Kama Tanzania ina amani kwanini viongozi mnatuweka foleni mpite?

Mpondoshilla

Member
Joined
Jul 4, 2022
Posts
36
Reaction score
132
Jana nikiwa nimetoka zangu katika mihangaiko mida ya saa nane hivi kufika pale uwanja wa ndege gari zikawa foleni tumekaa hapo weee nikaona madereva wanazima magari mara konda kakaa mlangoni miguu ikiwa chini ya lami tukawa tunajiuliza kuna nini?

Kama nusu saa hivi tukasikia
Wioo wiooo wiooo wiooo
Aa kudadeki kumbe ni kakiumbe kamoja tu kametoka zake sijui wapi huko kanatusimamisha maelfu ya watu ili kapite

Kwanini wasikae tu pamoja kwenye foleni na sisi?
 
Duu hili jina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…