MgonjwaUkimwi,
Ahsante sana gwiji na karibu sana.
Nadhani hapa umeeleza kwa kirefu sana tofauti ambayo nimeizungumzia hapo juu. Sababu ya kutoa mfano wa sisi yaani waafrika kuwa vipofu tunaojaribu kwenda sambamba na demokrasia iliyoundwa kwa watu wenye vision (mabepari). Ni wakati gani bara Afrika limepoteza demokrasia yake kama sio wakati wa kutawaliwa?...Na isije kuwa hata hiyo elimu tunayopewa ni uwezo wa kutembea Ulaya na kusema sanaaa! huku tukiwa mikono mitupu...Na kama tujuavyo mkono mtupu haulambwi...Je, kuna elimu ya Uzalishaji inayomlenga kipofu!
Binafsi nakubaliana sana na maelezo yako na hata kama kuna mafunzo ktk kujenga demokrasia hii mpya, je hivi kweli hakuna haja ya kufahamu tofauti zetu na kuziacha nje zile ambazo hazimsaidii kipofu!.... sidhani kama shule ya vipofu hutumia vifaa vya elimu sawa na hivyo vya waenye kuona.
Kwa mtazamo huo, naogopa hata kusema hizi project zinazoundwa na viongozi wetu hivi kweli zimeundwa kwa kumlenga na kuzingatia upofu wetu kurahisisha hiyo transition na sio kumjaza majukumu mlemavu na kutegemea ataweza ku - perform sawa na mtu mzima. Je, serikali zetu zimeweza kuweka vipengele vya sheria za kumlinda ama kumpa unafuu kipofu?...haki inayomlenga kipofu dhidi ya mabepari.
Watu wengi tumekuwa tukizungumzia mifano ya China Urusi na nchi nyinginezo ambazo zimepiga hatua na zipo ktk kasi ya ajabu kiuchumi, lakini sote tumeshindwa kuelewa kwamba China hawakuingia Ubepari macho juu. China hawakubinafsisha mali zao za Umma kwa wageni hadi hivi majuzi tu! na miradi mingi ya wageni (foreigner) ni ile mipya ambayo wao hawakuwa nayo kama wajamaa. Urusi ambao mwanzo walipotea step na kuanza kubinafsisha kwa wageni toka mwanzo, walisimamisha zoezi hilo na kuanza kulitazama upya...Sasa hivi wanabinafsisha mali zao za Umma kwa wananchi wazawa kwanza na hao kuingia Ubia na mashirika ya nje. Na mwisho wote kwa pamoja yaani China, Urusi, Malaysia na nchi changa zote kusini mwa Asia isipokuwa India zimeweka wazawa mbele na wageni huingia ubia ama kuanzisha miradi mipya....serikali imeweka sheria kuwalinda wananchi wake (vipofu) nazo ni pamoja na kuhakikisha mzawa lazima ashike zaidi ya asilimia 50 ya shirika!... kazi sasa ipo kwa hao mabepari.. kusuka ama kunyoa!
Note this:- Hakuna hata nchi moja inayopiga hatua kiuchumi kwa kugawa mali zake kwa wageni... isipokuwa nchi za kiafrika. Yes, sisi maskini hatuna uwezo kwa hiyo pia tukumbuke hatuwezi kuchukua mifano ya wengine matajiri wanaobinafsisha mali zao kwa wazawa!... Kwa mtaji wetu huu hakuna mfano bora kabisa wa kusema mbona wale wamefanikisha?
Tanzania tumekubali kwamba sisi ni maskini na serikali tu ndio pekee yenye kiutajiri cha ushikaji.. Serikali ndiyo imeshika Ubia na wageni na sio wananchi! na ndio sababu kubwa uliyoendeleza RUSHWA nchini kwa sababu hakuna mwenye uchungu na hiyo asilimia ya serikali zaidi ya Kiongozi huyo CEO kuwa Chukua Chako Mapema (CCM).
Na mwisho ndio sababu kubwa hata yangu ku-challenge huo Uhuru wetu kwani nilitegemea Uhuru ni kuondokana na hizi imani ama mila za kikoloni ziwe kupitia dini ama Utawala na turudishe tamaduni zetu zenye demokrasia yetu ambayo wageni walitukuta nayo, kisha hapa katikati itafutwe suluhu ya mawasiliano kibiashara baina yetu.
Teh teh teh!
Mimi kubishana na mtu km wewe ni kupoteza wakati tu.
Sasa hata mimi nikitaka Kuufuata huyo UKRISTO nakuwa napata tabu sana kuueelewa kwanini UNA UONGO KUPITA KIASI?
Hebu nisaidie hapa.!
Manake huwenda we ukawa karibu na PAPA muabudu mzungu kuliko mimi.
Tazama hii sarakasi ya ANDIKO.
Michael binti wa Saul hakupata mtoto mpaka kifo chake.(2 samweli 6:23)
Michael binti wa Saul alikuwa na wavulana watano (2 Samweli 21:8)
Benjamin alikuwa na watoto watatu. (1 Mambo ya Nyakati 7:6)
Benjamin alikuwa na watoto watano. (1 Mambo ya Nyakati 8:1-2.
Harun alikufa huko Hor. (Hesabu 33:38)
Haruni alikufa huko Mosera (Kumb. 10:6)
Yehoremu alishikilia kutawala wakati akiwa na umri wa mika 32 alifariki katika miaka 40,(2 Mambo ya Nyakati 21:5) (2 Mambo ya Nyakati 21:20).
Baada ya kifo chake mtoto wake mdogo alishikilia serikali na alikuwa na umri wa miaka 42 wakati ule.(2 Mambo ya Nyakati (22:1-2).
Kana kwamba mwana mdogo alikuwa miaka miwili zaidi kuliko baba mzazi! (9. Mat 5:17; Mat 5:38-40; Hebrew 7:12).
Sungura hucheua (Mambo ya Walawi 11:6). Lakini ukweli ni kwamba Sungura hacheui kabisa.
Yuda aliyemsaliti Yesu alivitupa vile vipande vya fedha alivyopewa kwa udhalimu wake huo, kisha alijinyonga na
wakuu wa Makuhani wakavichukua vipande vya fedha na wakanunulia shamba la kuzikiwa watu (Mat 27:5-7).
Lakini (Matendo 1:18), inasema kwamba Yuda mwenyewe alinunua konde kwa ijara aliyoipata kwa udhalimu wake huo na kisha akaanguka na kupasuka na matumbo yake yote yakatoka.
Yesu alifyolewa na wanyanganyi wawili aliposulubiwa pamoja nao. (Marko 15:32 ; Mat. 27:44).
Lakini katika Luka 23:39-40, inasema kuwa mnyanganyi mmoja ndiye aliyemfyolea Yesu.
Yuda alijinyonga.(Mat. 27:5).
Lakini katika Matendo 1:18, imeandikwa kwamba alianguka na kupasuka matumbo yake
Mwanadamu aliumbwa baada ya uumbaji wa wanyama.(Mwanzo 1:25-26).
Lakini katika (Mwanzo 2:18-20), inaonekana mwanadamu aliumbwa kwanza.
Mwandishi wa Torati siye Nabii Musa mwenyewe.
Basi Musa mtumishi wa bwana akafa huko katika nchi ya Moabu kwa neno la Bwana. (Kumb. 34:5).
Mwandishi wa Kitabu cha Mathayo si Mathayo mwenyewe ambaye ni mwanafunzi wa Yesu.(Mat. 9:9).
Yaani hio ndio imani unayoita SAFI KABISA?
Teh teh teh.