Nimesoma comments za baadhi ya watu humu, ama kwa hakika baadhi ni wadini sana. Unaendekeza ubaguzi wa kidini hata umefikia hatua ya kuwazungumzia wakristo kwa kutaja vyakula wanavyokula; kwamba ni wala Nguruwe. Tambua kwamba hata hao jamaa zako pia wapo wala Nguruwe na tambua kwamba sio kila Mkristo anakula Nguruwe. Napenda kukufahamisha kwamba, RAIS anateua viongozi kulingana na sifa, majukumu, na mahitaji ya nyakati husika. Pia tambua kwamba Rais ni mwanasiasa, ana chama chake ambacho pia kina taratibu zake. Rais anazingatia Katiba na Sheria pamoja na tamaduni za Watanzania. Watanzania hatuna utamaduni wa kuendekeza udini. Tambua kwamba zipo dini nyingi sana, sio Ukristo tu na Uislamu. Hakuna hata kifungu kimoja katika Katiba na Sheria kinachosema kwamba Rais anatakiwa kuteua kwa kuzingatia DINI ya MTU. Mtu hawezi kuteuliwa eti kwa kuwa yeye ni Mkristo safi au Muislamu bora; zipo sifa za msingi na za maana zaidi ya huo UWIANO WA KIDINI UNAOZUNGUMZIA. Mwisho, nikushauri kwamba, naomba ndugu zetu Wakristo na Waislamu tukazane kuwapatia watoto wetu elimu dunia ili wawe wataalam wenye sifa bora ambazo zitawasaidia kupata fursa mbalimbali za kushiriki Ujenzi wa Taifa letu katika nafasi mbalimbali ndani ya Serikali na hata katika sekta binafsi. Tunahitaji Madaktari, Mainjinia, Manesi, Wanasheria, Wataalam wa Uchumi na Fedha na kadhalika. Naomba ya Kanisani na ya Msikitini tuyaache hukohuko kwenye Nyumba hizo Takatifu za Ibada; tumpe nafasi Rias aongoze Nchi na tusimkwamishe kwa kuanza kuingiza fikra za udini katika teuzi zake. Tanzania tumekua na Marais wa dini tofauti tangu uhuru na Marais hawa wametujengea na kudumisha undugu na umoja ambao ni muhimu sana kwa ustawi wa Taifa letu. Amani yetu ni muhimu sana kuliko dini zetu kwa sababu amani ikivunjika hakuna atakayepona, awe mkristo au muislamu au mhindu. Tuipende Nchi yetu na tutoe mawazo chanya ya kuboresha na tusipoteze muda katika hoja za kutugawa kama hili la UDINI. Mungu Ibariki Tanzania. Vumilieni!!!!!!!