Kama Serikali ya Tanzania haina dini, Mungu anayetajwa katika wimbo wa taifa ni yupi?

Kama Serikali ya Tanzania haina dini, Mungu anayetajwa katika wimbo wa taifa ni yupi?

Nendeni shule jengeni shule na vyuo msilalamike tu mnafundisha.madrasa tu.mnategemea m compete na wanaojenga shule na vyuo???
Kwani nyie mmejenga au wazungu ndiyo waliowajengea ili wawatendee watoto vibaya?na sasa wanawalazimisha muoane jinsia moja
 
Usipende kubisha kila kitu,JF hatujajiunga leo tumeshuhudia mengi humu.Ukiondoa hayo tumeshuhudia mengi mpaka baadhi ya viongozi wa nchi wenye imani za kiislamu kuzushiwa mambo ya ajabu kama kuuza tausi wa ikulu n.k

Hatuko hapa kumchafua wala kumsingizia mtu jambo.

Kwa ushahidi kabisa alipoteuliwa Jaji Othman Chande wakristo wenzako hapa walikaukiwa mate.Wengine walifika mbali mpaka wakasema ni ushawishi wa Othman Rashid.Sisi hapa tumeshusha data sio mambo ya kuhisi.Jahazi hili linaelemea upande mmoja.Hili jambo halileti picha nzuri ukizingatia shule na vyuo walivyoenda hao wateule hata sisi tumeenda.
Mkuu, weka link tu ya hayo, jamaa yako kasema hayo malalamiko ya wakristo yapo humu, si ulete tu huo uzi? Ubishi wa nini?
 
Kwani nyie mmejenga au wazungu ndiyo waliowajengea ili wawatendee watoto vibaya?na sasa wanawalazimisha muoane jinsia moja

Mbona nyie waarabu hawajawajengea??zaidi ya mafundisho ya kujitoa muhanga
 
Si ulifungua uzi wewe juzi wanalia lia kuwa wafanyakazi wa RITA wameonewa.

Mkuu uzi ulihusu NIDA si RITA hata hivyo mimi sina deal lolote na hizi taasisi zaidi ya kuleta taarifa tu
 
Hii mbegu ya udini isiachwe ikastawi katika nchi hii,kamwe watu wasipewe madaraka kwa mitazamo ya dini na madhehebu yao.UWEZO WA KUMUDU KAZI TU.
 
Kwa hiyo haina dini halafu wakuu wa mikoa wanakuwa waislamu sita na wakristo zaidi ya ishirini. Sasa hao wakristo wamepataje uteuzi kama serikali haina dini na nafasi hazikutangazwa popote!!!

Huu udini wa Magufuli utaligawa taifa na kuvuruga umoja wa kitaifa. Toka ameanza kufanya teuzi jicho lake limeona asilimia 85 wakristo na asilimia 15 waislam. Sasa hawa wakristo wakianza kutumia vibaya madaraka na kuweka wakristo wenzao kama ilivyo Tanesco tutafika? Mimi ni mkristo ila sipendi hiyo hali
Kwani hao 20 ni wazaire ama watanzania? Halafu unaposema Magufuli mdini una maana gani Magufuli ni muumini wa ukristo ktk dhehebu la wakatoliki wa roma na hapo sina hakika kama hao wote 20 ni wa wakatoliki wa roma
 
Hii hoja yako ingekuwa na nguvu kama tungekuwa tunaona randomness katika diversity za watu pindi selection zinapofanyika, kwa mfano iwapo kuna teuzi Waislamu wakawa wengi, kesho katika teuzi nyingine wakawa wachache au wasiwepo kabisa, Hii ingeonekana kuwa hakuna Bias, Lakini teuzi zote wanakuwa Minority tu, Hii inazua maswali mengi sana.
Lakini pia hoja yako ingekuwa na nguvu kama watu hawajawahi kuhoji selection hizi kwa jicho la kidini, kwa mfano NSSF watu wamelia udini weeeeh eti kwa sababu na waislamu nao walianza kupewa nafasi, Au Chukulia kwa mfano Mwenyekiti mstaafu mzee Mtei alipolia na JK kwamba kateua waislamu wengi kwenye bunge la Katiba, Au kelele za watu humu JF kuwa Kikwete mdini kwa kumteua Profesa Assad!. Haya yakitokea hamuwatetei hawa watu, na nyinyi mnaungs mkono hoja au mnakaa kimya, Lakini teuzi zinapokuwa hazina waislamu wengi mnasema eti " Uzalendo, Elimu, weledi na Uchapakazi ndiyo vilivyozingatiwa na si dini ya mtu". Huu ni unafiki.
Mkuu kama una maana mjinga moja akikosea inabidi na wewe umfuate? Nadhani huyo mtei alikosolewa vile vile kama tunavyofanya hapa. Ukipeleka maombi ya kazi na cv huandiki kama wewe ni mtaalam wa sala tano ama ni mjumbe wa baraza la walei wa kanisa bali elimu yako na ujuzi wako. Shaurini vijana kujikita katika shule msipende kuwadhurutidha wakasome dini bila kuwakazania na elimu dunia.
 
W
dini mnzoongelea mmezikopi za kwenu mmeziacha....
Kweli kabisa ISIS inawaomba watu kama mtoa mada waende levante kwenye nchi mpya huna haja visa wala nini visa kuwa muislam wa madhehebu ya suni.
 
