Kwa hiyo haina dini halafu wakuu wa mikoa wanakuwa waislamu sita na wakristo zaidi ya ishirini. Sasa hao wakristo wamepataje uteuzi kama serikali haina dini na nafasi hazikutangazwa popote!!!
Huu udini wa Magufuli utaligawa taifa na kuvuruga umoja wa kitaifa. Toka ameanza kufanya teuzi jicho lake limeona asilimia 85 wakristo na asilimia 15 waislam. Sasa hawa wakristo wakianza kutumia vibaya madaraka na kuweka wakristo wenzao kama ilivyo Tanesco tutafika? Mimi ni mkristo ila sipendi hiyo hali
Hivi dini ndo inayofanya kazi au utendaji wa mtu. Hoja ya udini sijui nini haina mashiko kabisa
Wakati dini haitakiwi kuwa kigezo katika teuzi, ukweli utabaki kuwa Tanzania ina historia mbaya ya kushughulikia malalamiko ya waislamu.
Ushahidi wa kutosha upo na ushuhuda kutolewa na waandishi wakristo kwamba Nyerere alilibeba kanisa lake.
Pale Tanzania ilipoongozwa na Rais ambaye alikuwa ni muislamu,members wa jf wa dini ile walikuwa wanalalamikia kila teuzi ambayo mteuliwa ni mwisilamu. Kama dini si kigezo kwa teuzi ni kwa nini hili lilifanyika?
Ni wazi jamii ya Tanzania ina wananchi wengi ambao ni waumini wa dini ya ukristo na waumini wa dini ya uislamu.
Nchi nyingi zimeingia kwenye migogoro, mauaji ya kutisha na hata vita baina ya waumini wa dini hizi.
Wakati dini si kigezo cha teuzi, jambo la uwiano wa kijamii haliwezi kudharauliwa na Rais anapofanya teuzi zake. Katika dini zote hizo wapo wananchi wanaokidhi vigezo vya uteuzi kama dini si kimoja wapo.
Kukinga ni bora kuliko kuja kutibu majeraha au maradhi.
Wanaomshauri Rais wamkumbushe kwamba jamii inapitia majina ya wateule wake na yapo malalamiko kwamba teuzi zake zinaegemea zaidi kwa watu wake.
Kwa wale watakaobeza tahadhari hizi zinazotolewa na kuelekezwa kwa Mkulu , angalieni orodha ya teuzi zake na ni kwa nini wanakosekana "Kiranga/viranga" wengi katika orodha hiyo?
Kujigeuza au kujifanya mbuni si suluhisho la malalamiko yanayotolewa na kujifanya hatujali malalamiko hayo ni kutengeneza mgogoro wa kijamii kwa makusudi huku tukijua madhara yatakayotokana na mgogoro huo yatakuwa na athari mbaya na kubwa kwa jamii yetu.
Aliye na macho haambiwi tazama!
Kwakweli, aibu imewashika na udini wao, wana roho mbaya za ajabu sana, walitegemea waislamu na wao waanze kupiga kelele lakini wameona kimya nafsi zinawasuta,