Hii hoja yako ingekuwa na nguvu kama tungekuwa tunaona randomness katika diversity za watu pindi selection zinapofanyika, kwa mfano iwapo kuna teuzi Waislamu wakawa wengi, kesho katika teuzi nyingine wakawa wachache au wasiwepo kabisa, Hii ingeonekana kuwa hakuna Bias, Lakini teuzi zote wanakuwa Minority tu, Hii inazua maswali mengi sana.
Lakini pia hoja yako ingekuwa na nguvu kama watu hawajawahi kuhoji selection hizi kwa jicho la kidini, kwa mfano NSSF watu wamelia udini weeeeh eti kwa sababu na waislamu nao walianza kupewa nafasi, Au Chukulia kwa mfano Mwenyekiti mstaafu mzee Mtei alipolia na JK kwamba kateua waislamu wengi kwenye bunge la Katiba, Au kelele za watu humu JF kuwa Kikwete mdini kwa kumteua Profesa Assad!. Haya yakitokea hamuwatetei hawa watu, na nyinyi mnaungs mkono hoja au mnakaa kimya, Lakini teuzi zinapokuwa hazina waislamu wengi mnasema eti " Uzalendo, Elimu, weledi na Uchapakazi ndiyo vilivyozingatiwa na si dini ya mtu". Huu ni unafiki.