Kama taarifa ya janga la korona haina umuhimu Tanzania kwanini vyombo vyetu vya habari viendelee kutoa taarifa za mataifa mengine?

Kama taarifa ya janga la korona haina umuhimu Tanzania kwanini vyombo vyetu vya habari viendelee kutoa taarifa za mataifa mengine?

Baadhi ya vyombo vya habari kama ITV na UTV hapa nchini kila baada ya taarifa ya habari hutoa summary ya mwenendo wa maambukizi ya korona duniani.

Je kuna faida au madhara gani kwa wananchi kusikia taarifa ya mwenendo wa Korona kwa mataifa ya nje tu bila kujua kinachoendelea nchini?

Je, kwanini vyombo vya habari kama ITV au TBC haviandai vipindi maalumu kuonyesha vifo na namna wanavyozika waliokufa kwa korona nchi kama Brazil na Elqurdo badala ya kutangaza namba tu na kutangaza Corona ipo chukua tahadhali?

Kama kweli taarifa za korona hazina umuhimu na hazihitajiki hapa nchini kwanini viongozi wetu wakuu kwa nyakati tofauti wiki iliyopita walipotoa taarifa ya kupungua kwa korona walitaja takwimu/namba?
Wabongo mna ujinga mkubwa sana..wao walisha wahi kupata kipindu pindu? acha wabebe msalaba wao,yani mnatamani maisha ya wazungu kiasi mnatamani mpaka magonjwa yao
 
Wabongo mna ujinga mkubwa sana..wao walisha wahi kupata kipindu pindu? acha wabebe msalaba wao,yani mnatamani maisha ya wazungu kiasi mnatamani mpaka magonjwa yao
Ulisoma baada ya kumaliza kuandika?
 
ILICHOFANYA SERIKALI NI KUWATOA HOFU WANANCHI ILA MKUMBUKE NA KUISHI KWA KUCHUKUA TAHADHARI, MAANA LAZIMA MAISHA
YAENDELEE
MNGEWEZA KUKAA LOCKDOWN MIEZI 6 NYIEEEE
AU MWAKA...
KIUKWELI KWENYE HILI SERIKALI ILICHEZA KAMA PELE

OVA

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Big up JPM and team yako
 
Lengo ni propaganda zaidi. Kujaribu kuonyesha kuwa sisi ambao hatukuchukua hatua kali tuko vizuri zaidi kuliko wao.

Kimsingi taarifa zimekaa kishabiki zaidi kuonyesha kwa majirani hali ni mbaya zaidi ndiyo maana tumewakataza wasitangaze wa kwetu kabisa hata kama wakipatikana.

Yale yale ya mbuni kujificha kwa kuficha kichwa mchangani.
 
Tena nimewasikia TBC Leo saa kumi,wanaripoti watu walioufa kwa Corona huko Brazil tena bila aibu.
 
Mkuu acha kujifanya muzungu

Africa haijaathirika na corona hata Who wamekiri hilo
Afrika sio kwamba haijaathirika bali bado hatujawapima watu wetu kwa sababu ya ukosefu wa vitendea kazi.
Kwa sababu si wote waliombukizwa na virusi vya Corona wanaonyesha dalili kwa hiyo si rahisi kuwangundua bila kuwapima.
Aidha nchi nyingi za Afrika zinategemea mashine moja kupima maambukizi vifo na waliopona ni vigumu kupata takwimu halisi zinazohusiana na ugonjwa wa Corona.
Hata hivyo takwimu za leo zinaonyesha Afrika ina maambukizi 129,620 na watu 3,795 wameshapoteza maisha.
Afrika ya Kusini ni nchi ya 30 duniani kati ya nchi zenye maambukizi makubwa ikiwa na ikiwa na maambukizi 27,403 na vifo vya watu 577.
Ugonjwa huu sio wakuchukulia kimasihara wala kubeza,ni janga ambalo inaitupasa kulichukulia kwa uzito wa kipekee.
 
Nadhan n ushamba huwez shadadia kutangaza matatizo ya wenzako na kuonesha uzto wa tatzo then kwako unafcha hili n jambo la kushangaza ,Na kama co tatzo kubwa kama tunavyoaminishwa kipi kinachotusukuma kutangaza taarifa zczotuhusu?
 
Back
Top Bottom