Serikali haina dini wala kabila wala jinsia.Mtu yeyote anayetaka uongozi utolewe kidini,kikabila au kijinsia anachemka.Serikali ya Tanzania sio serikali ya shirikisho ya vyama vya kidini ,kikabila au kijinsia kuwa kila chama kipate mwakilishi wao humo!!!!
Tanzania waislamu wengi wako kimkoa wako mikoa mitano tu dar es salaam ,Pwani,tanga,lindi na Mtwara.Huko kwingine mikoa mingine kimkoa wengi wanakuwa ni wakristo na wapagani.
Lakini kuwaita wengi ni waislamu kwenye mikoa niliyoitaja ni kuwaonea pia sababu waislamu wa mikoa hiyo hula nguruwe pori na kunywa pombe kuanzia mnazi,gongo pombe za kisasa nk wengi ni mashahidi kwenye hili watu tunaishi nao mitaani tunawajua.
Ukisema mtu achague mwislamu mtu utakuwa unamaanishi nini? Yeye ni Mungu aangalie mwislamu kweli ni yupi na feki ni yupi?
serikali ya Tanzania si msikiti au kanisa unaotafuta maimamu au mapadri wa kusalisha serikalini maofisini.Hivyo anayetafutwa na kuteuliwa haangaliwi ni swala tano au huwa hasali anatafutwa mchapa kazi.
Wale mliozoea kupewa vyeo kwa sababu ya sigida iliyoko usoni ya kuswali Sana swala tano au kuvaa Rozali au tasbihi ndefu shingoni au mkononi ,au misalaba mingi uliyovaa shingoni hakukufanyi iwe sifa ya kuteuliwa na serikali kwenye awamu ya HAPA KAZI TU.Nenda kawaombe wakupe vyeo misikitini au makanisani.
HAPA KAZI TU sio nani dini gani.Unapotafuta mtu wa kuzoa takataka au kutapisha choo hutafuti dini gani