Kwani dini ni wakristo na waislamu tu? Je, na wale wanaoabudu miungu mingine nao waanze kuhoji juu ya teuzi za mh raisi? Hizo dini zenu kaeni nazo huko, sisi tunachotaka ni huduma bora za kijamii kwa wananchi basi.
Siku zote mimi naamini kuwa watu wenye udinidini uwezo wao wa kufikiri ni mdogo.

Hao wanaoabudu miungu Mapagani sijui Marastafar. Hao hawakushiriki, wala kutoa mchango wowote katika kupigania uhuru wa taifa hili. Waislamu wanahaki ya kulalamika... Waislamu kwa asilimia kubwa ndio waliopigania uhuru wa taifa hili, tulitoa mali zetu na kila kitu tukawaweka hawa Wagalatia halafu leo wanajidai wanatubagua hii si sawa, dhulma hii ina mwisho wake!
 
Hao wanaoabudu miungu Mapagani sijui Marastafar. Hao hawakushiriki, wala kutoa mchango wowote katika kupigania uhuru wa taifa hili. Waislamu wanahaki ya kulalamika... Waislamu kwa asilimia kubwa ndio waliopigania uhuru wa taifa hili, tulitoa mali zao na kila kitu tukawaweka hawa Wagalatia halafu leo wanajidai wanatubagua hii si sawa, dhulma hii ina mwisho wake!
Kwani kazi ya serikali ni kujenga makanisa au misikiti? Je kazi ya serikali ni kufadhili kuenea kwa injili au uisilamu? Kama si hivyo unawezaje teteaje point yako kwa kutumia logic umuhumu wa swala la udini katika teuzi mbalimbali? Hebu nikuulize: kwa mfano kama waziri wa afya ni mkristo, je, ukristo wake utakuwa na mchango gani katika huduma za afya? Jibu ni hapana. Kwa kifupi ni kwamba, kuzingatia kigezo cha udini kwenye teuzi ni nonsense! Watu watateuliwa kwa uwezo wao wa kufikiri na kufanya kazi.
 
Kama hoja ni ya watu kuteuliwa kwa uwezo wao wa kufikiri na kufanya kazi. Miaka nenda miaka rudi wanaopata kuteuliwa kwa asilimia kubwa ni wale wale wavaa misalaba. Inamaana kwamba hawa ndio wenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kufanya kazi?
 
Yaani mimi nakushangaa wewe kukomaa na hii issue ambayo haitusaidii kama taifa? Nimeuliza kazi ya serikali ni kujenga makanisa au misikiti? Je, ni kufadhili kuenea kwa injili au uisilamu? Au unataka 50/50 kwa waislamu na wakristo katika teuzi? Je ukristo wa kiongozi ndo utakuondolea umaskini? Je, uislamu wa kiongozi utakuletea huduma bora za afya? Je uislamu ama ukristo wa kiongozi utachangia kuongeza pato la taifa? Jibu ni hapana.
 
Ni kwamba unauliza maswali, lakini huyapendi majibu yangu. Unauliza maswali halafu unajijibu mwenyewe na kulazimisha niamini hivyo.
 
Ni kwamba unauliza maswali, lakini huyapendi majibu yangu. Unauliza maswali, lakini unajijibu mwenyewe na kulazimisha niamini hivyo.
Dini tuwaachie wenye dini. Namshukuru Mungu mimi sio mdini ila nachukia watu wenye udiniudini, sipendi kumsema mtu kwa sababu ya dini yake. Nina marafiki wa dini tufautitofauti, tukikukana kuzungumza hatuzungumzii kabisa mambo ya udini. Ila kiukweli watu wa dini fulani mna udini sana, hususani mnaotokea mikoa flani flani along the coast!!
 
Hakuna mafundisho katika kitabu chetu yanayotuagiza tuumie kimya kimya. Mimi ni Muislamu na nitaendelea kuwa hivyo. Dini yangu ni Uislamu.
 
Nilichokiona hapa JF ni kwamba watu wamegawanyika, haijalishi hoja ya nani ni nzito au dhaifu, lakini watu wamegawanyika. Tusiombee hali hii ikaenda hadi mitaani, ikishafika huko, hata kama serikali itafanya jema gani, bado kuna kundi kubwa tu la watu wataquestion motives zake.
Ni vizuri Serikali ikawa makini katika teuzi hizi, hapa simaanishi wateuliwe watu kwa " Quota", bali namaanisha ni lazima teuzi hizi zireflect diversity ya nchi yetu.

Chadema iliwahi kuitwa chama cha " Wakaskazini" kwa sababu ya composition ya uongozi wake, wengi kutoka mikoa ya kaskazini mwa Tanzania, Chadema kila walipokuwa wanajitetea kuwa " Wao wanaangalia ujuzi, weledi, uchapakazi n.k, na hawaangalii mtu alipotoka", hata hivyo utetezi huu haukukubaliwa na watu wote, na kwa kulitambua hili Chadema imeanza kuchukua hatua za kukifanya chama chao kiwe na sura ya Kitaifa zaidi.

Hivyohivyo na katika teuzi hizi, iwapo katika kila uteuzi, watu wenye mulelekeo fulani hawamo au wamo kwa uchache mno , japo watu hao ni sehemu ya population kubwa ya nchi hii, then ni lazima kundi hilo litajiuliza kulikoni?.

Siombei tugawanyike, Lakini serikali isipokuwa makini, hili linaweza likawagawa watu, Unfortunately siombei tufike huko, kwa sababu nchi hii ni nchi yetu sote, tunataka tufanikiwe sote, na wote tule kwa pamoja mkate wa uhuru.
 
Back
Top Bottom