Kama taifa tuna katiba isiyofaa, tumuombe Mungu Rais Samia Suluhu asipate kiburi. Vinginevyo ni majanga

Kama taifa tuna katiba isiyofaa, tumuombe Mungu Rais Samia Suluhu asipate kiburi. Vinginevyo ni majanga

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2020
Posts
4,170
Reaction score
6,757
Taifa letu lina katiba mbaya sana maana imemrundikia Rais madaraka makubwa mno. Sioni umuhimu wa kutaja ibara zilizompa ais mamlaka makubwa. Lakini toka ibara ya kwanza mpaka ya mwisho rais wa JMT ana mamlaka makubwa sana. Anaweza kufanya chochota anachotaka na hakuna wa kumuuliza. Na hii huwa mbaya zaidi kama rais wetu akiwa na kiburi.

Tuna katiba ambayo imetamka wazi Rais hawezi kushitakiwa kwa jinai yoyote akiwa madarakani. Sasa je kwa kutumia madaraka yake akifanya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa nini asishitakiwe?

Tumuombe Mungu Rais wa sasa asiwe na kiburi, maana kama akiwa na kiburi, hata mtu akimtongoza binti yake tunaweza kusikia alitekwa na kufungwa jiwe zito kisha kutumbukizwa baharini. Na hakuna hatua zozote za kisheria dhidi yake zitachukuliwa.
 
Dawa ya kiburi kaburi.Amepita madrasa twaamini atalimbuka
 
Back
Top Bottom