Kama Serikali ya Tanzania haina dini, Mungu anayetajwa katika wimbo wa taifa ni yupi?

Kama Serikali ya Tanzania haina dini, Mungu anayetajwa katika wimbo wa taifa ni yupi?

Naona unazidi kuendekeza unafiki wako, Kwann akiteuliwa Muislam inakuwa issue sana na kila mtu ataimba udini, akiteuliwa mkristo mnalazimisha watu wanyamaze...

Serikali Haina dini ila ratio ya 90% kwa 10% kwenye uteuzi is merely unacceptable.

Kama mtu anategemea kuwa atapewa cheo kwa sababu ni dini fulani ajiandae kuumia.Karne hii tunakoelekea hataweza ku fit popote iwe ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania.Hii dunia ni ya wachapa kazi.Ndio maana hata Magufuli aliweza kupita.Uchapakazi ndio kitambulisho kilichompa kazi.

Wale wanaotegemea uzuri wa sura(UMALAYA),UKabila,au udini watafutika kwenye faili la ajira na uteuzi FOREVER.

Ni wajibu wa dini zote kuanza kuwajenga watu wao kuwa kigezo cha wao kufika mbali ni kusoma sana na kuchapa kazi sana.Porojo za kuwajenga kuwa udini ni sifa ya wao kupewa uteuzi au ajira ni kuwapotezea muda na kuwaharibu tu waumini wao
 
Hivi dini ndo inayofanya kazi au utendaji wa mtu. Hoja ya udini sijui nini haina mashiko kabisa
 
Hivi dini ndo inayofanya kazi au utendaji wa mtu. Hoja ya udini sijui nini haina mashiko kabisa

Tatizo linakuja pale pattern ya uteuzi inavyokuwa inafanana na kujirudiarudia, inafanya watu tujiulize maswali mengi sana. Umesahau Edwin Mtei alivyodai JK kateua waislamu wengi kwenye bunge la katiba. The same Logic inatumika sasa kuuliza hizi teuzi kulikoni?
 
Tatizo ni unafiki wa wala NGURUWE, wakati wa jk mbona matamko yalikuwa mengi sana sahv kimya
Ttatizo mnapenda kubebwa bebwa,
Wanawake wabebwe kwa kupewa nafasi maalumu na nyie nao??

JK aliwajengea shule huko kwao mkoani Pwani wazee wakachoma shule, akawapelekea umeme kulikua hakuna umeme na bandari mpya mijitu siku anaondoka madarakani inamuuliza mzee unatuachaje mbona hujatufanyia la maana??

Hata JK mwenyewe alibaki amechoka.
 
Uzalendo, Elimu, Uchapakazi, Weledi havipatikani kwa watu wa dini moja.

Sema Uzalendo, Elimu, Uchapakazi, Weledi unapatikana kwa watu.Weka nukta hapo usiongeze neno wa dini zote kuna wasio na dini pia usiwanyanyapae.Wanatakiwa watu wazalendo,weledi,wenye elimu na wachapakazi.Full stop pasiongezwe kitu nyuma ya hayo.
 
Hii hoja yako ingekuwa na nguvu kama tungekuwa tunaona randomness katika diversity za watu pindi selection zinapofanyika, kwa mfano iwapo kuna teuzi Waislamu wakawa wengi, kesho katika teuzi nyingine wakawa wachache au wasiwepo kabisa, Hii ingeonekana kuwa hakuna Bias, Lakini teuzi zote wanakuwa Minority tu, Hii inazua maswali mengi sana.
Lakini pia hoja yako ingekuwa na nguvu kama watu hawajawahi kuhoji selection hizi kwa jicho la kidini, kwa mfano NSSF watu wamelia udini weeeeh eti kwa sababu na waislamu nao walianza kupewa nafasi, Au Chukulia kwa mfano Mwenyekiti mstaafu mzee Mtei alipolia na JK kwamba kateua waislamu wengi kwenye bunge la Katiba, Au kelele za watu humu JF kuwa Kikwete mdini kwa kumteua Profesa Assad!. Haya yakitokea hamuwatetei hawa watu, na nyinyi mnaungs mkono hoja au mnakaa kimya, Lakini teuzi zinapokuwa hazina waislamu wengi mnasema eti " Uzalendo, Elimu, weledi na Uchapakazi ndiyo vilivyozingatiwa na si dini ya mtu". Huu ni unafiki.
 
Kuna baadhi ya mambo c yakuhoj wala kudadis sana ukiona kaa kimya
 
Tatizo linakuja pale pattern ya uteuzi inavyokuwa inafanana na kujirudiarudia, inafanya watu tujiulize maswali mengi sana. Umesahau Edwin Mtei alivyodai JK kateua waislamu wengi kwenye bunge la katiba. The same Logic inatumika sasa kuuliza hizi teuzi kulikoni?
Ndo tatizo LA viongozi wa Africa kila raisi huvutia kwake akipata uongozi. Hizo ndo favouratism na nepotism haishangazi hata ku complain mana jk naye aliwabeba sana watu wake mfano Chuo cha Udom udini ulivotamalaki
 
akiteuliwa Muislam inakuwa issue sana na kila mtu ataimba udini.

Wewe kama ni msomi ulitakiwa uandike "baadhi ya watu akiteuliwa muislamu wanaimba udini" lakini kama wewe sio msomi ni wale wategemea kubebwa na mbeleko ya udini ndio maana unaandika "kila akiteuliwa mwislamu kila mtu anaimba udini "kama ni kila mtu ina maana ni pamoja na wewe.Kitu ambacho si kweli.Nina wasiwasi na wewe ni wale wenye elimu ya kuunga unga wanaoishi kwa fadhila za kubebwa kidini huku kichwani wakiwa weupe
 
Back
Top Bottom