Kama TANESCO wameshindwa kazi na wamekosa dira, kwanini wasiruhusu makampuni binafsi yagawe umeme?

Kama TANESCO wameshindwa kazi na wamekosa dira, kwanini wasiruhusu makampuni binafsi yagawe umeme?

Greataziz

Senior Member
Joined
Feb 8, 2018
Posts
124
Reaction score
99
Hili huwa najiuliza mara kwa mara Sana Naombeni JamiiForums msilichanganye kule kwenye thread ya TANESCO macomment mengi sana huenda hata hawataona maana hii imekua kero sana kwa sisi Raia.

Waziri na wizara kwa ujumla sijui kama Wana Mkakati wowote wa kuondokana na Tatizo La Mgao wa Umeme naona wapo tu wanasubiria waamke waende ofisini warudi kulala Ukiachana na Mkakati walokua nao MAGUFULI na Waziri Wake.

Hii imekua kero sana kwa sisi Raia ambao Tunategemea Umeme ili tule na wapate pesa ya kutukata TOZO kila Siku kukatika umeme kuanzia asubuhi mpaka saa 1 jioni maeneo mengi mikoani ni kero Sana hususani Mbeya Wanakata sana ni miezi 2 sasa mkoani mbeya mgao unaendelea.

Mwaka uliopita kama sijakosea viongozi wengine walisingizia Mvua na kuwa huko nyuma walikuwa wanawalazimishwa kuwasha umeme kwenye miundombinu mibovu, Wakazima muda mrefu kuwa wanakarabati tukasema sawa sasa sijui mwaka huu wameandaa Sababu gani zingine najua fika watasema ni VITA ya UKRAINE maana mtu wa kumtupia tena lawama hayupo sidhani kama itawezekana kupata wa kumrushia lawama.

Swali langu kwanini wasiruhusu Makampuni mengine yatuuzie umeme kama ilivo simu Ttcl wameboresha sana Huduma baada ya kupata washindani zamani walikua wanaringa sana na huduma mbovu.

Na kama Waziri amekosa dira na mkakati wowote wa kuondokana na mgao anasubiria kila mwaka aandae sababu za kutuambia ndio chanzo cha mgao basi apishe wenye uwezo huo watekeleze.
 
Katika idara inayoongoza kwa wizi na ufisadi hapa nchini namba moja ni idara ya nishati.
Hivyo wanasiasa wetu kamwe hawawezi kukubali kuona idara hiyo inapata ushindani toka kwenye makampuni binafsi ili waendelee kufaidi keki ya taifa.
 
Na siku wakiruhusu makapuni menginee yasambazee umeme ,nazani tanesco ndio itakuwa mwisho wao ..
 
Na siku wakiruhusu makapuni menginee yasambazee umeme ,nazani tanesco ndio itakuwa mwisho wao ..
Bora iwepo hivyo hivyo kuliko isipokuwepo kabisa, isipokuwepo tutalia na kusaga meno. Hoa mabwana umeme wanaoitumia tanesco kuhujumu nchi iwapo tanesco itondoka watakuwa na access ya moja kwa moja kuwahujumu raia na hatutawafanya chochote.
 
Tuliza mshono, watu wauze majenereta.
Aiseee unanifumbua macho Kumbe ni mkakati wa kuuza jenereta ila haya mambo hayakuwepo wakati wa Kaleman na Magufuli mgao wa umeme ulikuwa ni historia walipoingia tu huyu waziri ndio tumeanza kuona hili tatizo la mara bwawa limekauka mpaka anachukua ndege kupiga picha....
 
Na siku wakiruhusu makapuni menginee yasambazee umeme ,nazani tanesco ndio itakuwa mwisho wao ..
Bora tutaamua sisi tuchague Tanesco au kampuni ingine inayotoa huduma bora na wao wataamka na kuacha kufanya kazi kimazoea, kama nanunua unit moja kwa 350 na bado huduma mbovu nikiuziwa na kampuni ingine unit 1 kwa 450 ila umeme wa uhakika sioni hasara
 
aliye mteua waziri, waziri mwenyewe, mamenaja wa tanesco (walio wengi) uwezo wao uko chini sana
 
tulia tulia, mabwawa yamekauka
Kama mabwawa yakikauka yote nchini manake tutakua gizani milele manake uongozi hauna mkakati wala dira wanaenda tu kama kichwa cha mwendawazimu maana kila mwaka ni mgao mgao hamna mbinu za kuja na mkakati wa kutatua hili watasema VITA ila licha ya VITA wenzetu umeme haukatiki hovyo
 
Poleni sana...

Ngoja waje kukupa muongozo kwa kukuomba number yako ya siku na location...
 
Back
Top Bottom