalenga kutugawa na kupandikiza chuki ktk jamii.
 
Hizo takwimu za kusema waisilamu nchi hii wapo zaidi ya 65% ndizo zinazowadanganya. Mwaka 2012, shirika la habari la taifa lilifichua siri ya muda mrefu na kutangaza kuwa Tanzania kuna waisilamu 32%, wakristu 52%, wasio na dini 14% na dini nyingine asilimia iliyobaki. Kuhusu kuumia, hapo hakuna namna kwani tulimpenda wenyewe, tukamchagua wenyewe, tukawapuuzia wengine. JPM endelea kuteua tu bila kuzingatia dini ya mtu, hata BAKWATA wateulie mgalatia
 
Ingekuwa hao waislam unaowazungumizia n wale wanoendana na matendo ya mtume Muhammad (s.w) ningekuunga mkono lkn hawa wala rushwa, mafisad, wezi, wenye uchu wa madaraka, ambao wapo tayar wengne wafe ,wapate vlema kwa ajl ya mafanikio yao. Mm cion umuhmu kabsa wape watu madaraka kwa sababa wanamajna ya kislam alafu matendo yao ya ovyo. Huko itakuwa n kuuzalilisha uislam
 

Wale wapumbavu wenzenu wanaouwana Iraq, Syria, Yemeni, Libya, Misri mpaka mnamhukumu mtoto wa miaka minne eti kifungo cha maisha jela!! na kwingineko huko nako yuko Magufuli au kuna wakristo? ukipata jibu ndiyo utajua hata hapa humuonewi nchi aliachiwa mtu wenu angalia alivyoiharibu kwa ujinga huohuo unaotaka kuuleta hapa tambua genge ulilomo siku zote halilidhiki na kila mahali mnalalamika tu tumeshawazoea na uongozi hamuuwezi kote duniani siyo hapa Tanzania tu.
 
Kwan lengo la serikali ni kutufundisha quran au biblia? Quran kuna misikiti biblia kuna makanisa period.
Serikali ni kututumikia wananchi.
Sasa dini ya nn??
 
Halafu hawa watu siijui wapoje,kila utawala unapobadirika wanaanzisha hoja za kijinga kama hii safari hii hatudanganyiki tunasonga mbele kujenga Taifa la Tanzania sio la Kikristo/wala Islam
Mkuu tatizo ni uwezo wa kufikiri au ni kujitoa ufahamu? Hivi hilo taifa litajengwa vipi kama kuna sehemu ya jamii inahisi imetengwa hata kama wewe unaona sio kweli? Kutakuwa na maendeleo kweli kama 50% wanafanya kazi na wengine 50% wananung'unika? Hata kule Sudan kabla Sudani ya kusini hawajajitenga walikuwa wanatoa hoja kama hizi kuwa kazi zinatolewa kuangalia weledi na ujuzi, ni wapi wamefika? Unataka na sisi tufike huko.

La msingi kama kuna kundi linalalamika inabidi ifike mahali kuwe na mjadala wenye tija. Kukejeli hakusaidii sana hata kama unaona si kweli kwa sababu anayeona anaonewa bado ataendelea kuona hivyo na kwa sababu anaishi na kupumua unakuwa unatengeneza bomu ambalo baadaye litakuathiri hata wewe unayetoa hizo kejeli.
 
Mbona hausemi waziri mkuu na makaumu wa rais ni waislam?ambao ndio washauri wakuu wa rais katika kuteua nafasi mbali mbali?
Katiba haimlazimishi raisi kufuata ushauri wa mtu yeyote.
 
Eti 65% ya Watanzania wamesoma Madrasa? Yaani Waislamu? Usintanie mleta mada, Waislamu Tanzania ni 30% Wakristo ni 62% walobaki wengine wakiwemo Hindu, Buda na Pagan, hupendi tafuta ndimu.
 
Pamoja na sheria, taratibu na kanuni za serikali watu wengi duniani hufanya kazi kulingana na utamaduni na mazingira waliyolelewa na ndiyo maana ukienda Marekani kule maofisini unakuta watu wanafanya tafrija zinazoendana na utamaduni wao kama "halloween". Vivyo hivyo japokuwa watu wanapaswa kufanya kazi kulingana na sheria, taratibu na kanuni kwa Tanzania ila hawako hivyo kwa sababu ni binadamu na binadamu huishi kulingana na alivyolelewa na kukuzwa. Unapokuwa na jamii yenye makundi mbalimbali na ikatokea una kundi moja tu linaendesha serikali ni rahisi sana kwa mahitaji ya watu wa makundi mengine kusahaulika. Na ndiyo maana kuna kelele za kuongeza uwiano wa wanawake katika nafasi za uongozi kwa sababu hiyohiyo kuwa kunapokuwa na wanaume wengi kila mahali ni rahisi kwa mahitaji ya wanawake kusahaulika.
 
Eti 65% ya Watanzania wamesoma Madrasa? Yaani Waislamu? Usintanie mleta mada, Waislamu Tanzania ni 30% Wakristo ni 62% walobaki wengine wakiwemo Hindu, Buda na Pagan, hupendi tafuta ndimu.
Asante kwa kump nondo na data..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…