Wakati dini haitakiwi kuwa kigezo katika teuzi, ukweli utabaki kuwa Tanzania ina historia mbaya ya kushughulikia malalamiko ya waislamu.
Ushahidi wa kutosha upo na ushuhuda kutolewa na waandishi wakristo kwamba Nyerere alilibeba kanisa lake.
Pale Tanzania ilipoongozwa na Rais ambaye alikuwa ni muislamu,members wa jf wa dini ile walikuwa wanalalamikia kila teuzi ambayo mteuliwa ni mwisilamu. Kama dini si kigezo kwa teuzi ni kwa nini hili lilifanyika?
Ni wazi jamii ya Tanzania ina wananchi wengi ambao ni waumini wa dini ya ukristo na waumini wa dini ya uislamu.
Nchi nyingi zimeingia kwenye migogoro, mauaji ya kutisha na hata vita baina ya waumini wa dini hizi.
Wakati dini si kigezo cha teuzi, jambo la uwiano wa kijamii haliwezi kudharauliwa na Rais anapofanya teuzi zake. Katika dini zote hizo wapo wananchi wanaokidhi vigezo vya uteuzi kama dini si kimoja wapo.
Kukinga ni bora kuliko kuja kutibu majeraha au maradhi.
Wanaomshauri Rais wamkumbushe kwamba jamii inapitia majina ya wateule wake na yapo malalamiko kwamba teule zake zinaegemea zaidi kwa watu wake.
Kwa wale watakaobeza tahadhari hizi zinazotolewa na kuelekezwa kwa Mkulu , angalieni orodha ya teuzi zake na ni kwa nini wanakosekana "Kiranga/viranga" wengi katika orodha hiyo?
Kujigeuza au kujifanya mbuni ni suluhisho la malalamiko yanayotolewa na kujifanya hatujali malalamiko hayo ni kutengeneza mgogoro wa kijamii kwa makusudi huku tukijua madhara yatakayotokana na mgogoro huo yatakuwa na athari kubwa.
Aliye na macho haambiwi tazama!